JK unayajua haya?

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Kuna habari kuwa anaweza kufa eidha leo au Jumapili

Mwananyamala Hosp mtamuua mama huyu!
Imeelezwa kuwa hali ya mwanamke mjamzito ambaye kiumbe chake kimefia tumboni tangu wiki iliyopita, bado ni tete, huku ndugu zake wakijitahidi kutafuta tiba ili kunusuru maisha yake.

Kwa mujibu wa dada mkubwa wa mgonjwa huyo ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake kwa kuogopa kuendelea kukosa ushirikiano kutoka Hospitali ya Mwananyamala, alisema hali ya ndugu yao si nzuri.

“Kusema kweli ndugu yetu bado hali yake si nzuri, maana hata hii (leo) jana tumerudi tena Hospitali ya Mwananyamala lakini hakuna tiba tuliyopata,” alieleza.

Aliongeza kuwa hata jana walipokwenda na kumtafuta daktari wa kuwasaidia, aliwaeleza kuwa wasubiri muda wa wiki mbili waliopangiwa awali.

Alisema kutokana na majibu hayo, waliamua kurudi nyumbani na mgonjwa huyo huku wakijaribu kuwasiliana na ndugu wengine, ili kutafuta fedha kwa ajili ya kumpeleka katika hospitali binafsi.

“Kwa sasa hatuna njia nyingine, kwa muda huu tunajaribu kukusanyana na kufanya kikao ili tumpeleke katika hospitali binafsi, kwani hatuwezi kukaa kwa wiki mbili, kwani hali yake ni mbaya,” alisisitiza.

Hivi karibuni hospitali hiyo imekuwa ikigubikwa na tuhuma mbalimbali, ikiwa pamoja na kumbadilishia mwanamke mmoja mtoto na kumpa mfu.

http://www.darhotwire.com/home/news/2009/11/26/mwananyamala_hosp_mtamuua_mama_huyu.html
 
Mwananyamala hospital
na temeke hospital ni wauaji wakubwa..
Ni kila siku habari hizo hizo.
 
Ndo hapo sasa tatizo lilipo. Kama hata issue za moja kwa moja za utendaji kama hizi zitahitaji JK aingilie kati, huo muda wa kutalii na bembea utakuwa haupo. Hii inaonyesha lipo tatizo la kiungozi kama kila kitu kitahitaji yeye a micromanage
 
Mfumo mzima wa sekta ya afya una mapungufu na changamoto nyingi sana. Inabidi watu warudi kwenye meza na kuangalia upya mikakati yao ktk swala hili la afya zetu kwa kweli.

Ikiwa kutokomeza malaria tu ni hadidhi!!!, mapesa ya miradi ya malaria yanafanya nini kama hata kuangamiza mbu hawawezi aibuuuu!!!!
 
Kuna habari kuwa anaweza kufa eidha leo au Jumapili
Game hapa umedunda! Kuna taratibu ambazo ni lazima zifuatwe inapokuwa "Intra Uterine Fetal Death" mtoto kufia tumboni is non urgent issue unless otherwise, nafikiri hao jamaa wa Mwananyamala wako 100% along the path lakini kwa midomodomo ya hao ndugu na udaku wa gazeti inajaribu kuharibu jina la Hospitali bila sababu za msingi, toka lini mtoto kufia tumboni anaweza kumuua mzazi? kama kungekuwa na hatari hiyo sidhani kama angepewa ruhusa kwenda nyumbani, haya magazeti mengine ni magazeti taka ambayo hayaelimishi bali ni kuchafua hali ya hewa tu, Magazeti yaje na ukweli wenye picha halisi, si mbaya yakaongelea ukosefu wa vifaa mahospitalini, vifo vinavyotokea kwa uzembe wa madaktari na manesi wao, ulevi uliopindukia kwa baadhi ya madaktari etc...bila kumuonea mtu au Hospitali fulani,
 
Shida ya madaktari wa nchi hii ni kwamba hawawathamini watea wao (wagonjwa). Hawaoni umuhimu wa kuzungumza na mgonjwa na kumwelimsha hatua walizofikia. Mgonjwa anatahamaki maana hajapewa details zozote za hat next, zaidi ya kuambiwa 'njoo baada ya wiki mbili'. Hii ni kupeleka mambo kibabe. Mweleze kinagaubaga mgonjwa wako juu ya tatizo na njia ya kulitatua. Mruhusu akuulize maswali, yajibu; mkiachana kila mmoja atakuwa na amani ya kufuatilia makubaliano.

Pamoja na hayo, sikubaliani na maelezo yako eti kwamba mtoto kufia tumboni is a non urgent issue. Akiozea tumboni? Inategemea na case, ndio maana kuna njia za kusafisha. Naturally kiumbe kilichokufa kitatoka baada ya muda fulani, lakini hiyo haimaanishi kusiwe na uangalizi. Ikitokea complication je?
 
Game hapa umedunda! Kuna taratibu ambazo ni lazima zifuatwe inapokuwa "Intra Uterine Fetal Death" mtoto kufia tumboni is non urgent issue unless otherwise, nafikiri hao jamaa wa Mwananyamala wako 100% along the path lakini kwa midomodomo ya hao ndugu na udaku wa gazeti inajaribu kuharibu jina la Hospitali bila sababu za msingi, toka lini mtoto kufia tumboni anaweza kumuua mzazi? kama kungekuwa na hatari hiyo sidhani kama angepewa ruhusa kwenda nyumbani, haya magazeti mengine ni magazeti taka ambayo hayaelimishi bali ni kuchafua hali ya hewa tu, Magazeti yaje na ukweli wenye picha halisi, si mbaya yakaongelea ukosefu wa vifaa mahospitalini, vifo vinavyotokea kwa uzembe wa madaktari na manesi wao, ulevi uliopindukia kwa baadhi ya madaktari etc...bila kumuonea mtu au Hospitali fulani,

I suspect wewe unatibiwa TRAUMA CENTRE mabako kumwona consultant inabidi ikutoke laki 5!

pili HOSPITALI ya Mwananyamala haihitaji magazeti ya udaku kuiharibia jina kwani performance yake tayari inatosha kuiharibia jina

Tuulize sie tunaokaa Mwananyamala Kisiwani na kutibiwa pale ndio tutakwambia ukweli

Kama unataka ndugu yako afe mpeleke Temeke,Mwananyamala au Ilala.
 
Mfumo mzima wa sekta ya afya una mapungufu na changamoto nyingi sana. Inabidi watu warudi kwenye meza na kuangalia upya mikakati yao ktk swala hili la afya zetu kwa kweli.

Ikiwa kutokomeza malaria tu ni hadidhi!!!, mapesa ya miradi ya malaria yanafanya nini kama hata kuangamiza mbu hawawezi aibuuuu!!!!

Sio afya tu! Miundo mbinu, elimu, utawala bora, katiba na sheria,..... ni mfumo mzima wa uongozi wa nchi.

Wakati ambapo jiji lina ufinyu wa barabara kiasi hiki, lami na uzima wake katika barabara ya Old Bagamoyo inatinduliwa. Hii ni dhihaka na kufuru kwa walipa kodi. Lini serikali itaanza kusikiliza matatizo ya watu wake?? Tunahitaji hizo barabara zipanuliwe, hata kama zitashindiliwa changarawe tu potelea mbali. Badala yake wanakwangua lami, barabara inabaki nyembamba vilevile!

Tumelaaniwa? Hata kama ni msaada, si tuuelekeze kwenye priorities zetu? Mimi nina hakika ni kodi zetu hizo. Halafu tunawaangalia tu.
 
Quote:

Game hapa umedunda! Kuna taratibu ambazo ni lazima zifuatwe inapokuwa "Intra Uterine Fetal Death" mtoto kufia tumboni is non urgent issue unless otherwise, nafikiri hao jamaa wa Mwananyamala wako 100% along the path lakini kwa midomodomo ya hao ndugu na udaku wa gazeti inajaribu kuharibu jina la Hospitali bila sababu za msingi, toka lini mtoto kufia tumboni anaweza kumuua mzazi? kama kungekuwa na hatari hiyo sidhani kama angepewa ruhusa kwenda nyumbani, haya magazeti mengine ni magazeti taka ambayo hayaelimishi bali ni kuchafua hali ya hewa tu, Magazeti yaje na ukweli wenye picha halisi, si mbaya yakaongelea ukosefu wa vifaa mahospitalini, vifo vinavyotokea kwa uzembe wa madaktari na manesi wao, ulevi uliopindukia kwa baadhi ya madaktari etc...bila kumuonea mtu au Hospitali fulani,

I suspect wewe unatibiwa TRAUMA CENTRE mabako kumwona consultant inabidi ikutoke laki 5!

pili HOSPITALI ya Mwananyamala haihitaji magazeti ya udaku kuiharibia jina kwani performance yake tayari inatosha kuiharibia jina

Tuulize sie tunaokaa Mwananyamala Kisiwani na kutibiwa pale ndio tutakwambia ukweli

Kama unataka ndugu yako afe mpeleke Temeke,Mwananyamala au Ilala.

