JK sasa fanya hivi!!

JK sasa fanya hivi!!

mayenga

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2009
Posts
4,118
Reaction score
1,974
Mheshimiwa rais,

Kila mzalendo mwenye kupenda taifa hili,amefarijika sana na hotuba yako ya jana ulyoitoa katika kambi ya Kaboya,pale wilayani Muleba,karibu kabisa na kijijini kwetu.Umeonesha na kuudhihirisha ulimwengu kuwa pengine kimya kingi kina mshind😵nyo lako limepeleka ujumbe kwa nchi maadui na rafiki ya kwamba nchi hii iko imara na iko tayari kujilinda na kamwe mtu asidhubutu kutuchezea.

Kama raia mwema,ningependa kutoa ushauri ufuatao ili agizo na karipio lako liwe na mashiko.

1.Kuunda tume ya kijeshi au ya majaji kupitia mfumo mzima wa ajira katika majeshi yetu.Zipo tuhuma kuwa na ni ukweli ulio wazi kuwa nchii hii ina idadi ya wanajeshi,maaskari na maafisa wa ngazi za juu wa Usalama wa taifa, ambao si raia wa nchi hii.Katika hili,waraka wa Mtikila unaodai nchi jirani kupenyeza raia wa nchi zao na kuingia katika vyombo vya usalama,utakusaidia sana

2.Kuzifanyia kazi tuhuma juu ya chama chako,watendaji wako na ikiwezekana kuwafuta kazi mara moja watendaji wa ngazi za juu wa majeshi yetu ambao wamekuwa na tuhuma lukuki.

3.Kumfuta kazi mara moja Waziri wa sasa wa Ulinzi na jeshi la kujenga taifa,ambaye zipo tuhuma za wazi juu ya PHD yake.Ni aibu kwa jeshi kuongozwa na mtu ambaye ni mwongo.Kwa uwezo wake wa namna hiyo siyo kwamba uwepo wake waweza kuwa unachochea roho na moyo wa uasi dhidi ya wanajeshi wetu wapendwa?

4.Kujenga heshima ya Ikulu hasa katika mfumo mzima wa utendaji na utoaji wa matamko.Mtamko yanayotolewa na nyumba yetu pale Magogoni,yamekuwa yakiacha maswali mengi juu ya umakini na mfumo mzima wa utendaji katika nyumba yetu takatifu.Efficiency starts from WITHIN not from WITHOUT.

5.Kujiondoa mara moja katika shrikisho la Afrika Mashariki na kubakia na SADC pamoja na mashirika mengine ya kimataifa ambayo yana lengo la kutunufaisha.Kwa sasa hali ilivyo,kutokana na udhaifu wa watendaji tulionao katika wizara zetu,Wakenya na Waganda,hasa Wakenya,wamelitumia vizuri shirikisho hilo kujichukulia ardhi,kujipatia kazi,kufungua makampuni utitiri bila kufuata kanuni na taratibu za uwekezaji.Hii inapunguza usalama.

6.Kutopuuza kabisa,narudia kutopuuza kabisa malalamiko yanayotolewa na wanajeshi wetu dhidi ya maisha duni na stahili nyingine.Uzoefu unaonesha kuwa,mapinduzi katika nchi nyingi yamefanywa na wanajeshi wa kawaida na wala siyo mabrigedia,makanali wala majenerali.

7.Kuunda Wizara ya vijana peke yao,bila kuichanganya na wizara nyingine.Unda vijiji vya vijana,tunayo mapori mengi nchi hii,yatenge mapori tuliyo nayo,wape zana za kisasa vijana,wazazalishe chakula na uzalendo katika vijiji hivyo.Uangalizi wao uwe chini ya watu wenye upeo na maadili.Wasiwasi wangu ni kuwa kwa hali inavyokwenda,wimbi la vijana wanaohitimu mafunzo ya JKT,wanaofukuzwa toka CCP,wanaomaliza vyuo na shule ni BOMU kama alivyosema mshirika wako Edward.

