Membe S K
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 1,389
- 1,215
NAFASI YA SEKTA BINAFSI KWENYE UCHUMI WETU
Andiko hili linaongelea nafasi na umuhimu wa sekta binafsi katika uchumi na maendeleo yetu tangu tulipoubwaga ujamaa wa Mwl Nyerere na kuingia kwenye mfumo wa kibepari. Kiufupi andiko hili linasema kwamba mchango wa sekta binafsi katika pato la taifa ni mdogo. Sekta binafsi haijapewa malezi ya kutosha na badala yake imebanwa na mdororo wa uchumi unaolazimisha serikali kuweka kodi kandamizi. Pia sekta hii muhimu inadumazwa na maamuzi/sera zisizo rafiki. Utitiri wa kodi na mazingira yasiyo rafiki kwa sekta binafsi yanasababisha sio tu ugumu wa maisha lakini pia kuzorota kwa biashara ya nje na kuigeuza nchi yetu kuwa shimo la takataka la bidhaa zisizo na ubora wala viwango. Ili uchumi wetu ukuwe na kuwa stahimilivu kuna haja kubwa ya kuikuza sekta binafsi kwa gharama zozote ili iwe sekta inayoendesha uchumi kwa asilimia kubwa.
UTANGULIZI
Tangu tupate Uhuru 1961 hadi kipindi cha Hayati Ally Hassan Mwinyi (R.I.P) nchi yetu ilikuwa inaendeshwa na SEKTA YA UMMA chini ya mfumo wakijamaa wa Mwl Nyerere (R.I.P). Kwenye mfumo huu SEKTA BINAFSI ilikuwa haramu na kila ilikojitokeza ikaitwa biashara za MAGENDO. Miaka ya mwisho ya 80 ubepali ambao ndio nguzo ya sekta binafsi ukaushinda mfumo wa kijamaa wa Mwl Nyerere na hivyo nchi yetu "ikabadilisha gia bondeni" na kuanza kuhalalisha sekta binafsi kupitia msemo uliompa jina la utani aliyekuwa rais wakati huo mzee Mwinyi: RUKHSA. Yaani biashara na shughuli binafsi zilizokuwa MAGENDO zikapata Rukhsa.
Miaka ya mwanzo ya 90 nchi zilizokuwa zinafuata mfumo wa kijamaa unaopiga vita sekta binafsi zikalazimishwa na shirika la fedha duniani (IMF) na pacha wake Benki ya Dunia kufanya UBINAFSHISHAJI wa njia zote kuu za uchumi. Lengo likiwa kuongeza ufanisi katika uchumi wa nchi hizo kwasababu inaaminika sekta ya umma haiwezi kuwa fanisi.
HII INA MAANA GANI KWETU?
Maana yake sekta binafsi kama ingekuwa mtoto ilizaliwa miaka ya mwisho ya 90 na kuanza kuota nywele miaka ya mwisho ya 2000. Kwa maneno mengine kama ni mtoto basi sekta binafsi ndio kwanza sasa inaonyesha dalili ya kuota jino moja la mbele. Yaani kimsingi sekta hii muhimu kwa uchumi na maendeleo yetu ni changa mno kwa sasa.
Kwa kulijuwa hili vipindi vya uongozi wa Hayati Benjamin Mkapa (R.I.P) na Jakaya Kikwete vilijikita katika kuipanua na kuikuza sekta hii kwa kuendeleza ubinafshishaji na kutengeneza mazingira rafiki kwa makuzi ya sekta hii. Kwenye vipindi hivi kwa mfano kodi kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo hazikuwa kikwazo cha biashara zao na wigo wa biashara ulipanuka. Tunaweza kusema vipindi hivi sekta binafsi ilinawili.
UKUAJI WA SEKTA BINAFSI TANZANIA
Ukuaji wa sekta binafsi kwenye nchi ambayo ilifuata siasa za kijamaa unategemea sana SERA na mikakati ya nchi. Hii ni pamoja na kuhakikisha shughuli za serikali na mashirika ya umma zinaratibiwa na kufanywa na sekta binafsi. Mfano ujenzi wa makao makuu Dodoma ufanywe na kampuni binafsi ya ndani, au rais anapofanya mikutano elekezi na mabalozi wake afanyie kwenye hotel ya kampuni binafsi ya ndani badala ya kufanyia kwenye ofisi za serikali.
