JM Luxury coach: Mbadala wa Scandinavia Express

JM Luxury coach: Mbadala wa Scandinavia Express

Kasahau 5 alliance na Mtoto wa Mwanza pia wapo vizuri. Na kwa kusafiri kwangu maeneo mengi naamini Mtwara ndio sehemu yenye asilimia 90 ya mabasi ambayo ni mazuri na hayana ubabaishaji.

observation yako ni ukweli mtupu. nilimuambia Mtu mmoja kusini kuna magari ambayo ni luxury kuliko hata barabara ya Dar Arusha.
 
ama hakika gas ni kichocheo cha maendeleo kusini.sikutegemea itafika siku moja mtu ataleta tangazo kutangaza bus zake zinazoenda kusini mwa tz.ni kiashirio tosha kwamba sasa kusini ni lulu kibiashara na ushindani ni mkubwa.

wamakonde akina THE BIG SHOW fungeni mkanda, punde kidogo wachaga,wasukuma,wahaya,wanyakyusa,wangoni nk watawaheshimu.lol

shikamoo gas.

Nimekusoma Mkuuu.

Wa mwisho atakuwa wa kwanza.

Imeshaandikwa hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Scandinavia haitakaa itokee Tanzania tena. Sijui mzee Mohamed ameanzisha biashara nyingine
That was the bus. Dar Bukoba kwa passport. Dar Musoma kwa passport. Dar Nairobi. Dar Mombasa. Dar Tanga. Dar Arusha name it na route hiyo walikwenda ispokua Mtwara maana hakukua na abiria wenye hadhi ya kupanda MARCO POLO ANDARE CLASS

Yaani wewe kaka ni zaidi ya Zombie. Yaani Mtwara watu wanapanda ndege tangu enzi hizo halafu washindwe kupanda basi? Kukariri ni jambo baya sana. Badala ya kuwa realistic kuwa wakati ule barabara haikuwa nzuri kupeleka basi Luxury badala yake unaleta porojo! Ndo shida ya kusadiki mambo ya kuambiwa na wewe bila utafiti unameza kama lilivyo, halafu unakuja kudanganya jamvini humu

Huo ni uongo wa mchana kweupe!?
 
Kaniudhi sana huyo mtu eti hatukuwa na hadhi ya kupanda scandivia, kwa lipi la ajabu walilokuwa nalo..!!
 
Yataje hayo ya Dar Arusha halafu weka picha. Kampuni zake zinafahamika: Dar Express, Kilimanjaro, Ngorika, Sai Baba. Yote tunayafahamu. Ni Yutong, Benz na Scania- ambazo zimechoka.
Tuje Dar Mtwara ni Maning Nice, Machinga, 5 Alliance, MJ Luxury, Hamanj na mengine mengi. Kama tungeweza kupata picha za mabasi hayo ya route hizo( Yaani Dar- Arusha City na au Dar-Mtwara Municipality tungeondoa ubishi) . Ila sasa route za kusini mabasi mazuri ni Dar Mtwara na kidogo Dar Masasi, ila wilaya zingine magari hayaridhishi, tofauti na kaskazini kule karibia kila wilaya mabasi ni mazuri kiasi
 
observation yako ni ukweli mtupu. nilimuambia Mtu mmoja kusini kuna magari ambayo ni luxury kuliko hata barabara ya Dar Arusha.

Ni ubishi usio na tija , kuna watu humu wanajifanya wajuaji sana.Kazi kumeza kila wanalosimuliwa bila kuhakiki. Ukweli ulio wazi ni kuwa Dar-Mtwara ndo kuna basi luxury na standard bora kuliko sehemu yoyote kuanzia Dar.
 
Tashirifu pia inatoa huduma nzuri kwenda Tanga kunani bila kusahau Bazuu v.i.p
 
Kaniudhi sana huyo mtu eti hatukuwa na hadhi ya kupanda scandivia, kwa lipi la ajabu walilokuwa nalo..!!

Nimewahi kupanda route ya Dar Iringa, Dar Dodoma na Dar Arusha! Hakuna tofauti ya hali ya u luxury tofauti na yale ya Dar Xpress. Tofauti yao kubwa ilikuwa ni umakini na kwamba muda ukifika hataka kama abiria ni kumi, basi linaondoka.

Lakini eti uniambie ndege zote zinazoenda Mtwara eti basi liwe bora kuliko ndege ni kichekesho. Itakumbukwa kabla ya uwanja wa ndege wa pale Songwe Mbeya uwanja wa ndege wa Mtwara ulikuwa namba nne: JNIA, KIA, Mwanza Airport na Mtwara Airport.
Ni zombie na anaetumia kinyesi tu ndo anaweza kusema usafiri wa basi ni luxury kuliko ndege!
 
