kamainaumasema
Member
- Sep 22, 2014
- 75
- 19
Jana kama ulimsikia Deo filikunjombe alivyomnukuu Thabit kombo utagundua kuwa kuna mamlaka kubwa aliificha kuisema ambayo ni Rais mwenyewe, rejea nukuu yake kwa Thabit kombo.
Nikumbushe
Jana kama ulimsikia Deo filikunjombe alivyomnukuu Thabit kombo utagundua kuwa kuna mamlaka kubwa aliificha kuisema ambayo ni Rais mwenyewe, rejea nukuu yake kwa Thabit kombo.
Udhaifu wake uko wazi kuanzia anapomteua waziri mkuu pamoja na baraza la mawaziri. Yani hajifunzi chochote kutokana na makosa ya huko nyuma? Kule kulikuwa na EPA mara akaingia RICHMOND akang'oka mwenye nywele nyeupe ingawa sio mzee, kisha OPERATION TOKOMEZA UJANGILI wakang'oka watu 3, sasa ESCROW huyo tena ni baba lao. Yani ina maana hakuna hata jambo moja JK alilojifunza kutoka kwenye EPA-----RICHMOND----OPERATION TOKOMEZA na sasa ESCROW? Angekuwa makini angekuwa ameshajifunza jambo ili kuzuia ESCROW. Je; huyu ni rais au ni dalali wa mafisadi?
jamaa aliendesha nchi kibabe kweli kweli. na kuna madudu mengi sana yalifanyika kipindi chake lakini nani alithubutu kwenda kumfunga paka kengele? hata huyo slaa, hebu niambie miaka 5 ya kwanza pale bungeni chini ya utawala wa mkapa alifanya nini? tunajua hakufanya lolote maana naye anaroho pia. ukweli ni kwamba Kikwete katutoa tongotongo wengi sana. hata hizo haki watu wanazojidai kuzijua kama sio uwazi wa Kikwete wala tusingezijua.Mkuu Abunuas ninakumbuka katika utawala wake Mkapa na kuwalinda viongozi wake alikuwa anawatuhumu baadhi ya wabunge kuwa "wanawivu wa kijinga"