8.Mwisho kabisa,ikitokea nchi hii iakenda vitani,ni raia wa nchi hii ambao watapigana kuikomboa,ni raia wa nchii hii watakaotoa senti yao ya mwisho ili nchi iwe salama.Jeshi haliwezi kupigana peke yake bila kuungwa mkono na raia.Hivyo basi,kwa hali ilivyo sasa,mahusiano ya majeshi yetu na raia lazima yaangaliwe kwa umakini mkubwa.Matukio ya polisi na wanajeshi wetu katika siku za karibuni,yanazidi kujenga usugu wa chuki miongoni mwa raia.Mshauri Waziri wako Mkuu aombe radhi kwa kauli yake kwa wananchi na azuie vyombo vya usalama kupiga raia.Hii itasaidia kuungwa mkono ikiwa mambo yatakwenda mrama.

Ni ushauri tu Mzee wa Magogoni.
 
Mkuu ni ushauri mzuri, lakini wananchi nao hasa wanasiasa ambao wanatumia makjukwaa ya kisiasa kujipatia umaarufu kwa kukebehi, kupotosha na hata kudhihaki vyombo vyetu vya ulinzi watambue kuwa kufanya hivyo ni kujijengea uadui na vyombo hivyo na ni vyema wakatafuta umaarufu kupitia sehemu zingine.
 
Hongera sana JK kwa kutoa msimano wa Nchi yetu juu ya usalama wetu hasa kwa wote ndani na nje wanaodhani amani yetu inaweza kuchezewa kirahisi.
 
Jk hana lolote!! Akimgusa Kagame maana yake atakuwa anapigana na Mseveni, Kenyata na Kagame.. Ana ubavu???

cattle.jpg
 
Jk hana lolote!! Akimgusa
Kagame maana yake atakuwa anapigana na Mseveni, Kenyata na Kagame.. Ana
ubavu???

cattle.jpg

mkuu, hao uliowataja ni cha mtoto ukilinganisha na marafiki zetu. ukiigusa Tanzania utakuwa umeigusa Marekani, China, Ufaransa, Afrika ya Kusini, Zimbabwe, Namibia na nchi zote za SADC. Tanzania imejitengenezea jina na ina permanent friends ambao ni mataifa makubwa tofauti na hao nyang'au uliowataja
 
Ushauri wako ni mzito sana lkn hofu yangu ni usahihi wa tarifa zoko kwani sina uhakika kama ajira ktk vyombo vyetu vya ulinzi na usalma zinagawiwa kama pipi kiasi kwamba mtu anapewa kama anagawiwa karanga nadhani zinahitaji uchunguuzi wa kina kabla ya kuchukua hatua yoyote
 
Una hakika kama atayafanyia kazi haya?

Mheshimiwa rais,

Kila mzalendo mwenye kupenda taifa hili,amefarijika sana na hotuba yako ya jana ulyoitoa katika kambi ya Kaboya,pale wilayani Muleba,karibu kabisa na kijijini kwetu.Umeonesha na kuudhihirisha ulimwengu kuwa pengine kimya kingi kina mshind😵nyo lako limepeleka ujumbe kwa nchi maadui na rafiki ya kwamba nchi hii iko imara na iko tayari kujilinda na kamwe mtu asidhubutu kutuchezea.

Kama raia mwema,ningependa kutoa ushauri ufuatao ili agizo na karipio lako liwe na mashiko.

1.Kuunda tume ya kijeshi au ya majaji kupitia mfumo mzima wa ajira katika majeshi yetu.Zipo tuhuma kuwa na ni ukweli ulio wazi kuwa nchii hii ina idadi ya wanajeshi,maaskari na maafisa wa ngazi za juu wa Usalama wa taifa, ambao si raia wa nchi hii.Katika hili,waraka wa Mtikila unaodai nchi jirani kupenyeza raia wa nchi zao na kuingia katika vyombo vya usalama,utakusaidia sana

2.Kuzifanyia kazi tuhuma juu ya chama chako,watendaji wako na ikiwezekana kuwafuta kazi mara moja watendaji wa ngazi za juu wa majeshi yetu ambao wamekuwa na tuhuma lukuki.

3.Kumfuta kazi mara moja Waziri wa sasa wa Ulinzi na jeshi la kujenga taifa,ambaye zipo tuhuma za wazi juu ya PHD yake.Ni aibu kwa jeshi kuongozwa na mtu ambaye ni mwongo.Kwa uwezo wake wa namna hiyo siyo kwamba uwepo wake waweza kuwa unachochea roho na moyo wa uasi dhidi ya wanajeshi wetu wapendwa?

