John Cheyo: Mazungumzo ya maridhiano kuendeshwa kwa gredi yaani ya 'ukubwa' wa vyama viwili tu siyo sahihi

17 February 2023

Mzee John Cheyo - Hili la vyama vinavyojiita Chama Tawala na Chama Kikubwa kuteka agenda za nchi halikubaliki

Mwenyekiti wa chama cha UDP Mh. John Cheyo alalamika siasa kuwekwa "gredi" vyama gani vinaweza kujadili katiba ya nchi, maana kwa sasa suala hili linajadiliwa na vyama viwili tu kimoja kinajiita ni tawala na kingine ni chama 'kikubwa' huku vyama vingine vinavyoitwa vya mfukoni vikiachwa nje ya mjadala huu mkubwa.

Mzee Cheyo anasema umri wake umamueleza kuwa leo chama kinaweza kuwa kikubwa na tawala lakini kesho kikawa kidogo hivyo ikitokea mazungumzo muhimu je chama hicho huko miaka ijayo kitabaguliwa ?

Anaongeza kuwa ustaarabu wa kisiasa uwe katika nyanja zote na siyo lugha tu. Hili la ukubwa na huyu mtawala haikubaliki hivyo baraza la vyama la siasa lipewe hatamu na jukumu la kuongoza mazungumzo yatayojumuisha vyama vyote badala ya vyama viwili kujifungia chumbani bila wananchi kushirikishwa na ushirikishwaji ndiyo people's power ya wale rafiki zetu.

Mkongwe huyo wa siasa anasema maisha ni magumu ni katika mifuko yao wananchi inayosababishwa na bei ya mafuta kupanda. Hivyo hii ya serikali kuamua kuagiza mchele kutoka nje haitasaidia kupunguza bei ya mchele dukani.

Jibu la kukabiliana na mfumuko wa bei ni kutumia neno moja tu ruksa la rais mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi na hivyo bulk procurement ya wachache kuagiza (kununua) mafuta ndiyo mzizi wa mfumuko wa bei /root cause ya mfumuko wa bei unaonufaisha wanunuzi wachache wa mafuta kupitia bulk procurement.

Ruksa ya Mzee rais Ali Hassan Mwinyi kuacha milango wazi kwa kila kitu ndiyo jibu endelevu / sustainable la kukabiliana na mfumuko wa bei hivyo EWURA na TBS wabaki kuwa wasimamizi wa ubora wa bidhaa na baada ya hapo bei ya mafuta itakuwa chini ya Tshs 2,000 kwa lita na hili litapelekea mfumuko wa bei wa kila kitu nchini kwenda chini na maisha kuwa nafuu.

Wafanyabiashara wa vitu na bidhaa zote hata mafuta lazima wawe wengi na ndiyo unafuu kwa maisha ya wananchi utapatikana, hii zimamoto ya kusimamia bei ya mafuta au kuagiza mchele toka nje kukabiliana na ughali wa maisha siyo suluhisho la kudumu.

John Cheyo mfanyabiashara wa siku nyingi anasema watanzania zaidi ya nusu hawaishi mashambani, bali wanaishi mijini na shamba lao ni mifukoni hivyo mchele toka Katavi, Shinyanga na Mbeya kuwa juu kwa walaji wa mijini unasababishwa na bei ya juu ya nishati ya mafuta ya dizeli na siyo vinginevyo pia wala ruzuku haitasaidia jibu ni neno ruksa kuruhusu biashara huria ya wafanyabiashara wengi wa biashara za ndani na nje.

Mzee John Cheyo anafurahishwa na waziri wa kilimo Hussein Bashe kutoyumbishwa na mbinyo wa kelele za kutoa bei elekezi kwa mazao ya wakulima au kufunga mipaka wakulima kuuza soko la nje. Mazao ni Mali ya wakulima anasisitiza Mzee John Cheyo na hiyo ndiyo sera ya UDP ya kuwajaza mapesa watanzania ikiwemo wakulima.

Hilo umeliona sasa Bw. Cheyo? Kitoe Chama chako mfukoni na ukipandishe kiwe chama kikuu Cha upinzani nchini nawe ufurahie kukeba ajenda zote za upinzani nchini😊
 
Kama kawaida JamiiForums tofauti na media zingine Tanzania, hutoa nafasi sawa kupitia unlimited airtime kwa vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa kutupia sera zao JF au kufungua verified account za wasemaji wa chama jukwaani. Kisha wasomaji JamiiForums kutoa mawazo huru au kuhoji kwa kifu yao bila uoga.

