Sina uhakika ni lini alifariki lakini hadi mwishoni mwa mwaka 1999 nilikuwa najua kuwa alikuwa amefariki, huenda ni mwaka huo ama kabla.
Nachojua hakuwahi kubadili jina. J
ina Mohammed Hussein lilikuwa ni la kumshabikia aliyewahi kuwa mchezaji nyota wa Bandari ya Mtwara, Yanga na Simba, Mohammed Hussein "Mmachinga." Wakati John Kaduma akichora jarida la Tabasamu, crew ya jarida hilo ilikuwa ikijipigia chapuo kuwa inatumia mtindo wa wachezaji uwanjani wa 4-4-2 waliokuwa wakiuita
"Samba Msele" na ndiyo maana John Mathias Kaduma alijipa jina la mcheza mpira.
Majina mengine ya bandia ya John Kaduma yalikuwa,
- Fogasta
- John Black
- Baba Jack (Jina la bintiye Jacqueline)
- Tanzania One
Wimbi la Kitintale nakumbuka aliyechora ni Chrisantus Katembo (Chris Katembo). Wakati huo naona Kaduma hakuwa na amani katika Sani hasa baada ya kufariki Said Mbwana Makatta Bawji aliyekuwa kiongozi na mtunzi wa Hadithi Mahiri kama
Maji Mazito na Kizaizai iliyokuwa na akina Mayuku, Zumo, Mzee Ole, Obi, Linda na Seba.
Kaduma ameathiri sana mtindo wa uchoraji wa wasanii wengi wa Tanzania, miongoni mwao ni mimi. Nafikiria namna fulani ya kurudisha nguvu/kumbukumbu zake japo kidogo but in a modern way.
Tunawamiss Born Town, Bush Stars, Makwekwe. Tunawamiss Ndumilakuwili (Profesa), Madenge, Kipepe, Bob Mazish, Lodi Lofa, Pimbi, Mzee Mwalubadu, Kizibao, Wanzuki n.k.
Tunakumbuka kosa alilofanya Mzee Mwalubadu kulazimisha Kizibao apangwe matokeo yake akasababisha penati iliyofanya Bush Stars wafungwe.
Siku hiyo Ndumilakuwili hakusema "Yan Kibadachi, Yan Shodan Kataa!"
RIP John M. Kaduma.