JKT: Mchezo wa ndama utaamsha madume

JKT: Mchezo wa ndama utaamsha madume

Hivi hawa walikaa kambini kwa muda gani?. Serikali iangalie upya jinsi ya kuwasaidia mana hawa vijana watatumia mbinu kutuvamia na mapanga majumbani kwetu.
 
ooh kumbe ili ufike JWTZ lazima upite JKT? na Kama ndio intake zote za JKT zinaingiaga Jeshini?
sina uhakika na hili, jw itakuwa haina uwezo wa kuchukua wote watokao jkt, lkn nafasi zinapo tokea kwanini wasichukue miongoni mwa jkt?
 
Ajira million mlizoahidi zipo wapi? Tukidai ahadi zenu mnaanza kulia wacha tuandamane
Ajira alizoahidi sio za kuajiri serikalini tu ni pamoja na sekta binafsi.

Mfano kuruhusu BODABODA na wauza vocha za simu tu ajira zao zimeshapita hiyo milioni moja ukiongeza ajira zilizozalishwa baada ya barabara nyingi kuwekwa lami ambako utakutana na wauza matunda,vyakula. vinywaji etc kando ya hizo barabara mpya zilizojengwa hiyo milioni ilishapitwa siku nyingi.
 
....twendeni mistuni,maneno mengi ya nini
 
hawa vijana wanafanana na wale waliotembea maili maelfu kutoka Shy kukutana na Mh. Rais!!

Kuna tatizo la msingi kwa vijana wetu... Kazi ipo.
 
hivi unajiua tawala nyingi zinaanguka kwa tatizo la ajira na matatizo ya kiuchumi? usilichukulie hili suala kimzaha
Sasa wakiandamana wa JKT wa vyuo vikuu nao wafanyeje?waache ubabaishaji,nani aliwaambia kuwa baada ya JKT kuna ajira?waende makampuni ya Ulinzi au waji organize waombe mkopo wafungue kampuni yao ya ulinzi na sio kuliazimisha serikali iwaajiri wakati wengi wao ni STD 7 na form four division 5
 
sina uhakika na hili, jw itakuwa haina uwezo wa kuchukua wote watokao jkt, lkn nafasi zinapo tokea kwanini wasichukue miongoni mwa jkt?

Jeshi dogo la kisasa linahitaji akili nyingi kuliko nguvu, hawa jkt wetu wana akili au nguvu? kama wana nguvu waende wakatafute kazi Majembe auction mart na jiji badala ya JWTZ ambako zinatumika satellites na askari wachache sana wa miguu lakini wenye elimu za sheria, utawala, uhandisi, afya, uhasibu na n.k ili wanapoikamata ardhi, mitaa, miji na nchi wajue nini cha kufanya kuwasaidia watu waliowateka, wakomboa au nchi wanayoikalia. Hivyo sidhani kama vijana hawa wa jkt wana kiwango cha elimu kinachokidhi dhana ya jeshi dogo lakini la kisasa. Je, wanafundishika nini kwenye vyuo vyovyote hapa duniani au ni darasa la saba na form 4 fail? Kama yuko kijana wa jkt mwenye division kuanzia 3 na kuendelea au mwenye diploma, degree au master ya fani yoyote nadhani anaweza kuchukuliwa JWTZ kwa urahisi. Ndugu zangu jeshi siku hizi limeachana na matumizi ya bunduki za SAR, SMG, G3, n.k vitani, vifaa vingi ni computerized ambavyo unahitaji askari mmoja tu kuweza kuangamiza adui wengi, kusema kwamba jw itatoa ajira kwa ma-jkt wote tunajidanganya wenyewe na hiyo ni hatari zaidi kwakuwa utakuwa na jeshi kubwa mno ambalo utashindwa kulihudumia kikamilifu hatimaye litafanya uasi kwa kutumia silaha walizonazo mikononi. Nionavyo mimi JKT iwezeshwe ili iwe taasisi kubwa sana ya uzalishaji wa mazao ya kilimo, ufugaji, viwanda, uvuvi, madini, misitu, nyuki na uhandisi nchini ili vijana wengi walijenge taifa kwa kuajiriwa JKT na kufanya uzalishaji wa hali ya juu wa kutegemewa kulilisha taifa na nchi majirani. Mfano, JKT wavue samaki kwenye kina kirefu na kuwasindika na kutafuta masoko nnje na ndani pamoja na kupewa jukumu la kulisha na kuvisha majeshi yetu, shule, vyuo, magereza, n.k. Kwa mtindo huu nchi itasonga mbele na vijana watajenga nchi yao kwa njia halali. Kuandamana kwenda Ikulu ni kutapatapa sawa na wale vijana wanaoiba mifuniko ya chemba za maji machafu barabarani na kuiba vibao vya alama za barabarani. Tunahitaji viongozi wenye vision na taifa hili sio kuwateka na kuwatesa vijana wanaotapatapa kwa njaa huku tukiwa na ardhi, madini, misitu, bahari na mbuga.
 
Aaah! mafunzo waliyopata hawa ni ya kuchoma singe tu adui 2 kwa kutumia SAR na kuonyeshwa kwa macho bunduki aina ya G3, SMG, LMG na bomu la RPG 7v basi, hawana kingine zaidi ya kuimba, mguu pande mguu sawa, kunyakuwa na kupita juu ya kamba.
Aaaa bana, hii imezuiliwa.
 
hawa wahitimu wa JKT siyo wajinga kudai ajira inawezekana ni kweli serikali iliwahidi kuwapa ajira sasa wanawageuka na kuwakamata viongozi wao kwenda kuwatesa hii itakuwa ni kuongeza tatizo siyo kumaliza tatizo JK wape ajira hawa vijana kama walivyoahidiwa na serikali yako ya ccm.
 
Aaah! mafunzo waliyopata hawa ni ya kuchoma singe tu adui 2 kwa kutumia SAR na kuonyeshwa kwa macho bunduki aina ya G3, SMG, LMG na bomu la RPG 7v basi, hawana kingine zaidi ya kuimba, mguu pande mguu sawa, kunyakuwa na kupita juu ya kamba.


Jiridhishe kwa hayo na nafsi yako iridhike kuwa unaongea ukweli, kwamba matumizi ya SAR na hizo nyingine ulizoandika yako tofauti!!!
 
Serikali iliyopo madarakani inastahili lawama kwa asilimia zote kwani wao ndio walituahidi waTANGANYIKA maisha bora........sasa wanadai walichoahidiwa wanaonekana waasi.......
 
Jiridhishe kwa hayo na nafsi yako iridhike kuwa unaongea ukweli, kwamba matumizi ya SAR na hizo nyingine ulizoandika yako tofauti!!!

nimekaribia ukweli? samahani mkuu
 
JKT ya sasa hivi ni jkt ya maslahi binafsi, ya kujifananisha na wazalendo halisi wa nchi hii, hata wabunge walijaribu kwenda ili kujitafutia ufananisho.
Hawa vijana hawakuiva kijeshi na wala hawajui walifuata nini jeshini!
 
Jesh la Kujenga Taifa ndo maana na dhima halsi ya JKT,sasa hawa vjana wanataka Taifa ndo liwajenge wao?
 
Back
Top Bottom