JKT: Mchezo wa ndama utaamsha madume

JKT: Mchezo wa ndama utaamsha madume

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,255
Reaction score
16,185
Mwili ulinisisimka nilivyoona na kusikia kuwa "askari" waliomaliza mafunzo ya JKT bila kupatiwa ajira rasmi wanataka kuandamana kuelekea Ikulu. Mmmh, nikasema sasa huu ni ukurasa mpya katika historia ya majeshi yetu hapa nchini.

Askari hawa wamepata wapi ujasiri wa kuandamana kwenda Ikulu kuonana na Amiri jeshi mkuu? nani yuko nyuma yao? utamaduni huu wameupata wapi?

Kwanini wasingeazia kwa Mkuu wa majeshi kwanza kabla ya kwenda kwa Amiri jeshi mkuu?. Kama kweli vijana hawa watafanikisha malalamiko yao kwa njia hii basi iko siku "kaka zao" pia walioko kambini wanaweza kufuata njia hii hii ya kudai malalamiko yao, maana inawezekana na wao wanayo malalamiko makubwa pengine kuzidi haya ya "wajukuu zao" yaani mchezo wa ndama wanaocheza mchezo wa kupigana ndani ya zizi unaweza kuamsha hamu na hamasa ya madume nayo kuanza kupigana.
Hatua tunazoziona sasa dhidi yao ni jitihada za kuwatenganisha ndama kwa kuwatoa zizini na kuwavisha kamba shingoni na kuwafunga kwenye vigingi juani ili waache kucheza mchezo wao huu hatari kwa usalama wa zizi na ng'ombe wengine (give a dog a bad name and ......)

Ni vema suala la vijana hawa wa JKT lichambuliwe kwa kina bila kutoa majibu ya juujuu na ya hasira. Inavyoonekana malengo ya mafuzo yao ya JKT hayakueleweka vema kwao, au yuko mtu aliyekiuka maagano au yuko mtu nyuma yao anawashauri vibaya
 
Serekali izuwie wasije uziwa viwembe maana utakuwa mwanzo wa kununuwa mapanga.....
 
Mwili ulinisisimka nilivyoona na kusikia kuwa "askari" waliomaliza mafunzo ya JKT bila kupatiwa ajira rasmi wanataka kuandamana kuelekea Ikulu. Mmmh, nikasema sasa huu ni ukurasa mpya katika historia ya majeshi yetu hapa nchini.

Askari hawa wamepata wapi ujasiri wa kuandamana kwenda Ikulu kuonana na Amiri jeshi mkuu? nani yuko nyuma yao? utamaduni huu wameupata wapi?

Kwanini wasingeazia kwa Mkuu wa majeshi kwanza kabla ya kwenda kwa Amiri jeshi mkuu?. Kama kweli vijana hawa watafanikisha malalamiko yao kwa njia hii basi iko siku "kaka zao" pia walioko kambini wanaweza kufuata njia hii hii ya kudai malalamiko yao, maana inawezekana na wao wanayo malalamiko makubwa pengine kuzidi haya ya "wajukuu zao" yaani mchezo wa ndama wanaocheza mchezo wa kupigana ndani ya zizi unaweza kuamsha hamu na hamasa ya madume nao kuanza kupigana.

Ni vema suala la vijana hawa wa JKT lichambuliwe kwa kina bila kutoa majibu ya juujuu na ya hasira. Inavyoonekana malengo ya mafuzo yao ya JKT hayakueleweka vema, au yuko mtu aliyekiuka maagano au yuko mtu nyuma yao anawashauri vibaya.

Wadau;
Tukumbuke kuwa JK mwenyewe alipokuwa anatetea udhalimu wa CCM na Serikali yake ktk kupindisha na kuangamiza Mependekezo ya ktk RASIMU YA 2 ya Tume ya Warioba iliyopendekeza Serikali 3, akiwa Bungeni Dodoma, JK alitisha watu kuwa ndani ya Serikali 3, endapo Wanajeshi hawatapata Maslahi yao wanavyotaka, wataandamana mabarabarani kwenda Ikulu, na Vifaru na Serikali itavunjika! Maneneo hayo hayo yalirudiwa na Mteule mwingine wa Ikulu, William Lukuvi, na pia viongozi kadhaa wa CCM wa ngazi za juu walitishia kila mara!...Wao waliyasema hayo yote wamesahau kuwa kudai HAKI haina cha aina ya serikali iliyopo madarakani, kama ni 3, 2 au 1! Kama mnadanganya wananchi na Vijana wetu walio JKT na msipoenda vyema haraka, hata wale walio kambini nao watafuata HAKI hadi Ikulu...! Hiyo haitakuwa sababu ya Serikali 3, bali ni kutokana na uovu wa watawala. Viongozi wetu wanatafuta shida wenyewe kwa kuufanya uongo kuwa jadi yao na huwa wepesi sana kusahau!
 
