Jogoo hawiki lakini ana watoto wawili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jogoo hawiki lakini ana watoto wawili

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Hmaster, Mar 30, 2011.

 1. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Filauni! Nilikuwa na mpangaji mwenzangu katika nyumba moja Dar. Jamaa alikuwa ni rafiki yangu sana na alitokea kuniamini sana kwani alikuwa ananihadithia mambo mengi sana. Hata akipata utata wa jambo furani hakusita kuniomba ushauri kwa vile hata kielimu mimi nipo juu kiasi. Pamoja na kazi nzuri aliyonayo huyu jamaa sikumuona hata siku moja akiwa bize na wakinadada zaidi ya kutaniana nao tu hapa na pale. Akirudi kazini, alitumia muda mwingi kutazama tv, kupika, kuoga na hatimaye kulala. Mimi nilimsifia sana kwa hali hiyo si unajua mtu kujiheshimu. Kutokana na hali hiyo niliogopa hata kumweleza miadi yangu ya kujirusha kwa kuogopa jamaa ataniona namna gani.
  Kuna siku tulitoka kwenda kutazama mechi ya mpira kiwanjani na wakati wa kurudi mi nilimueleza mwenzangu huyo kwamba atangulie home kwani mimi nilikuwa na miadi na mtu hivyo namsubiri baa furani. Jamaa akanieleza kwamba naye angenifuata kwani ana mazungumzo na mm. Tukaenda na tulipokuwa hapo alinipa A to Z ya hali yake tangu apate ujana. Jogoo wake anawika akiwa peke yake lakini akiwa na mtetea anakaa kimya hata siku nzima. Ndo maana akaachana na mitetea kwa kuogopa kudhalilika. Akaniomba ushauri, nikamwambia aende kwanza hosp. Akaenda akatibiwa kln tatizo bado. Huku na huku lakini wapi na umri wake sasa ni miaka 39. Mwisho hata kunieleza maendeleo yake akawa haniambii na akawa kama ananikwepa kwa aibu na mwisho akahamia sehemu nyingine na mawasiliano yakafa.
  Jambo la kushangaza ni kwamba katika kipindi cha miaka takribani mitatu hivi tuliyopotezana tulikutana maeneo flani akiwa na mwanamke akiwa na mtoto mgongoni huku na yeye kamshika mwingine na kuniambia huyo ni mke wake na hao ni watoto wake. Nikashangaa sana na mwisho nikawapongeza, sikuweza kumuhoji kitu. Je inawezekana alipona au "kapewa alee"
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Ulivyohadithia it sounds like tatizo lake lilikuwa ni la kisaikolojia, na sio la kimaumbile. Mtu kama huyo akipata counselling an kuishinda hofu yake, na kakutana na mwanamke ambaye ni mwelewa na supportive...basi huwa anachapa kazi bila tatizo lolote. Kama huyo mwanamke kweli ni mkewe, ina maana yuko comfortable naye na atakuwa ametulia kiakili kiasi cha kuweza kuperform poa tu. So kuna uwezekano ni kweli hao ni wanae...unless, alikuwa jogoo hawiki kabisaaa na akakudanganya.
   
 3. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Ndani ya siku moja lolote linaweza tokea na mtu akapona kabisa maradhi yake. Kama uliachana naye kwa miaka mitatu ni kipindi kirefu sana cha kupata tiba.
  Hao watakuwa watoto wake vinginevyo kwa sababu anajua unajua hali yake ungegundua tu wasiwasi wake na kutotulia wakati anakuintrodyuzi kwa shemeji.
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Halikuwa tatizo kubwa sana, hata Mkuyati huenda ulisaidia.
   
 5. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,197
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hizo ni siri zake binafsi.

  Kama ameamua alee mwache aendelee sio kila mtu anataka kulea damu yake ati.

  Mimi binafsi naona kama haituhusu mpaka aje kuomba ushauri mwenyewe.
   
 6. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Unajua huyo alikuwa anasumbuliwa na wasiwasi tu, labda sasa alipopata mwanamke wa kuishi nae akamzoea sana mpaka woga ukaisha kwa hiyo mambo yake yakawa murua
   
Loading...