17 February 2023
Mzee John Cheyo - Hili la vyama vinavyojiita Chama Tawala na Chama Kikubwa kuteka agenda za nchi halikubaliki
Mwenyekiti wa chama cha UDP Mh. John Cheyo alalamika siasa kuwekwa "gredi" vyama gani vinaweza kujadili katiba ya nchi, maana kwa sasa suala hili linajadiliwa na vyama viwili tu kimoja kinajiita ni tawala na kingine ni chama 'kikubwa' huku vyama vingine vinavyoitwa vya mfukoni vikiachwa nje ya mjadala huu mkubwa.
Mzee Cheyo anasema umri wake umamueleza kuwa leo chama kinaweza kuwa kikubwa na tawala lakini kesho kikawa kidogo hivyo ikitokea mazungumzo muhimu je chama hicho huko miaka ijayo kitabaguliwa ?
Anaongeza kuwa ustaarabu wa kisiasa uwe katika nyanja zote na siyo lugha tu. Hili la ukubwa na huyu mtawala haikubaliki hivyo baraza la vyama la siasa lipewe hatamu na jukumu la kuongoza mazungumzo yatayojumuisha vyama vyote badala ya vyama viwili kujifungia chumbani bila wananchi kushirikishwa na ushirikishwaji ndiyo people's power ya wale rafiki zetu.
Mkongwe huyo wa siasa anasema maisha ni magumu ni katika mifuko yao wananchi inayosababishwa na bei ya mafuta kupanda. Hivyo hii ya serikali kuamua kuagiza mchele kutoka nje haitasaidia kupunguza bei ya mchele dukani.
Jibu la kukabiliana na mfumuko wa bei ni kutumia neno moja tu ruksa la rais mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi na hivyo bulk procurement ya wachache kuagiza (kununua) mafuta ndiyo mzizi wa mfumuko wa bei /root cause ya mfumuko wa bei unaonufaisha wanunuzi wachache wa mafuta kupitia bulk procurement.
Ruksa ya Mzee rais Ali Hassan Mwinyi kuacha milango wazi kwa kila kitu ndiyo jibu endelevu / sustainable la kukabiliana na mfumuko wa bei hivyo EWURA na TBS wabaki kuwa wasimamizi wa ubora wa bidhaa na baada ya hapo bei ya mafuta itakuwa chini ya Tshs 2,000 kwa lita na hili litapelekea mfumuko wa bei wa kila kitu nchini kwenda chini na maisha kuwa nafuu.
Wafanyabiashara wa vitu na bidhaa zote hata mafuta lazima wawe wengi na ndiyo unafuu kwa maisha ya wananchi utapatikana, hii zimamoto ya kusimamia bei ya mafuta au kuagiza mchele toka nje kukabiliana na ughali wa maisha siyo suluhisho la kudumu.
John Cheyo mfanyabiashara wa siku nyingi anasema watanzania zaidi ya nusu hawaishi mashambani, bali wanaishi mijini na shamba lao ni mifukoni hivyo mchele toka Katavi, Shinyanga na Mbeya kuwa juu kwa walaji wa mijini unasababishwa na bei ya juu ya nishati ya mafuta ya dizeli na siyo vinginevyo pia wala ruzuku haitasaidia jibu ni neno ruksa kuruhusu biashara huria ya wafanyabiashara wengi wa biashara za ndani na nje.
Mzee John Cheyo anafurahishwa na waziri wa kilimo Hussein Bashe kutoyumbishwa na mbinyo wa kelele za kutoa bei elekezi kwa mazao ya wakulima au kufunga mipaka wakulima kuuza soko la nje. Mazao ni Mali ya wakulima anasisitiza Mzee John Cheyo na hiyo ndiyo sera ya UDP ya kuwajaza mapesa watanzania ikiwemo wakulima.
Uzee bwana, asha sahau yeye ni CCM...Mwenyewe ushajikatia tamaa kujiweka fungu la vyama vya mfukoni wacha tujadili tutakupa mrejesho
Roho ya Shetani isivyo na aibu, akawageuka wenzie..Sasa mbona JPM mpaka aliapa kukiua CDM? Kama CDM ni cha mfukon kwann alipambana nao? Teka, tesa, uaaaa, filisi, wape kesi uhujumu,na kibaya zaid baada ya kuwanunua CDM akawapa na nafas za uongoz!!! Je ukijichunguza maneno yako huoni kama unaupungufu wa ubongo?
Uchaguzi uliopita kituo alichopiga kura Cheyo na mkewe walipata kura 1 na hakuna iliyoharibika... akili mu kichwa...Hv mnajadiliana nn na chama chenye wanachama wawili?? Yaani mume ndo mkiti Taifa, na mke ndo Katibu mkuu Taifa.. chama ambacho hakina kbs mtandao wa wanachama popote, kimeshindwa kuwashawishi hata majirani kujiunga nacho... Mzee cheyo na UDP yake ni ccm kwa 100% .. sasa wanaitwaje kwenye kujadiri katiba mpya wkt vinawakilishwa na baba yao ccm???
Kila mjadala wa katiba ukifika mnaanza kutisha watu mara mabeberu, mara ushoga utaingizwa kwenye katiba mara muungano utavunjwa!! Why? Mbona mara ya mwisho mlifuta maoni yote ya Warioba mkaweka yenu? Kwani mtashindwa kufuta hizo "ajenda" za mabeberu?Bila ya mantiki...
Kwenye maridhiano kuhusu Ukweli na Haki Yafanyike baada ya Rais SSh kuwa nje ya Nyadhifa yake. Iwe ni 2025 au 2030.... Ikiwa na maana waliohusika kwa namna moja au nyingine wawe nje ya mfumo unaoweza legeza Haki kutendeka. Wawepo nje ya mapazia.
Vilevile Kuhusu Katiba
Vyama vikubaliane kwa pamoja, watoe tamko la pamoja kulinusuru Taifa hili kutoka kwa mikono ya mabeberu na Vibaraka hai wa Ukoloni Mamboleo, ambao wansubiri kwa hamu kutumia mwanya unaojitokeza kupenyeza Ajenda zao.
Kwa sasa bunge linaweza kujikita kuboresha kanuni za Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi.
Naungana na Mzee Mapesa, Kwani
Sioni sababu ya kuharakisha mambo muhimu ya Taifa kwasababu ya Majabali wawili wa CHADEMA. Ikiwa ni pamoja na CCM? mapendekezo ya Mzee Mapesa yazingatiwe.
TL, Mbowe, Ndio tunawaonea huruma ya mateso mliyopata, lakini kwa sasa kuna mamluki na vibaraka wa mabeberu wanaotaka kutumia mwanya huu kuweza kuingiza ajenda zao, je mnataka kwenda na historia kama wawezeshaji? Sidhani.
Upo uwezekano wa vishinikizo.?..sawa, tunaheshimu Demokrasia? basi, tuanze kwenye vyama vya Siasa vyote nchini....kabla hatujaenda na hayo Kitaifa. Wakati huo tukiwa tunalinda a "Sovereign State"
Tutafika,
Kitaeleweka
.
15 January 2023
Makambako, Iringa
UJENZI WA OFISI YA KUBWA YA CHAMA CHA CHADEMA JIMBO LA MAKAMBAKO UNAENDELEA KWA KASI
Mikutano ya hadhara itakuwa katika eneo hili na ujenzi unaenda kwa kasi kukaribisha na kupokea ugeni wa kitaifa toka makao makuu ya CHADEMA.
Wanachama jimbo la Makambako wamesema wanajitolea kwa moyo mmoja huku wakiwa na furaha kwa kutembea vifua mbele kukijenga chama kwa ajili ya kizazi cha sasa na kizazi kinachokuja ...
Tena ni wananchi wenyewe wanajitolea kwa hali na mali huku wakiwa na furaha kubwa wa mchango wao kuleta mabadiliko ya kisiasa TanzaniaChadema ipo very organized nafurahi
Ukubali au usikubali ila Gwajiboy alikuwa mkubwa kwa mikakati zaidi yakoNaunga mkono hoja
P