Mkakati mwingine ni sheria za kodi. Kwamba biashara mpya ipewe upendeleo maalum (preferential treatment) wa kodi kwa kipindi CHA KUTOSHA. Vilevile serikali ihami biashara changa za ndani dhidi ya ushindani wa bidhaa au huduma kutoka nje (infant industry protection), huku ikihakikisha viwanda vinatumia mali ghafi au rasilimali watu kutoka ndani ya nchi.
NAFASI YA SEKTA BINAFSI KWENYE UCHUMI WETU.
Rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za nchi vilinawili sambamba na sekta binafsi chini ya uongozi wa Mkapa na Kikwete. Sakata la sakata la EPA, Sakata la ESCROW na kashfa kadhaa wa kadhaa za ubadhilifu zikaitumbukiza nchi kwenye madeni na kuzorotesha ukuaji wa uchumi. Matokeo yake deni la serikali kwenye sekta binafsi likawa linakua kwa kasi na hivyo kuidhohofisha sekta hiyo.
Bidhaa na huduma mbalimbali kutoka Kenya, China na India vikawa vinaingia kwa kasi kufidia ombwe la ufanisi wa sekta binafsi. Hii ikaikaba koo sekta binafsi ambayo tayari ilishaumizwa na mdororo wa uchumi na madeni.
Sekta binafsi iliumizwa zaidi na sera/maamuzi za hayati John Magufuli (R.I.P). Maamuzi ya Magufuli kutaka nchi ijiendeshe yenyewe kwa kodi zake zilidumaza kabisa sekta binafsi ambayo tayari ilishapoteza pumzi miaka ya mwisho ya JK. Haikuwa jambo geni kusikia biashara kadhaa zikifungwa kipindi cha Magufuli kwa wafanyabiashara kushindwa kulipa kodi. Wafanyabiashara wengine walidaiwa malimbikizo ya kodi ya miaka ya mwanzo ya JK, malimbikizo ambayo tayari yalishafanywa kuwa mtaji. Lakini pia biashara mpya zilipelekwa nchi jirani na huku wawekezaji kadhaa wakisitisha maamuzi ya kuwekeza Tanzania, wawekezaji wa mradi wa gesi Lindi kwa mfano. Tulipokuwa tunaimba vyuma kukaza hatukujua vitanzi vya sekta binafsi vilikuwa vinakaza mara dufu.
Mdororo wa uchumi na madeni unailazimu serikali sasa 'kuinyonga" sekta binafsi kwa utitiri wa kodi. Kibaya zaidi kwa miaka takriba 10 sasa serikali imejikita kwenye uwekezaji wa miundombinu mbinu, uchimbaji madini na nishati huku mazao yanayotupa hela za kigeni yakiachwa kwenye orodha ya vipaumbele, kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia 2023. Miundombinu, madini na nishati sio sekta zinazozalisha moja kwa moja au kutoa ajira nyingi. Hivyo basi uwezo wa serikali kumudu matumizi katika kutoa huduma za jamii na miradi mingine ya maendeleo umepungua na hivyo kulazimika kutafuta namna ya kuongeza kodi.
Jumla kuu ya haya yote ni kwamba ingawa uchumi unakua kwa kiasi cha kuridhisha mchango wa sekta binafsi kwenye pato la taifa unatia huruma. Benki ya Dunia kwenye ripoti yake ya December 19 mwakajana imesema kwamba Tanzania lazima iondokane na uchumi unaokua kutokana na sekta ya umma kwenda kwenye uchumi unaokua kutokana na sekta binafsi.
Nafasi ya sekta binafsi kwenye pato la taifa imeshuka kuanzia 2012 kwa mujibu wa tathmini za muda mrefu za Benki ya Dunia 2023. Pamoja na ukuaji unaoridhisha wa biashara ya nje mchango wa biashara hii kwenye pato la taifa umekuwa ukipungua mwaka hadi mwaka huku madini na utalii vikichukua nafasi ya mazao ya kilimo ambayo ndio nguzo yetu ya biashara ya nje.
ATHARI ZA UTITIRI WA KODI
Moja ya athari kubwa zaidi ni kuizamisha sekta binafsi. Tumeona wafanyabiashara wakigoma kufungua maduka kutokana na kodi na sera kandamizi. Sekta binafsi inapobanwa kwenye nchi inayopigana kutoa huduma na kulipa madeni inasababisha ugumu wa maisha unaomkabili karibu kila moja.
