Lord OSAGYEFO
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 3,086
- 4,881
WAJUMBE MPAKA WATISHWE NDIO WAPITISHE BAJETI YA CHAMA
Spika wa Bunge, Job Ndugai amewaambia Wabunge kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 90(2)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Tanzania ana uwezo wa kuvunja Bunge endapo litakuwa limekataa kupitisha bajeti ya serikali iliyopendekezwa.
Ameyasema hayo leo, Juni 22 ambayo ni siku ya kuhitimisha bunge la Bajeti. Ambapo kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Kanuni 229 wabunge wanapiga kura za wazi kwenye kupitisha bajeti hiyo.
Kwa mwaka wa fedha 2021/22 Serikali imependekeza bajeti ya Tsh. Trilioni 36.26