JKT wasogeza mbele tarehe ya kuripoti makambini kutoka tarehe 05 hadi tarehe 07 Juni 2016

Uncle Elroy

JF-Expert Member
May 22, 2016
1,174
1,086
MABADILIKO YA TAREHE YA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT KWA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2016.

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linautangazia umma mabadiliko ya tarehe ya kuripoti makambini vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2016 na
kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2016.

Taarifa ya awali kwa vyombo vya habari nchini iliainisha tarehe ya kuripoti kuwa ni tarehe 01 June hadi tarehe 05 Juni 2016.

Tarehe hiyo imefanyiwa mabadiliko badala yake vijana hao wanatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 07 June hadi tarehe 10 June 2016
bila kukosa.

Atakayesikia tangazo hili amtaarifu na mwezie.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 31 Mei 2016
 
MABADILIKO YA TAREHE YA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT KWA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2016.

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linautangazia umma mabadiliko ya tarehe ya kuripoti makambini vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2016 na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2016.

Taarifa ya awali kwa vyombo vya habari nchini ilianisha tarehe ya kuripoti kuwa ni tarehe 01 June hadi tarehe 05 Juni 2016. Tarehe hiyo imeafanyiwa mabadiliko badala yake vijana hao wanatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 07 June hadi tarehe 10 June 2016 bila kukosa.

Atakayesikia tangazo hili amtaarifu na mwezie.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano

Makao Makuu ya JKT

Tarehe 31 Mei 2016
 
Labda tusubiri Tu ,Hata wao wanafahamu ,Pengine wana mkakati tofauti kwa Mwaka huu...Hata mimi sifahamu, Ila maadm na wao Ni watu wenye uelewa...Tungoje tuone!
 
Wakati wa kuomba mkopo ukifika huwa wanaruhusiwa kurudi nyumbani wanaapply then wanarudi vikosini kazi za watu zinaendelea
ohoo mkopo unaapply before hujaenda jkt na kurudi nyumbani huwaga kuja kuapply vyuo,sasa turudi round mbili serkal yenyew haina hela
 
Na Vipi kuhusu nakala ya vyeti vya kuzaliwa na vyeti vya kidato cha Nne??Kama vinahitajika katika kutuma maombi ya mkopo...hii ina maana watakao kwenda Jeshi inabidi waende na nakala hizo???Kwa maana kama wataruhusiwa kutuma maombi wakiwa Jeshini...na ukute mtu Hana nakala yoyote!!!!
 
ILA kama watatoa fomu mapema ,kabla watu hawajaanza kuripoti itakuwa vyema...ama sivyo watatoa taarifa ili ijulikane cha kufanya...ama sivyo wao wanaelewa ...pengine Mambo yamebadilika kwa Mwaka huu....Tuishi kimazoea..
 
Na Vipi kuhusu nakala ya vyeti vya kuzaliwa na vyeti vya kidato cha Nne??Kama vinahitajika katika kutuma maombi ya mkopo...hii ina maana watakao kwenda Jeshi inabidi waende na nakala hizo???Kwa maana kama wataruhusiwa kutuma maombi wakiwa Jeshini...na ukute mtu Hana nakala yoyote!!!!
km ndoivo inabd waeke mahakama yakuapia pamoja na mtendaji Wa kata
 
Back
Top Bottom