4.Kujenga heshima ya Ikulu hasa katika mfumo mzima wa utendaji na utoaji wa matamko.Mtamko yanayotolewa na nyumba yetu pale Magogoni,yamekuwa yakiacha maswali mengi juu ya umakini na mfumo mzima wa utendaji katika nyumba yetu takatifu.Efficiency starts from WITHIN not from WITHOUT.

5.Kujiondoa mara moja katika shrikisho la Afrika Mashariki na kubakia na SADC pamoja na mashirika mengine ya kimataifa ambayo yana lengo la kutunufaisha.Kwa sasa hali ilivyo,kutokana na udhaifu wa watendaji tulionao katika wizara zetu,Wakenya na Waganda,hasa Wakenya,wamelitumia vizuri shirikisho hilo kujichukulia ardhi,kujipatia kazi,kufungua makampuni utitiri bila kufuata kanuni na taratibu za uwekezaji.Hii inapunguza usalama.

6.Kutopuuza kabisa,narudia kutopuuza kabisa malalamiko yanayotolewa na wanajeshi wetu dhidi ya maisha duni na stahili nyingine.Uzoefu unaonesha kuwa,mapinduzi katika nchi nyingi yamefanywa na wanajeshi wa kawaida na wala siyo mabrigedia,makanali wala majenerali.

7.Kuunda Wizara ya vijana peke yao,bila kuichanganya na wizara nyingine.Unda vijiji vya vijana,tunayo mapori mengi nchi hii,yatenge mapori tuliyo nayo,wape zana za kisasa vijana,wazazalishe chakula na uzalendo katika vijiji hivyo.Uangalizi wao uwe chini ya watu wenye upeo na maadili.Wasiwasi wangu ni kuwa kwa hali inavyokwenda,wimbi la vijana wanaohitimu mafunzo ya JKT,wanaofukuzwa toka CCP,wanaomaliza vyuo na shule ni BOMU kama alivyosema mshirika wako Edward.

8.Mwisho kabisa,ikitokea nchi hii iakenda vitani,ni raia wa nchi hii ambao watapigana kuikomboa,ni raia wa nchii hii watakaotoa senti yao ya mwisho ili nchi iwe salama.Jeshi haliwezi kupigana peke yake bila kuungwa mkono na raia.Hivyo basi,kwa hali ilivyo sasa,mahusiano ya majeshi yetu na raia lazima yaangaliwe kwa umakini mkubwa.Matukio ya polisi na wanajeshi wetu katika siku za karibuni,yanazidi kujenga usugu wa chuki miongoni mwa raia.Mshauri Waziri wako Mkuu aombe radhi kwa kauli yake kwa wananchi na azuie vyombo vya usalama kupiga raia.Hii itasaidia kuungwa mkono ikiwa mambo yatakwenda mrama.

Ni ushauri tu Mzee wa Magogoni.
 
Ushauri wako ni mzito sana lkn hofu yangu ni usahihi wa tarifa zoko kwani sina uhakika kama ajira ktk vyombo vyetu vya ulinzi na usalma zinagawiwa kama pipi kiasi kwamba mtu anapewa kama anagawiwa karanga nadhani zinahitaji uchunguuzi wa kina kabla ya kuchukua hatua yoyote

Mkuu,

Nimesema taarifa zilizotolewa na Mtikila kuhusiana na hili,inabidi zifanyiwe kazi.Haimaanishi kuwa mimi nina kitu kubwa zaidi ya waraka huo na tuhuma nyinginezo ambazo zimekuwa zikitolewa.
 
Ushauri wako ni
mzito sana lkn hofu yangu ni usahihi wa tarifa zoko kwani sina uhakika
kama ajira ktk vyombo vyetu vya ulinzi na usalma zinagawiwa kama pipi
kiasi kwamba mtu anapewa kama anagawiwa karanga nadhani zinahitaji
uchunguuzi wa kina kabla ya kuchukua hatua yoyote

Pia Mkuu, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vina utaratibu wa kujichunguza vyenyewe na watumishi wake. pindi inapobainika kuwa utaratibu haukufuatwa katika ajira, wahusika huchukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kushtakiwa na kufukuzwa kazi. hatua hivyo hufanywa ndani ya mahakama za ndani ya vyombo hivi. kwa mantiki hiyo, masuala ya jeshi huwezi kuyashughulikia katika mahakama za kawaida kama inavyopendekezwa
 
Una hakika kama atayafanyia kazi haya?

unavyosikia Rais ujue kuwa ni Taasisi. tatizo kuna watu wanamjudge JK badala ya kuangalia taasisi nzima. halafu vibaraka wa kagame humu JF wanatusumbua sana maana hawajui hata nini maana ya national interests
 
Mkuu taasisi si ina muongozaji lakini? au?
 