Hana tofauti na raisi wake huyu; eti 'mbona mnakuza machache mabaya tu, hakuna mazuri tunayofanya?' Watu waendelee kufa tukae kimya tu eti tusiharibu jina la hospitali. Hovyo kabisa.
 
Inabidi tuombe Mungu ageuze miyoyo ya hawa manesi na madaktari ili wawahudumie walalahoi! Kwani watoto wa wakubwa hawaendi kutibiwa mwananyamala
 
Halloo, samahani... wasiliana na waziri wa afya....... Mzee yuko Jamaika anabembea na wajukuu wa Bob Marley.....
 
I suspect wewe unatibiwa TRAUMA CENTRE mabako kumwona consultant inabidi ikutoke laki 5!

pili HOSPITALI ya Mwananyamala haihitaji magazeti ya udaku kuiharibia jina kwani performance yake tayari inatosha kuiharibia jina

Tuulize sie tunaokaa Mwananyamala Kisiwani na kutibiwa pale ndio tutakwambia ukweli

Kama unataka ndugu yako afe mpeleke Temeke,Mwananyamala au Ilala.

Game mimi ni mlalahoi kama wewe na yule na siku zote hutibiwa kwenye Hospital za aina hiyo, Ubovu wa Mwananyamala kama upo basi ni karibu Hospitali zote za serikali yetu zinahusika,(Vitendea kazi vibovu, Nidhamu ya chini, etc...) Lakini unapozungumzia mtoto kufia tumboni "bila kuwa na tatizo jingine" eti itamuua mama mzazi hapo umefulia kawaone wanafunzi pale Muhimbili watakueleza mtiririko wa matibabu ya mtu aliyepatwa na masahibu ya aina hiyo, Mimi binafisi niliwahi kuuguza pale Mwananyamala wanaperform vizuri na nawapa >80%, Tusidanganyane jamani, Mwananyamala wanarecord nzuri kulinganisha na wilaya zingine ambazo kwa wiki wanaua kinamama wajawazito 7-10 na hakuna kelele kutoka magazeti yetu ya udaku, nani anajua Maternal Death za Rufiji, Bariadi Tandahimba, Bunda, Liwale, Ujiji, Mpanda etc...Sasa ukizisikia hizo ndio unaweza koa fahamu milele, la msingi nchi yetu hii kila angle kumeoza na sio Mwananyamala tu ila kwa kuwa waojua kuchonga sana na uwepo wa magazeti ni hapo mjini basi Ilala, Temeke, Mwananyamala ni sehemu ya machinjio? SIO KWELI!
 
Siasa ndiyo inaua nchi yetu na wananchi, nani waziri husika? Nini kilisababisha apewe uwaziri na kuacha fani yake kama hakuna mabadiliko kwenye hiyo wizara?
 
Rais atayajuaje haya wakati kila kukicha yuko mikoani au nje ya nchi kubembea!!!!

Kila kukicha mikoani kuna tatizo gani kama anafanya kazi na wajibu wake huko? ulitaka kila kikicha ashinde dar au?
kubembea labda ilikuwa part ya mapumziko tu kama wengi wa wana JF walivyochangia kuwa ni vema rais akapumzika....kupumzika sio kukaa tu chini jamani....,kubembea! kubarizi na wajukuuu kuwasimulia hadithi, kunywa togwa jamvini na bibi/babu yako pale kijijini kwako! hatuwezi kuwa na mtazamo mmoja wa nini tendo gani linamaanisha kupumzika na wapi mtu apumzike. Kila mtu anafahamu afanyaje ili apate pumziko iwe ndani au nje ya dar, mkoani au hata nje ya nchi. Inawezekana hata mie pia nipo wrong kudhani kuwa kwenye bembea alikuwa anapumzika.....

Kubembea hakumfanyi rais asijuwe matatizo ya wananchi wake unless hana nia ya kuyajua matatizo hata kama asingebembea!

A woman can be strong, confident and sexy
 
Back
Top Bottom