Vyama vingine visijitie unyonge wakati nafasi ya kuongea na umma mpana zaidi ya walio chumbani au baraza la vyama vya siasa upo hapa JamiiForums wamwage sera, mapendekezo na agenda zitakazogusa mustakabali wa nchi hii yetu sote upo.
Wadanganye, watakimbia mchana kweupe
 
17 February 2023

Mzee John Cheyo - Hili la vyama vinavyojiita Chama Tawala na Chama Kikubwa kuteka agenda za nchi halikubaliki

Mwenyekiti wa chama cha UDP Mh. John Cheyo alalamika siasa kuwekwa "gredi" vyama gani vinaweza kujadili katiba ya nchi, maana kwa sasa suala hili linajadiliwa na vyama viwili tu kimoja kinajiita ni tawala na kingine ni chama 'kikubwa' huku vyama vingine vinavyoitwa vya mfukoni vikiachwa nje ya mjadala huu mkubwa.

Mzee Cheyo anasema umri wake umamueleza kuwa leo chama kinaweza kuwa kikubwa na tawala lakini kesho kikawa kidogo hivyo ikitokea mazungumzo muhimu je chama hicho huko miaka ijayo kitabaguliwa ?

Anaongeza kuwa ustaarabu wa kisiasa uwe katika nyanja zote na siyo lugha tu. Hili la ukubwa na huyu mtawala haikubaliki hivyo baraza la vyama la siasa lipewe hatamu na jukumu la kuongoza mazungumzo yatayojumuisha vyama vyote badala ya vyama viwili kujifungia chumbani bila wananchi kushirikishwa na ushirikishwaji ndiyo people's power ya wale rafiki zetu.

Mkongwe huyo wa siasa anasema maisha ni magumu ni katika mifuko yao wananchi inayosababishwa na bei ya mafuta kupanda. Hivyo hii ya serikali kuamua kuagiza mchele kutoka nje haitasaidia kupunguza bei ya mchele dukani.

Jibu la kukabiliana na mfumuko wa bei ni kutumia neno moja tu ruksa la rais mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi na hivyo bulk procurement ya wachache kuagiza (kununua) mafuta ndiyo mzizi wa mfumuko wa bei /root cause ya mfumuko wa bei unaonufaisha wanunuzi wachache wa mafuta kupitia bulk procurement.

Ruksa ya Mzee rais Ali Hassan Mwinyi kuacha milango wazi kwa kila kitu ndiyo jibu endelevu / sustainable la kukabiliana na mfumuko wa bei hivyo EWURA na TBS wabaki kuwa wasimamizi wa ubora wa bidhaa na baada ya hapo bei ya mafuta itakuwa chini ya Tshs 2,000 kwa lita na hili litapelekea mfumuko wa bei wa kila kitu nchini kwenda chini na maisha kuwa nafuu.

Wafanyabiashara wa vitu na bidhaa zote hata mafuta lazima wawe wengi na ndiyo unafuu kwa maisha ya wananchi utapatikana, hii zimamoto ya kusimamia bei ya mafuta au kuagiza mchele toka nje kukabiliana na ughali wa maisha siyo suluhisho la kudumu.

John Cheyo mfanyabiashara wa siku nyingi anasema watanzania zaidi ya nusu hawaishi mashambani, bali wanaishi mijini na shamba lao ni mifukoni hivyo mchele toka Katavi, Shinyanga na Mbeya kuwa juu kwa walaji wa mijini unasababishwa na bei ya juu ya nishati ya mafuta ya dizeli na siyo vinginevyo pia wala ruzuku haitasaidia jibu ni neno ruksa kuruhusu biashara huria ya wafanyabiashara wengi wa biashara za ndani na nje.