Ni ubishi usio na tija , kuna watu humu wanajifanya wajuaji sana.Kazi kumeza kila wanalosimuliwa bila kuhakiki. Ukweli ulio wazi ni kuwa Dar-Mtwara ndo kuna basi luxury na standard bora kuliko sehemu yoyote kuanzia Dar.

Sema tumekosa picha tu. Yangechukuliwa mabasi kumi ya kampuni moja moja ya Route ya Dar- Arusha halafu Dar Mtwara tupime yap ni mazuri. Kiukweli ile route ina mabasi mazuri. Lakini hata Mbeya kuna mabasi mazuri
 
Kweli bhana nkuu, picha zingeongea zaidi. Halafu hilo jina lako linanikumbusha miaka dahali nyuma nishakula sana nikiwa Msimbati.
 
Nilipoambiwa na Rafiki yangu mmoja ambaye amepangiwa kituo cha kazi kusini mwa Tanzania kule Gas inapochimbwa Mtwara aliniambia kama naenda niwe makini kuchagua usafiri mzuri, vile sikuwa na uzoefu kusafiri mikoa ya kusini alinipa option ya magari/kampuni kama 3hivi machinga, maning nice na jm luxury na kuniambia kati hizo akaniambia nenda kachukue tiketi za jm, nilimuulza mbona mabasi hayo ni mageni njia hii? Akanijibu "ah hawa jamaa wapo kwenye game /huduma muda mrefu"

Nilichokikuta kwenye mabasi njiani tukienda mtwara.
kwanza nilipenda matangazo ya awali safari inapoanza likiwemo la kufanya sala, pili jamaa wanakuwa smart kwenye uniform na mabasi yao, pia issue ya uchafu kwamba mtu ukila usitupe nje uchafu -hii nimeipenda ila kwa mfumo wa ndugu zangu watanzania bado inasumbua wengi maana mpaka mwisho wa safari niliona wengine wamepewa mifuko ya uchafu lakini wakawa wanatupa ndani.ya bus, lililonifurahisha jamaa wanakataza abilia kusimama kuwahi mlangoni kushuka kabla bus halijasimama, hii imekaa vyema maana tatizo laweza kutokea bila hodi, nk.
Mwisho nilimpa big up driver na conda wake kwa hali ile walikuwa na bus lenye namba T956 CGK.

IN TAKE yangu angalieni msije.kuwa nguvu za soda maana mkisha nogewa tu mnajisahau, kwani tulikuwa na scandinavia jamaa walikuwa wazuri sana maana.hata abilia 5 gari inasonga mbele.

Na je,.mmekuwa mbadala au ni kipindi then mnahama biashara.

JM ni gari zinazoongoza kutokuwa na mvuto kwa abiria!
 
Ni kwel hao jamaa uliowataja wako vizuri. Mabasi ni mengi na tena yanaenda hadi kule kanda ya nyanda za juu kusini. Inasemekana ni tajiri kutoka Mbeya kama sikosei. Kwa kifupi, siku hizi ukiwa unaenda Mtwara unachagua tu aina ya basi na muda gani usafiri. Kuna route ya saa12, 4, 5,7 na saa9 alasiri. Ukitoka saa 9 saa4 usiku ushaingia Dar au Mtwara.
Ni mwanzo mzuri kuelekea maendeleo kule kusini ya Tanzania

Kaka, kwa mabasi haya sijawahi dhani kuwa yapo mengi mpaka nyanda za juu kusini, ukizingatia mimi kwetu ni Tanga hivyo kama yapo huko nafhani utatupa hisia zako kwa kile nilichosema pale juu.
 
Kaka, kwa mabasi haya sijawahi dhani kuwa yapo mengi mpaka nyanda za juu kusini, ukizingatia mimi kwetu ni Tanga hivyo kama yapo huko nafhani utatupa hisia zako kwa kile nilichosema pale juu.

Yako mengi sana tena mapya kabisa. Yako kituo cha mafuta pale makutano ya Mandela road na Taifa road karibu na Uwanja wa Uhuru na Taifa. Ni mengi mno! Route ya Mbeya ndo hasa ilikoanzia
 
Jm kwa kweli wako vizuri iringa na mbeya pia ndio wanaoenda vizuri
 
JM ni gari zinazoongoza kutokuwa na mvuto kwa abiria!

Hahahaaa...:O lengo langu siyo mabasi kukosa abilia, lakini kama na wewe ulitaka kujua kuhusu abilia siku ile niliyosafiri na bus lile lilikuwa limejaa hivo cjaona kiti kilichokuwa wazi.
La muhimu ni kile nolichovutiwa nacho nikiwa safarini, na kwa taarifa yako nilifuatilia kwa abilia wenzangu baadhi wakaniambia au kupingana na kauli yako kuwa hayana mvuto ila walisema kati ya mabasi pendwa mbeya na iringa no JM LUXURY COACH.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom