JKT: Mchezo wa ndama utaamsha madume

JKT: Mchezo wa ndama utaamsha madume

kwa mujibu wa JKT "Moja ya kipengele cha masharti ya kujiunga na JKT kinasema kuwa ‘Kwa kipindi chote nitakachokua ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa nitakuwa nafanya mafunzo ya kijeshi na ya stadi za kazi na maisha, na baada ya mkataba nitarejea nyumbani. Hivyo sitalidai Jeshi la Kujenga Taifa ajira, wala kulitaka linitafutie ajira/kazi’."

Kunavitu ambavyo sijavielewa na nimejaribu kupitia malengo ya uanzishwaji wa JKT ni kutoa mafunzo kwaajili ya kuajiriwa na serikali na kama ndio je ni Ajira zipi ambazo zinawafaa hawa JKT?
 
Hawa vijana ni mburukenge kabisa..hivi nani aliwaambia wakienda JKT serikali itawapa ajira?

Mkuu hawa watu wanatumika kisiasa haiwezekani vyombo vya habari vinawapa promo wakati malengo ya JKT yako wazi pengine mimi nimepitiwa na niko tayari kurekebishwa kwa hili ni Ajira zipi wanazitaka? na Kupita JKT ndo umekua certified kufanya kazi serikalini if anayo proffesional nyingine?
 
hivi unajiua tawala nyingi zinaanguka kwa tatizo la ajira na matatizo ya kiuchumi? usilichukulie hili suala kimzaha
Sasa wewe unaona ni sawa kila raia asiye na ajira aende kuidai Ikulu? hii ni akili au matope?
 
Mkuu hawa watu wanatumika kisiasa haiwezekani vyombo vya habari vinawapa promo wakati malengo ya JKT yako wazi pengine mimi nimepitiwa na niko tayari kurekebishwa kwa hili ni Ajira zipi wanazitaka? na Kupita JKT ndo umekua certified kufanya kazi serikalini if anayo proffesional nyingine?
Hawa wanataka eti wachukuliwe JWTZ wakanywe bia za bukubuku! Nchi hii imejaa vilaza wasiotaka kuumiza vichwa.
 
Hili dubwana JKT ni hatari sana kuliko wanavyofikiri..JK utaleta maafa sana nchi hii kwa ajili ya kukurupuka kwako
 
Nasikia kiongozi wao katekwa tayari, na kachomwa sindano za kupoteza kumbukumbu.
 
Hawa wanataka eti wachukuliwe JWTZ wakanywe bia za bukubuku! Nchi hii imejaa vilaza wasiotaka kuumiza vichwa.

Hawa kunawatu wako nyuma yao Haiwezekani Leo hii udai ajira wakati huna mkataba na Serikalini kwamba ukimaliza Jkt unapata kazi basi wote waliosomeshwa na Serikali vyuoni waingie barabarani na kudai serikali ilinisomesha ili iniajiri.
 
Mh hii point ni kweli, chadema weshaingia hapo halafu hawaoneshi jinsi gani watawasaidia
 
Hawa wanataka eti wachukuliwe JWTZ wakanywe bia za bukubuku! Nchi hii imejaa vilaza wasiotaka kuumiza vichwa.
Jwtz wanaitarajia iajili vijana kutoka jkt, kutu ambacho hawakifanyi kwa sasa kwani wanaajili nje ya jkt na mbaya zaidi nafasi hizo huuzwa kwa wenye pesa au huwapa ndugu zao.
 
Jwtz wanaitarajia iajili vijana kutoka jkt, kutu ambacho hawakifanyi kwa sasa kwani wanaajili nje ya jkt na mbaya zaidi nafasi hizo huuzwa kwa wenye pesa au huwapa ndugu zao.

ooh kumbe ili ufike JWTZ lazima upite JKT? na Kama ndio intake zote za JKT zinaingiaga Jeshini?
 
kwa mujibu wa JKT "Moja ya kipengele cha masharti ya kujiunga na JKT kinasema kuwa ‘Kwa kipindi chote nitakachokua ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa nitakuwa nafanya mafunzo ya kijeshi na ya stadi za kazi na maisha, na baada ya mkataba nitarejea nyumbani. Hivyo sitalidai Jeshi la Kujenga Taifa ajira, wala kulitaka linitafutie ajira/kazi'."

Kunavitu ambavyo sijavielewa na nimejaribu kupitia malengo ya uanzishwaji wa JKT ni kutoa mafunzo kwaajili ya kuajiriwa na serikali na kama ndio je ni Ajira zipi ambazo zinawafaa hawa JKT?
Hapo napo patamu,watu waliopata mafunzo ya Kijeshi wanazidi kuongzeka mtaani,pia ni hatari,tofauti na miaka ya 70-80 ukimaliza JKT unaenda Chuoni au Kazini
 
Mkuu hawa watu wanatumika kisiasa haiwezekani vyombo vya habari vinawapa promo wakati malengo ya JKT yako wazi pengine mimi nimepitiwa na niko tayari kurekebishwa kwa hili ni Ajira zipi wanazitaka? na Kupita JKT ndo umekua certified kufanya kazi serikalini if anayo proffesional nyingine?
Wanatumiwa na nani sasa?jamani tusiwe na majibu mepesi saaana
 
Wanatumiwa na nani sasa?jamani tusiwe na majibu mepesi saaana
walikua na mkataba na Serikali Iwapo watamaliza JKT wataajiriwa na Serekali?
To what extent mafunzo ya kijeshi wanayapata ni swala la msingi kwa fikra zangu ndogo lengo kuu lilikua hili la kuwaweka pamoja vijana wa nchi hii na kuwapa malezi kuhusu uzalendo na umoja ili kuondoa dalili za matabaka zilizoanza kujitokeza katika jamii baada ya uhuru

Dira

Kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa, hatimaye Tanzania iwe ni jamii yenye nidhamu, umoja, uzalendo, undugu, wakakamavu na kupenda kazi.
Dhima
Kuwalea vijana wa Tanzania, kinidhamu, uzalendo, ukakamavu na kuwafundisha ujuzi na hatimaye kuchangia katika ulinzi wa Taifa na maendeleo ya kiuchumi.
 
Ulinzi wa Taifa

  • Kuwapa vijana mbinu za kijeshi wawe Jeshi la akiba, kuwaandaa vijana watakaofaa kujiunga na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
  • Kuwaandaa vijana kusaidia katika majanga mbalimbali, mfano mafuriko, moto na ajali mbali mbali.
 
Wanatumiwa na nani sasa?jamani tusiwe na majibu mepesi saaana

Usalama wa nchi uko hatarini kuliko unavyodhani ikiwa hatua za kuzuia hazitajulikana.
1. Green brigade walipokea mafunzo ya kijeshi kwenye "kambi za siri". Wakufunzi ni wanajeshi.
2. Vijana wasio na elimu (wasio na sifa za kuajiriwa Serikali)wakapokea mafunzo ya kijeshi katika kambi halali za JKT.
Kilichobaki ni kuwachochea na kuwapa siraha. Itakapotokea hilo, Tanzania yenye amani haitakuwapo.
To prove wrong tafuta nchi ya Afrika yenue watu wasio na elimu au ajira Serikalini lakini wanamafunzo ya kijeshi kama iko salama.
Tanganyika yenye kupakana na nchi 8, katika mipaka yake mipana ni vigumu kuzuia upitishwaji wa silaha.
 
  • Thanks
Reactions: kdc
Back
Top Bottom