JNIA among Africa's worst airports

JNIA among Africa's worst airports

Naona watu wanaoitetea JNIA hakuna viwanja vingine wamefika zaidi ya vile vinavyotumiwa na fastjet
 
air.jpg

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki amesema uwanja wake umechakaa kiasi cha kukosa sifa za kuwa uwanja wa kisasa barani Afrika na dunia.

Kauli ya Malaki imekuja baada ya ripoti ya matokeo ya utafiti wa mtandao wa Sleeping in Airport uliyofanywa 2014 kuonyesha kuwa JNIA inashika nafasi ya nne kwa viwanja duni Afrika.

“Huo ni ukweli usiopingika kwa sababu uwanja ulijengwa zamani na miundombinu yake haikidhi mahitaji ya sasa…. hali ni mbaya,” alisema Malaki.

“Kiwanja kinakabiliwa na tatizo la miundombinu chakavu, vyoo visivyotosheleza na wakati huohuo kuzidiwa na wingi wa abiria, jambo linalosababisha huduma zake kuwa chini ya kiwango.

“Hatuwezi kuwa bora kwa uwanja huu… hebu fikiria uwanja uliojengwa kuhudumia watu milioni 1.2 kwa mwaka, sasa unahudumia watu 2.5 milioni, hapa lazima huduma zitakuwa chini ya kiwango na msongamo utakuwa mkubwa.”

Alisema katika kukabiliana na changamoto ya msongamano, ofisi yake iko katika hatua za kuongeza vizimba vya kugongea hati za kusafiria kutoka saba vya sasa na kuwa 21.

Alisema tayari wameshazungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani kwa ajili ya kuongeza wafanyakazi, pia kuunganisha na kuwa sehemu moja kwa mlango wa abiria wanaowasili na wa ndani, kazi itakayokamilika wiki mbili zijazo.

Utafiti

Utafiti wa Sleeping in Airport ulitokana na maoni ya wasafiri waliopitia uwanja huo ambao walielezea na kupiga kura kuhusu huduma, miundombinu na uwezo wa viwanja hivyo kutumika kama eneo la kulala wasafiri inapobidi.

Nafasi ya kwanza kwa uduni ilishikwa na uwanja wa kimataifa wa Khartoum, Sudan ukifuatiwa na N’dijili, Kinshasa DRC na Tripoli Libya nafasi ya tatu.

Katika taarifa yake, mtandao huo ulisema Afrika ina sifa ya kuwa na viwanja vingi vyenye sifa mbaya duniani, ikiwemo uchafu wa sakafu, vyoo, vitendo vya rushwa, ukosefu wa viyoyozi licha ya joto kali, migahawa ya kawaida lakini ghali na michakato ya usalama inayotia shaka.

Chanzo: Mwananchi
 
Uwanja wa ndege wa Dar si mbaya kama inavyofikiriwa ila kuna mambo ambayo yanaushusha hadhi kama ifuatavyo"

  • Chemba za maofisa wa uhamiaji check in/check out ni chache.
  • Sehemu ya Abiria kupokelea mizigo ni ndogo.
  • Vyumba vya abiria kusubiria kupanda ndege ni ndogo.
  • Hakuna usafiri wa mabasi ya abiria wa kawaida toka airport isipokuwa ghali kwa kutumia cab.
  • Parking ya magari ni ndogo mno na ni kero, nashangaa bustani kubwa ya maua na kuimwagilia badala ya kuweka parking ya magari.
  • Usubumfu ukiingia kuteremsha abiria hata kwa dakika mbili lazima utozwe kodi jambo ambalo airport nyingine ruksa kwa dakika 20 kushusha na kuchukua abiria.
  • Vyoo licha kuwa safi ni vichache mno.
  • Kutoruhusiwa wasafiri wanaounganisha usafiri kubaki uwanjani jambo ambalo huwaletea usumbufu na gharama zisizokusudiwa, viwanja vingi huruhusuwa kama Ethiopia airport kuna vitanda vya kulala uwanjani hadi raha.

Kinachoshusha hathi ya uwanja huo si uchafu tukilinganisha na viwanja vingine, isipokuwa hayo hapo juu na mengine ambayo wadau wanayajua. Kumbuka waliolalamikia na kutoa hitimisho hilo ni wasafiri ambao wanapounganisha usafiri hulala airport.
  • Mara moja nimelala Ethiopia airport kusubiria kuunganisha usafiri.
  • Mara tatu nimelala Dulles international airport, Washington DC, Marekani nikisubiria ndege kuunganisha.
Mara zote hizo sijapata usumbufu wala kuulizwa na kufuatwa na mtu mradi abiria ameteremka toka kwenye ndege na hajatoka nje ya airport. Dar ni usumbufu mtupu.

Kwamba uwanja ulijengwa siku nyingi ni hoja dhaifu, mbona Nairobi, Ethiopia, Heathrow (UK) na vinginevyo ni vya zamani kuliko wetu?

Abiria wa ndege hawahitaji maua yale pale mbele ya airport, panueni parking ya magari.
 
CCM imetufikisha hapa tulipo!! Inamaana hata Uwanja wa Mogadishu Somalia ni bora kuliko wa Dar es Salaam!!

Kama unaitakia Tanzania mema KATAA CCM

KATAA CCM
TANZANIA IPONE
 
Uwanja wa ndege wa Dar si mbaya kama inavyofikiriwa ila kuna mambo ambayo yanaushusha hathi kama ifuatavyo"
Chemba za maofisa wa uhamiaji check in/check out ni chache.
Sehemu ya Abiria kupokelea mizigo ni ndogo.
Parking ya magari

Hivi unaweza ukadiriki kusema uwanja wetu ni mzuri kweli??? Unalinganisha na uwanja gani? Hivi umetembea duniani na kuona viwanja bora vya ndege au unaropoka tu..?? Huo uwanja ni kama kituo cha daladala...

Huwa najisikia vibaya ninaposhuka na ndege, then jirani yako anakuuliza.. Huu ndiyo Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam..?? Huwa natoa jibu kwa huzun sana!!
 
Hivi unaweza ukadiriki kusema uwanja wetu ni mzuri kweli??? Unalinganisha na uwanja gani? Hivi umetembea duniani na kuona viwanja bora vya ndege au unaropoka tu..?? Huo uwanja ni kama kituo cha daladala...

Huwa najisikia vibaya ninaposhuka na ndege, then jirani yako anakuuliza.. Huu ndiyo Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam..?? Huwa natoa jibu kwa huzun sana!!

Ukubwa wa uwanja si ubora wa uwanja, ila huduma mbalimbali ndizo zinazokuwa kigezo cha ubora wa uwanja. Huwazi niambia uwanja wa Dar ni mdogo kuliko viwanja vingine vyote vya kimataifa barani Afrika.

Kwa uchafu uwanjani sina hamu katika moja ya terminal pale Ethiopia inayosafirisha abiria sehemu mbalimbali Afrika. Waithiopia wamejitahidi usafi terminal ya kusafirishia abira nje ya bara la Afrika.
 
Tuvumilie, Terminal III inajengwa kwa kasi sana. Ipo siku nitasimama pale nichukue picha mbili tatu hivi
 
Tuvumilie, Terminal III inajengwa kwa kasi sana. Ipo siku nitasimama pale nichukue picha mbili tatu hivi

Najua inajengwa na nimeona inaenda kwa kasi, lakini kinacholalakimikiwa si kuongeza terminal, ila huduma kama nilivyoainisha hapo juu. Terminal II kuna eneo kubwa sana lipo tupu na lingine limepandwa maua tu badala ya kujenga parking za magari.
 
Back
Top Bottom