JKT yatangaza nafasi za kujiunga kujitolea

JKT yatangaza nafasi za kujiunga kujitolea

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,123
Reaction score
3,511
Wakuu,

Tukajitolee kujenga taifa jamani:Alien::Alien::Alien:

----------

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, amewahimiza vijana wa Kitanzania wenye sifa kujitokeza kujiunga na nafasi za kundi la kujitolea.

Mpango huu unalenga kuwajengea vijana uzalendo, umoja wa kitaifa, pamoja na kuwapatia mafunzo ya stadi za kazi na maisha ili wawe na utayari wa kulitumikia taifa lao.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Mkuu wa Tawi la Utawala, Brigedia Jenerali Hassan Mabena, ameeleza utaratibu wa kuomba nafasi hizo kwa vijana wenye nia. Alisisitiza kuwa mafunzo haya ni fursa muhimu kwa vijana kupata ujuzi utakaowasaidia kujitegemea na kuchangia katika ujenzi wa uchumi wa nchi.

Aidha, Brigedia Jenerali Mabena amewataka vijana watakaoteuliwa kuhakikisha wanaripoti makambini kwa wakati kuanzia Februari 27 hadi Machi 4, 2026.

Hatua hii ni sehemu ya maandalizi ya awali ili kuanza mafunzo hayo ya kijeshi na stadi za kazi kama ilivyopangwa katika kalenda ya JKT kwa mwaka huu.


tole​
 
Wanatafuta namna ya kuwapunguza uraiani.

Huko unakula kile mnachozalisha. Kimsingi hakuna tofauti na maisha ya mtaani.
 
Vijana waende tu ili wakajionee mauzauza ya huko lakini wakatae kuajiriwa huko maana jeshi limekuwa la kiwendawazimu.
 
Mafunzo ya uuwaji na sisi wapi na wapi, acha niendelee na utakatifu wangu hapa MT Andrew.
 
Bora ujipigie vibarua vyako mtaani huku ukisoma ramani ya wapi utoboe
 
Kuna miradi mingi ya wakubwa huko JKT
Kama una mtoto au ndg usijaribu kumpeleka huko
ni bora umpeleke VETA

Ataenda kutaabika tu na kuharibikiwa akili!
 
Ningekua mm ndio raisi, nakamata anko t, nakamata Noel, nakamata juma lokole, nakamata coca. Alafu nawapeleka huko kwa lazima, mambo mengine tunayalea wenyewe tu
 
Back
Top Bottom