Ni ushauri tu Mkuu.Hii nchi ni yetu sote.

nakupongeza sana Mayenga kwa kutekeleza dhana ya uzalendo kivitendo. Tatizo humu JF kuna watu kazi yao ni kulia lia, kukebehi, majungu na kukatisha tamaa wale wanaotoa ushauri mzuri. big up sana mkuu
 
nimeipenda namaba 7....lakini hivi ushauri kama huuu huwa unafika kwa mhusika kweli?
Mheshimiwa rais,

Kila mzalendo mwenye kupenda taifa hili,amefarijika sana na hotuba yako ya jana ulyoitoa katika kambi ya Kaboya,pale wilayani Muleba,karibu kabisa na kijijini kwetu.Umeonesha na kuudhihirisha ulimwengu kuwa pengine kimya kingi kina mshind😵nyo lako limepeleka ujumbe kwa nchi maadui na rafiki ya kwamba nchi hii iko imara na iko tayari kujilinda na kamwe mtu asidhubutu kutuchezea.

Kama raia mwema,ningependa kutoa ushauri ufuatao ili agizo na karipio lako liwe na mashiko.

1.Kuunda tume ya kijeshi au ya majaji kupitia mfumo mzima wa ajira katika majeshi yetu.Zipo tuhuma kuwa na ni ukweli ulio wazi kuwa nchii hii ina idadi ya wanajeshi,maaskari na maafisa wa ngazi za juu wa Usalama wa taifa, ambao si raia wa nchi hii.Katika hili,waraka wa Mtikila unaodai nchi jirani kupenyeza raia wa nchi zao na kuingia katika vyombo vya usalama,utakusaidia sana

2.Kuzifanyia kazi tuhuma juu ya chama chako,watendaji wako na ikiwezekana kuwafuta kazi mara moja watendaji wa ngazi za juu wa majeshi yetu ambao wamekuwa na tuhuma lukuki.

3.Kumfuta kazi mara moja Waziri wa sasa wa Ulinzi na jeshi la kujenga taifa,ambaye zipo tuhuma za wazi juu ya PHD yake.Ni aibu kwa jeshi kuongozwa na mtu ambaye ni mwongo.Kwa uwezo wake wa namna hiyo siyo kwamba uwepo wake waweza kuwa unachochea roho na moyo wa uasi dhidi ya wanajeshi wetu wapendwa?

4.Kujenga heshima ya Ikulu hasa katika mfumo mzima wa utendaji na utoaji wa matamko.Mtamko yanayotolewa na nyumba yetu pale Magogoni,yamekuwa yakiacha maswali mengi juu ya umakini na mfumo mzima wa utendaji katika nyumba yetu takatifu.Efficiency starts from WITHIN not from WITHOUT.

5.Kujiondoa mara moja katika shrikisho la Afrika Mashariki na kubakia na SADC pamoja na mashirika mengine ya kimataifa ambayo yana lengo la kutunufaisha.Kwa sasa hali ilivyo,kutokana na udhaifu wa watendaji tulionao katika wizara zetu,Wakenya na Waganda,hasa Wakenya,wamelitumia vizuri shirikisho hilo kujichukulia ardhi,kujipatia kazi,kufungua makampuni utitiri bila kufuata kanuni na taratibu za uwekezaji.Hii inapunguza usalama.

6.Kutopuuza kabisa,narudia kutopuuza kabisa malalamiko yanayotolewa na wanajeshi wetu dhidi ya maisha duni na stahili nyingine.Uzoefu unaonesha kuwa,mapinduzi katika nchi nyingi yamefanywa na wanajeshi wa kawaida na wala siyo mabrigedia,makanali wala majenerali.

