JKT wametangaza nafasi za Kujiunga kwenye Mafunzo kwa Vijana wa Kidato cha Sita waliohitimu mwaka 2024

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
941
613
JKT LAWAITA VIJANA WA KIDATO CHA SITA MAKAMBINI

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, tarehe 24 Mei 2024, ametangaza nafasi za Kujiunga kwenye Mafunzo kwa Vijana wa Kidato cha Sita waliohitimu mwaka 2024.

Akitoa tangazo hilo kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Mkuu wa Tawi la Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa, Brigedia Jenerali Hassan Mabena, ameelekeza Wahitimu hao wa Kidato cha Sita 2024, waripoti kwenye Makambi ya JKT yaliyokaribu nao kuanzia tarehe 01, Juni 2024 hadi tarehe 07, Juni 2024. Aidha kwa wahitimu wenye uono hafifu au ulemavu (Physical disabilities) wakaripoti Kambi ya Ruvu JKT iliyoko Mkoani Pwani

Akizungumza na Wanahabari, Makao Makuu ya JKT, jijini Dodoma, Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema, taarifa zaidi kuhusu Vijana walioteuliwa, Vifaa na Makambi wanayopaswa Kwenda kuripoti zinapatikana kwenye tovuti ya jkt.go.tz
IMG-20240525-WA0016.jpg
IMG-20240525-WA0013.jpg
IMG-20240525-WA0014.jpg
IMG-20240525-WA0015.jpg
 
Back
Top Bottom