Mzee John Cheyo anafurahishwa na waziri wa kilimo Hussein Bashe kutoyumbishwa na mbinyo wa kelele za kutoa bei elekezi kwa mazao ya wakulima au kufunga mipaka wakulima kuuza soko la nje. Mazao ni Mali ya wakulima anasisitiza Mzee John Cheyo na hiyo ndiyo sera ya UDP ya kuwajaza mapesa watanzania ikiwemo wakulima.
MAMLUKI KAZINI WANAPANGA KUVURUGA MARIDHIANO hiki chama ni Miongoni mwa Vyama VISIVYO vya UPINZANI mnamkumbika huyu Mzee wakati wa Utawala KATILI wa MAGUFULI alivyokuwa anaendesha SIASA ZAKE?
Anatafuta UCHAWA kwa MAMA kwani NJAA ni KALI
 
Hakuna chama cha upinzani kisicho cha mfukoni

USSR
Sasa mbona JPM mpaka aliapa kukiua CDM? Kama CDM ni cha mfukon kwann alipambana nao? Teka, tesa, uaaaa, filisi, wape kesi uhujumu,na kibaya zaid baada ya kuwanunua CDM akawapa na nafas za uongoz!!! Je ukijichunguza maneno yako huoni kama unaupungufu wa ubongo?
 
Kuna vyama vilianzishwa kama biashara ya kupata pesa za ruzuku n.k.
Hata kauli mbiu zao zinajifafanua mfano huyu MAPESA, kuna mwingine UBWABWA.
SASA lazima apige yowe akiona posho za vikao zinampita.
Wapi vyama vingine hajashirikishwa, alie juu ataonekana tu, au alitaka viwe vinatajwatajwa kama Chadema. Dawa ni kuwa na wanachama wengi, hao ndio watakaokisemea chama.
Chadema kilianzishwa kama nini?
 
Hv mnajadiliana nn na chama chenye wanachama wawili?? Yaani mume ndo mkiti Taifa, na mke ndo Katibu mkuu Taifa.. chama ambacho hakina kbs mtandao wa wanachama popote, kimeshindwa kuwashawishi hata majirani kujiunga nacho... Mzee cheyo na UDP yake ni ccm kwa 100% .. sasa wanaitwaje kwenye kujadiri katiba mpya wkt vinawakilishwa na baba yao ccm???
 
17 February 2023

Mzee John Cheyo - Hili la vyama vinavyojiita Chama Tawala na Chama Kikubwa kuteka agenda za nchi halikubaliki

Mwenyekiti wa chama cha UDP Mh. John Cheyo alalamika siasa kuwekwa "gredi" vyama gani vinaweza kujadili katiba ya nchi, maana kwa sasa suala hili linajadiliwa na vyama viwili tu kimoja kinajiita ni tawala na kingine ni chama 'kikubwa' huku vyama vingine vinavyoitwa vya mfukoni vikiachwa nje ya mjadala huu mkubwa.

Mzee Cheyo anasema umri wake umamueleza kuwa leo chama kinaweza kuwa kikubwa na tawala lakini kesho kikawa kidogo hivyo ikitokea mazungumzo muhimu je chama hicho huko miaka ijayo kitabaguliwa ?

Anaongeza kuwa ustaarabu wa kisiasa uwe katika nyanja zote na siyo lugha tu. Hili la ukubwa na huyu mtawala haikubaliki hivyo baraza la vyama la siasa lipewe hatamu na jukumu la kuongoza mazungumzo yatayojumuisha vyama vyote badala ya vyama viwili kujifungia chumbani bila wananchi kushirikishwa na ushirikishwaji ndiyo people's power ya wale rafiki zetu.

Mkongwe huyo wa siasa anasema maisha ni magumu ni katika mifuko yao wananchi inayosababishwa na bei ya mafuta kupanda. Hivyo hii ya serikali kuamua kuagiza mchele kutoka nje haitasaidia kupunguza bei ya mchele dukani.

Jibu la kukabiliana na mfumuko wa bei ni kutumia neno moja tu ruksa la rais mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi na hivyo bulk procurement ya wachache kuagiza (kununua) mafuta ndiyo mzizi wa mfumuko wa bei /root cause ya mfumuko wa bei unaonufaisha wanunuzi wachache wa mafuta kupitia bulk procurement.

Ruksa ya Mzee rais Ali Hassan Mwinyi kuacha milango wazi kwa kila kitu ndiyo jibu endelevu / sustainable la kukabiliana na mfumuko wa bei hivyo EWURA na TBS wabaki kuwa wasimamizi wa ubora wa bidhaa na baada ya hapo bei ya mafuta itakuwa chini ya Tshs 2,000 kwa lita na hili litapelekea mfumuko wa bei wa kila kitu nchini kwenda chini na maisha kuwa nafuu.