7.Kuunda Wizara ya vijana peke yao,bila kuichanganya na wizara nyingine.Unda vijiji vya vijana,tunayo mapori mengi nchi hii,yatenge mapori tuliyo nayo,wape zana za kisasa vijana,wazazalishe chakula na uzalendo katika vijiji hivyo.Uangalizi wao uwe chini ya watu wenye upeo na maadili.Wasiwasi wangu ni kuwa kwa hali inavyokwenda,wimbi la vijana wanaohitimu mafunzo ya JKT,wanaofukuzwa toka CCP,wanaomaliza vyuo na shule ni BOMU kama alivyosema mshirika wako Edward.

8.Mwisho kabisa,ikitokea nchi hii iakenda vitani,ni raia wa nchi hii ambao watapigana kuikomboa,ni raia wa nchii hii watakaotoa senti yao ya mwisho ili nchi iwe salama.Jeshi haliwezi kupigana peke yake bila kuungwa mkono na raia.Hivyo basi,kwa hali ilivyo sasa,mahusiano ya majeshi yetu na raia lazima yaangaliwe kwa umakini mkubwa.Matukio ya polisi na wanajeshi wetu katika siku za karibuni,yanazidi kujenga usugu wa chuki miongoni mwa raia.Mshauri Waziri wako Mkuu aombe radhi kwa kauli yake kwa wananchi na azuie vyombo vya usalama kupiga raia.Hii itasaidia kuungwa mkono ikiwa mambo yatakwenda mrama.

Ni ushauri tu Mzee wa Magogoni.
 
Mkuu taasisi si ina muongozaji lakini? au?

pamoja na kuwa kila Taasisi kuna muongozaji, Rais pia ana washauri katika masuala mbalimbali. iwe ulinzi na usalama, sheria au uchumi na uwekezaji. jk ni mmoja wa viongozi ambao wanaamini kuwa dhana ya ushirikishaji inaleta matokeo bora. pia anawaamini sana watu wa chini yake. vinginevyo angekuwa dikteta
 
Jogoo awike asiwike asubuhi lazima ifike ushauri umenenepa vizuri tu kivumbi ni je utafika kwa wahusika??
 
Naunga mkono Kauli ya JK na Membe.Foreign powers must respect our territorial intergrity.

Tuache ufisadi sasa tutumie raslimali zetu kunufaisha wananchi na tuimarishe ulinzi wa mipaka yetu kwa kuongeza bajeti ya ulinzi kuya-equip majeshi yetu.Tufanye millitary software and hardware upgrading.Tuachane na figter jets za kizamani maana wenzetu Uganda wamefanya shopping na kununua fighter jets modern kabisa na Kenye walifanya hivyo miaka 4 iliyopita kama mnakumbuka mtafaruku wa kidiplomasia ulioibuka baada ya MV FIONA kuzuiwa na shehena ya silaha nzito zilizokuwepo.Rwanda kupitia wizi wa raslimali za Congo wana figter Jets za masafa ya kati ambazo ni za kisasa kabisa.Sipendezwi na dalili za kurudi kwenye zama za arms race ila unapokua na silaha kali na jeshi vibrant unawatisha hata potential enemies.Kwa Detterence effect unapunguza hostility ya foreign powers dhidi yako.DRC wangekuwa wamejipanga akina Kagame wasingethibutu kudhamini M23

Ni lazima tuwe na taifa linalojiheshimu na pia linalo-command respect kutoka nje.

Kauli za Joyce Banda na Kagame zinachefua kweli kweli.Pamoja na kwamba tunajua JK ni dhaifu lakini sitapenda kuona Rais wa Nje akiitukana taasisi ya Urais na Watanzania kwa ujumla.Huko Rwanda ukipita kwenye forums zao utaona jinsi walivyomuona Kagame Shujaa na kuona Watanzania watu wa ovyo.

Kauli ya kumtaka aingie kwenye Dialogue na waasi inazua matusi mfululizo?Hapo ndipo unapogundua kwamba huyu jamaa hana adabu na hatuchukulii kwa uzito.

Ikitokea sasa hivi kukawa na jaribio kwenye mipaka hasa kutoka Rwanda hakuna haja ya kuongea tena.Let us teach him a lesson.Watanzania tuungane dhidi ya maadui wa nje.Tulinde dignity na pride yetu kama Taifa wakati huo tukirudi nyumbani tusiache kuonyana na kuwajibishana ili tuweze kuwa na taifa linalojiheshimu na linalostahili heshima kimataifa.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom