Johari anaswa...

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126




Na Richard Bukos
Blandina Chagula ‘Johari’, mdada anayetengeneza mkate wa kila siku kupitia Tasnia ya Filamu Bongo, amenaswa akiwa kwenye mazingira tata, saa 9:18 usiku, Jumapili iliyopita.
Johari, alikuwa ametinga kiwalo kinachomuacha nusu uchi, huku chini yake kukiwa na ‘ganda la kiroba’, ikidaiwa kwamba alitoka kujichochea sekunde chache kabla.

Tukio hilo, lilichukua nafasi kwenye Baa ya Meeda, Dar es Salaam ambako Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kujinafasi’, ilikuwa ikiangusha burudani yenye afya.

KUNA KITU NDANI YA JOHARI
Gazeti hili lilimkuta Johari amejiinamia, akiwa mnyonge mithili ya kifaranga kilichokosa mama, hali ambayo ilionesha kwamba alikuwa mbali kwa mawazo.
Mwanga wa kamera, wakati akifotolewa na paparazi wetu ndiyo uliomshtua na kusababisha awe mkali kama pilipili kichaa.

Hata hivyo, baadaye paparazi wetu alimtuliza Johari kwamba hakuwa akihitaji picha mbaya, isipokuwa ya pozi kwa ajili ya matumizi mazuri ya kiofisi.

Ombi hilo, Johari alilipokea lakini pamoja na kuonesha utulivu, bado sura yake ilithibitisha kuwa na kitu kinachomsumbua ndani kwa ndani.

JOHARI KIMYAA
Baada ya kukubali kupiga picha ya pozi, Johari aligoma kujibu maswali ya paparazi wetu na mara nyingi alikaa kimya kama hajasikia alichoulizwa.

Paparazi wetu alijitahidi kumhoji Johari kwa kila njia ili aseme kilichokuwa kinamsumbua lakini hakupata mafanikio.

PAPARAZI ADAIWA
Johari alipoondoka, mhudumu wa baa hiyo alimvaa paparazi wetu na kumdai kwamba amesababisha mteja wake aondoke.

“Yule Johari ni mteja wetu, pale alikuwa anakunywa kiroba, kikaisha akaagiza kingine, wakati anakisubiria, wewe ukafika na kuanza kumpiga picha. Nilipotaka kumletea akakataa kwa sababu yako, sasa naomba ulipe,” alisema mhudumu huyo.

Hata hivyo, paparazi wetu alikuwa imara, aligoma kulipa kwa maelezo kwamba Johari anayemfahamu siyo mlevi na huwa hanywi viroba.

RAFIKI AZUNGUMZA
Shosti wa Johari (jina tunalo) aliliambia gazeti hili: “Kuna kitu kinamsumbua Johari. Hivi sasa hayupo sawa ndiyo maana alikutwa Meeda usiku akiwa katika hali hiyo.

“Unajua Johari ni mtu safi, ni mrembo anayejiheshimu lakini kuna mambo yanamchanganya, ni mambo binafsi lakini huo ndiyo ukweli. Kusema ukweli rafiki yangu anahitaji msaada.”

KUTOKA RISASI
Gazeti hili linamshauri Johari atulize akili, anaweza kuwaona wataalamu wa saikolojia ili waweze kumsaidia. Tunamfahamu ni mwanamke anayejiheshimu na uwezo wake wa kisanii ni mkubwa. MHARIRI.

Picha bonyeza hapa Chanzo JOHARI ANASWA... - Global Publishers
 
Back
Top Bottom