Mwanzo wa ngoma ni lele! Hamkani si shwari tena!! (No longer at ease! - Chinua Achebe RIP); serikali ya CCM ikifanya maamuzi ya mzaha mzaha; kuchekacheka; utekaji nyara; vitisho na Akili za mbayuwayu bila uchambuzi wa kina na maamuzi makini!! hii sio dalili njema kabisa.
 
Mwili ulinisisimka nilivyoona na kusikia kuwa "askari" waliomaliza mafunzo ya JKT bila kupatiwa ajira rasmi wanataka kuandamana kuelekea Ikulu. Mmmh, nikasema sasa huu ni ukurasa mpya katika historia ya majeshi yetu hapa nchini.

Serikali inapaswa kutumia busara sana katika kushughulika na hawa vijana, ambao tayari wameshapatiwa mafunzo ya kijeshi. Ni ajabu sana kuona ukosefu wa busara ulioonyeshwa hadi sasa katika kushughulikia tatizo lao. Nimeshangaa kusinga kiongozi wao alitekwa kwa staili ya Ulimboka! Kimsingi, suala hili halikupaswa kufikia hatua ya wao kuandamana. Kutumia nguvu kuwazima ni kosa ambalo siku moja serikali itakuja kulijutia.
 
Vijana wanatumika bayana kabisa hili ninauhakika nalo kabisa.
 
Serikali inapaswa kutumia busara sana katika kushughulika na hawa vijana, ambao tayari wameshapatiwa mafunzo ya kijeshi. Ni ajabu sana kuona ukosefu wa busara ulioonyeshwa hadi sasa katika kushughulikia tatizo lao. Nimeshangaa kusinga kiongozi wao alitekwa kwa staili ya Ulimboka! Kimsingi, suala hili halikupaswa kufikia hatua ya wao kuandamana. Kutumia nguvu kuwazima ni kosa ambalo siku moja serikali itakuja kulijutia.
Kama wao wameshindwa kutumia busara kuna haja gani kutumia busara kuwasikiliza hata hivyo jeshini hakuna busara kunaamri tu basi,kwahiyo hata wao lazima wapelekwe kijeshi tu.
 
Misitu gani wataingia wakati misitu yote kuna makambi na vituo vya kijeshi

Ila amboni Tanga hamna!?? Basi watakwenda huko, kwani kama kungekuwa na kambi ya jeshi yasingewapata jwtz /polisi kama yaliyowakuta, Humu kuna watu mnaongea kama mmekatwa vichwa!!!
 
Hiyo ni dalili ya vijana kuchoshwa na ukiritimba, ubadhilifu na kupoteza imani kwa viongozi wakuu wa nchi.
Hali hiyo imesababisha vijana kukata tamaa na kuamua kujichukulia hatua wanayo amini kwamba ndio njia sahihi ya utatuzi wa matatizo yanayo wakabili.
 
...wanaojua kusoma alama za nyakati waliwataadhalisha mapema watawala ya kuwa kama wataendelea na ghiribu nchi haitatawalika lakini kwa kuwa wamejawa na kiburi waliamua kushupaa...

NI HERI YA WAJINGA WANAOJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA YA-WENGINE KULIKO WAPUMBAVU WANAOJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA YAO
 
Serikali inapaswa kutumia busara sana katika kushughulika na hawa vijana, ambao tayari wameshapatiwa mafunzo ya kijeshi. Ni ajabu sana kuona ukosefu wa busara ulioonyeshwa hadi sasa katika kushughulikia tatizo lao. Nimeshangaa kusinga kiongozi wao alitekwa kwa staili ya Ulimboka! Kimsingi, suala hili halikupaswa kufikia hatua ya wao kuandamana. Kutumia nguvu kuwazima ni kosa ambalo siku moja serikali itakuja kulijutia.

Aaah! mafunzo waliyopata hawa ni ya kuchoma singe tu adui 2 kwa kutumia SAR na kuonyeshwa kwa macho bunduki aina ya G3, SMG, LMG na bomu la RPG 7v basi, hawana kingine zaidi ya kuimba, mguu pande mguu sawa, kunyakuwa na kupita juu ya kamba.
 
Ajira million mlizoahidi zipo wapi? Tukidai ahadi zenu mnaanza kulia wacha tuandamane
 
Hawa vijana ni mburukenge kabisa..hivi nani aliwaambia wakienda JKT serikali itawapa ajira?

hivi unajiua tawala nyingi zinaanguka kwa tatizo la ajira na matatizo ya kiuchumi? usilichukulie hili suala kimzaha
 
Back
Top Bottom