Athari nyingine ni kuifanya nchi yetu kuwa shimo la kutupa bidhaa za nje zisizo na ubora. Kwa maana kwamba sasa bidhaa bora ambazo zingetengenezwa ndani sasa tunalazimika kuingiza kutoka nje. Kadri tunavyoingiza bidhaa nyingi kutoka nje ndivyo tunavyoua sekta binafsi na ndivyo uchumi wetu unavyoshuka, kadhalika maendeleo yetu.
KIFANYIKE NINI SASA?
Kwa ujumla wake kuwe na mikakati madhubuti na endelevu ya kuikuza sekta binafsi na kuipa kipaumbele. Muhimu zaidi kuwe na mikakati ya kuufanya uchumi wa nchi yetu kuendeshwa na sekta hii muhimu. Ili kufikia haya mambo yafuatayo yanahitajika.
Mosi, kuwe na mkakati wa kuongeza mchango wa kilimo kwenye pato la taifa ambao sasa ni chini ya asilimia 26 tu. Hili linahitaji utafiti wa kujua vikwazo vinavyopunguza uzalishaji na kuvipatia ufumbuzi. Hatuwezi kuacha kilimo kuendesha uchumi wakati kimeajiri zaidi ya robo-tatu ya idadi yetu.
Pili, kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji na kuondoa vikwazo vya uwekezaji na kuepuka kuweka vikwazo vipya kama vile kodi nk. Hili lifanyike kwa umakini na umuhimu kwasababu nchi yetu imekuwa na tabia ya kubadili vipaumbele na sera za uwekezaji kila uongozi mpya unapochukua madaraka. Lazima tujenge imani ya wawekezaji wa nje na ndani huku tukitilia mkazo kulipa madeni yao kwa wakati, kupunguza utitiri wa kodi, na kuwajengea miundombinu muhimu.
Leo hii mitandao inasambaza barua inayosemekana imeandikwa na mabalozi wa nchi mbalimbali za America na Ulaya wakiomba kukutana na waziri wa mambo ya nje, January Makamba, kuongea suala la wawekezaji kushindwa kufanya biashara kwa kusakamwa na kesi za kodi na mazingira yasiyo rafiki kwa wawekezaji kutoka nchi za nje. Kama barua hiyo ni kweli basi ipo haja ya kuiangalia upya sekta binafsi na kuipa pumzi mpya na pia kujenga imani ya wawekezaji wa ndani na nje.
Tatu, rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya fedha yanayosababisha mdororo wa uchumi lazima vizibitiwe. Kudorora kwa shughuli za uchumi kunailazimisha serikali kuikaba sekta binafsi kwa kuongeza kodi lakini pia kunaifanya nchi kutumia fedha za miradi kuagiza bidhaa ambazo zingezalishwa ndani na kutengeneza ajira.
Nne, kupanua soko la bidhaa zetu ndani ya Africa kwa kuendelea na jitihada za kujenga soko la pamoja na nchi za Africa Mashariki na jumuia ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Africa.
MWISHO
Sekta binafsi kwenye mfumo tulionao wakibepari ni sekta nyeti katika uchumi na maendeleo. Ili ilete matunda tarajiwa uwezo wake wakushirikisha umma kupata wafanyakazi/wafanyabiashara wenye elimu na ujuzi pamoja na soko la ndani la uhakika lazima vijitosheleze.
Pia sekta binafsi inashamiri na kufanikiwa tu pale inapojengewa mazingira ya haki katika mahusiano yake na serikali na muhimu zaidi inapomudu badiliko la uongozi wa nchi. Kamwe sekta binafsi haiwezi kukua na kuendesha uchumi wawekezaji na wafanyabiashara wanapokosa imani na serikali au serikali inaponyanyasa wawekezaji. Serikali inawajibika kuilea sekta hii kwa umakini wa hali ya juu.
Vilevile pamoja na kwamba nchi yetu imepiga hatua katika ujenzi wa miundombinu kwa nia ya kuamsha shughuli za uchumi, ubora na uwapo wa miundombinu lazima uende sambamba na uwapo wa sekta binafsi imara inayoweza kutoa ajira, kuongeza biashara ya nje, na kupanua wigo wa makusanyo ya kodi ambayo ndio nguzo ya serikali katika kutoa huduma za jamii. Pasipo sekta binafsi imara uwekezaji unaofanywa na serikali katika miundombinu, utalii, madini na nishati utakuwa wa gharama kubwa kiuchumi, kimaendeleo na hata kisiasa.
SEMA NIMESEMA
Membe S K
Mtama, Rondo Chiponda
Tel. +255689463664
email: smembe426@gmail.com
June 28 2024