Wafanyabiashara wa vitu na bidhaa zote hata mafuta lazima wawe wengi na ndiyo unafuu kwa maisha ya wananchi utapatikana, hii zimamoto ya kusimamia bei ya mafuta au kuagiza mchele toka nje kukabiliana na ughali wa maisha siyo suluhisho la kudumu.

John Cheyo mfanyabiashara wa siku nyingi anasema watanzania zaidi ya nusu hawaishi mashambani, bali wanaishi mijini na shamba lao ni mifukoni hivyo mchele toka Katavi, Shinyanga na Mbeya kuwa juu kwa walaji wa mijini unasababishwa na bei ya juu ya nishati ya mafuta ya dizeli na siyo vinginevyo pia wala ruzuku haitasaidia jibu ni neno ruksa kuruhusu biashara huria ya wafanyabiashara wengi wa biashara za ndani na nje.

Mzee John Cheyo anafurahishwa na waziri wa kilimo Hussein Bashe kutoyumbishwa na mbinyo wa kelele za kutoa bei elekezi kwa mazao ya wakulima au kufunga mipaka wakulima kuuza soko la nje. Mazao ni Mali ya wakulima anasisitiza Mzee John Cheyo na hiyo ndiyo sera ya UDP ya kuwajaza mapesa watanzania ikiwemo wakulima.

Kiinimacho cha muafaka kinaendelea.
 
UDP siku zote inaiunga mkono CCM hivyo automatically interest zao zinalindwa na CCM katika maridhiano hayo Mzee atulie hana jipya
 
Chama ambacho Uchaguzi ukifika kinatangaza kuwaunga mkono Wagombea wa chama kingine

Kweli kabisa, maana ile dhana muhimu ya chama chochote cha siasa dhumuni lake nambari moja ni kuchukua dola na uongozi wa nchi, hiki chama UDP kinaonekana hakina matamanio hayo zaidi ya kusindikiza wengine kwa kutoa matamko ya kusifu, kusujudu na kuwaunga mkono.

Toka maktaba:

Jumamosi, Februari 18, 2023 Local time: 15:14
HABARI

Chama cha UDP chadai maandamano ni uchochezi, uvunjifu wa amani​

11 Machi, 2018

1676722587683.png

Mwenyekiti wa chama cha upinzani UDP nchini Tanzania John Momose Cheyo amesema Jumapili maandamano yaliyopangwa kufanyika April 26, 2018 ni uchochezi na uvunjifu wa amani na kwamba, mambo yanayolalamikiwa yangeweza kutatuliwa kupitia mabaraza ya vyama vya siasa.

Maandamano hayo kwa mujibu wa Cheyo yanaratibiwa kupitia mitandao ya jamiii, gazeti la Mwananchi limeripoti.
Rais John Magufuli

Rais John Magufuli

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alivionya vyama vya siasa na wananchi ambao wamepanga kufanya maandamano.

Rais aliwataka waliojiandaa kutekeleza mpango waache mara mora vinginevyo watashughulikiwa.

“Nchi hii ni ya amani, ndiyo maana uvunjifu wa amani ulipoanza kutokea kule Kibiti tuliamua kuufuta mara moja. Kuna watu wanadhani tunafanya siasa kila wakati, kama wametumwa na baba zao kuandamana, watawasimulia vizuri.

Kwa mujibu wa maelezo ya Cheyo mabaraza ya vyama vya siasa yakitumika kikamilifu yanaweza kuondoa malalamiko ya wananchi na viongozi wa upinzani.

"Tusitake kufika hatua ya kuandamana barabarani ili kudai haki, Katiba mpya, Tume huru ya uchaguzi. Tukifikia huko amani iliyopo Tanzania tutashindwa kuipata tena na wananchi watakosa nchi nyingine yenye amani ya kukimbilia," amesema.

Gazeti la Mwananchi limeripoti kuwa Bw. John Cheyo alisema kama tatizo ni fedha kwa ajili ya mabaraza hayo kukutana, Rais John Pombe Magufuli anapaswa kutoa fedha kuyawezesha kufanya vikao.

"Siungi mkono hoja za kudai kuwepo mikutano ya hadhara hata kama ni kwa ajili ya kuongeza wanachama kama wanavyodai wengine, naamini kwa sasa mitando ya kijamii ina nguvu kuliko kitu chochote nchini," amesema Cheyo.

