Udhaifu wake uko wazi kuanzia anapomteua waziri mkuu pamoja na baraza la mawaziri. Yani hajifunzi chochote kutokana na makosa ya huko nyuma? Kule kulikuwa na EPA mara akaingia RICHMOND akang'oka mwenye nywele nyeupe ingawa sio mzee, kisha OPERATION TOKOMEZA UJANGILI wakang'oka watu 3, sasa ESCROW huyo tena ni baba lao. Yani ina maana hakuna hata jambo moja JK alilojifunza kutoka kwenye EPA-----RICHMOND----OPERATION TOKOMEZA na sasa ESCROW? Angekuwa makini angekuwa ameshajifunza jambo ili kuzuia ESCROW. Je; huyu ni rais au ni dalali wa mafisadi?