Amesema kabla ya kudai haki ya kuandamana, zipo nyingine wananchi wapaswa kuzipa kipaumbele zikiwemo haki ya kuishi, kupata maji safi na salama, elimu na afya.

"Hatuwezi kufika mahali tuseme nchi hii imepotea na hakuna demokrasia kisa tumekosa haki ya kuandamana, haki ya kufanya mikutano ya hadhara. Kila mtu alishuhudia mikutano ya kampeni za uchaguzi wa ubunge wa marudio katika majimbo ya Kinondoni na Siha ilivyogeuka sehemu ya kutukanana," amesema Cheyo.

"Kama kitu mnachokidai kiliweza kusababisha watu kugombana na askari hadi mauaji yakatokea hicho kitu hakitusaidii kama nchi," amesema Bw. John Cheyo.

Cheyo ameongeza yanayodaiwa kwa nguvu hayana faida na manufaa ya kila siku kwa sababu watu wanahitaji kupata wakati wa kulima na kuvuna.

"Hiyo mikutano iliyoshupaliwa sasa na kuhitajika kwa nguvu zote si kweli kwamba kila siku watakuwa barabarani kuhutubia wananchi, fedha tutatafuta saa ngapi, tutalima saa ngapi, hivyo ni vyema tutambue kila kitu kinachofanyika kupitia mambo ya siasa kisiwe kisingizio cha kusema nchi haina amani, haina uhuru," amesema Cheyo.

Amesema viongozi wa dini wanapaswa kuwa kiunganishi cha wananchi na viongozi wa vyama vya siasa na si kufanya kinyume cha hilo.
Source : VOA Swahili
 
16 February 2023

HASHIM RUNGWE - WAKUU WA WILAYA WAFUTWE, MAGARI YA V8, HELA WANAZIIBA SERIKALI

Kiongozi wa CHAUMMA party Mzee Hashim Rungwe kuwa matumizi ni makubwa mno land cruiser zote hizi hakuna ktk serikali hata za hapa Kenya na Zambia ...... Nyerere mwenyewe alistuka ndiyo maana hakuhamia Dodoma aliona mambo yanabadilika kwa kasi anaongeza kufafanua Mwenyekiti wa CHAUMMA party msomi advocate wa Mahakama Kuu, mfanyabishara wa muda mrefu kuwa miaka hii ya 2023 mafaili yote ya kazi za wizara na mashirika yapo ktk viganja vya mkononi kupitia simu, tablets na kompyuta hivyo hakuna haja ya kwenda Dodoma .....
Source : EastAfricaTV
 
15 February 2023

Said Soud Said mwenyekiti wa AAFP Taifa - Msiwe Mnamkimbiza rais wetu kwa misafara ya kasi

Sera yetu kubwa ni Siasa na Watu hivyo AAFP tunajikita zaidi ktk watu baada ya mikutano ya hadhara kuanza tena hivyo kama chama tunadhamana ya kuongea kwa niaba ya watu ambao ni wakulima, wavuvi, wafugaji, wafanyabiashara ili utajiri wa nchi hii utasaidia kuondoa maadui watatu wakuu yaani ujinga maradhi na umasikini.

Nchi hii si masikini ni tajiri hivyo tutatetea wanyonge nasi AAFP tupo katika mkondo huo kuwasemea wananchi masikini, wajinga na waliosongwa na maradhi huku nchi inanuka njaa bila sababu .... huku mawaziri, wabunge na viongozi wa serikali kwa mamia wanakula viyoyozi ..

Watu hawali chakula mpa usiku wamegeuka kuwa kama mnyamandege popo kutokana na ughali wa maisha .....

Awataka wasaidizi wa mheshimiwa rais wasimwendeshe resi / kasi Rais Samia Hassan ktk misafara yake ili apate wasaa angalau wa kuteremka kutoka ktk gari aulize bei ya mchele au kusikiliza vilio vya wananchi kuhusu ugumu wa maisha ...

Mwenyekiti huyo wa AAFP taifa amesema raia wanampenda sana rais wa jamhuri ya muungano hivyo wasimnyime nafasi asitembee kwa miguu mara kwa mara ili ajue maisha yakoje nchini ..... AAFP Alliance for Tanzania Farmers Party

Back
Top Bottom