JK: Ningeboronga CCM ingenitimua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Ningeboronga CCM ingenitimua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyambala, Jun 26, 2010.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  JK: Ningeboronga CCM ingenitimua

  • Atamba anajivunia rekodi yake ya miaka mitano

  RAIS Jakaya Kikwete amesema anaamini iwapo angekuwa ameshindwa kutekeleza kikamilifu Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyomuingiza madarakani mwaka 2005 asingethubutu kugombea tena.

  Kikwete alitoa tambo hizo jana wakati akizungumza na wanachama wa CCM 350 wa Mkoa wa Dar es Salaam waliojitokeza kumdhamini.

  “Inawezekana watu hawaijui vizuri CCM, kama leo ningekuwa nimeboronga ningekuwa nimefukuzwa siku nyingi lakini kutokana na kutekeleza ilani ya chama vizuri, naweza kusimama na kuomba watu wanichague,” alisema.

  Akizungumzia uamuzi wake wa kumteua mwanaye kuzungusha fomu za kusaka wadhamini, Kikwete alisema hakuna tatizo lolote katika kufanya hivyo.

  Kikwete alisema chini ya utaratibu aliouweka, viongozi wa wilaya watakuwa na jukumu la kuandaa fomu za wadhamini zilizoletwa.


  “Wale waliokuwa wakijiuliza maswali nadhani majibu wameyapata…kinachofanywa na hao vijana ni kukusanya fomu ambazo viongozi wamezifanyia kazi kwa kutafuta wadhamini, hivyo kazi ya wanafunzi sio kutafuta wadhamini wao wananiletea wadhamini ambao wamepatikana,” alisema.


  Kikwete anatoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tu tangu Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba, amtetee kwa uamuzi wake wa kumteua Ridhiwani ambao baadhi ya makada na viongozi wa juu wa chama hicho wamekuwa wakiuelezea chinichini kuwa unaoonyesha namna rais alivyopoteza imani kwa viongozi wenzake.


  Wakati Kikwete mwenyewe akitoa taarifa hiyo, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais nayo imelazimika kukanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti moja la kila siku (siyo Tanzania Daima) zilizokuwa zikimtaja waziri wa zamani wa fedha, Zakia Meghji, kuwa ni mtu ambaye yuko katika mawazo ya Kikwete kwa ajili ya kuwa mgombea mwenza wake katika uchaguzi wa Oktoba.


  Mbali ya hilo, Ikulu katika taarifa yake hiyo ya maandishi iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Salvatory Rweyememu, imekanusha kupata kufanyika kwa mawasiliano yoyote kati ya Rais Kikwete na Meghji kuzungumzia wadhifa huo ambao kiitifaki ni wa pili kimamlaka kitaifa.


  “Hayo ni mawazo na matakwa binafsi ya waandishi wa habari, huo katu si msimamo wa Rais Kikwete…Kwa sasa Rais anashukuru suala la mgombea mwenza hajaanza kulishughulikia kwani wakati wake bado. Hivyo maneno hayo hayana chembe ya ukweli,” ilieleza taarifa hiyo.


  Taarifa hiyo ya Ikulu inakuja wakati kukiwa na vuguvugu la chini chini kuhusiana nafasi ya mgombea mwenza ambayo ndiyo itakayotoa makamu wa rais iwapo watashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Kuibuka kwa ubashiri wa mtu gani anayepaswa kushika nafasi hiyo umekuwa mkubwa tangu ibainike kuwa Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, ambaye ndiye aliyekuwa akitarajia kuwa mgombea mwenza achukue fomu ya kugombea urais wa Zanzibar.
  My Take:

  1. Ni lini CCM imewahi kumfukuza kiongozi wake katika ngazi ya kitaifa kwa sababu ya kuboronga in the last 30yrs?

  2. Ktk vitu vyote vinavyonifurahisha ni jamaa kujittutumua eti ana rekodi ya mafanikio ya miaka mitano. Hivi kwa hali iliyopo Tz sasa haoni hata aibu kulisema hilo?

  3. Wa kulaumiwa in huge terms ni wananchi maana wao ndiyo wanaona na kufeel hicho kinachoitwa rekodi lakini hawako tayari kukanusha wala kuhoji........
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jun 26, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Tambalism ni tabia ya kawaida ya waswahili hata tukiboronga vipi; hatuna tabia ya kukubali makosa.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,606
  Likes Received: 82,206
  Trophy Points: 280
  Aboronge mara ngapi tena!? Amesahau kwamba baadhi ya Wakongwe ndani ya CCM walitamka hadharani kwamba CCM ina utamaduni wa kuachiana ili Rais wa kutoka chama chao amalize awamu zake mbili? Lowassa, Mramba, Karamagi, Rostam, Chenge, Mkono na wengine wengi wamethibika kama ni mafisadi. CCM kama ingekuwa ina utamaduni wa kutimuana hawa wote wangetimuliwa Bungeni lakini kwa kuwa hawana utamaduni huo bado wanapeta tu na si ajabu wakapitishwa tena kugombea 2010.
   
 4. m

  magee Senior Member

  #4
  Jun 26, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  nimemnukuu mkulu hapo juu jamani..........ana haki ya kusema hivi,ni kweli watu wengi hawaijui ccm na ndo maana wako tayari kuipigia kura tena kifupi nimemsoma mkuu anachosema ni kuwa ccm inapenda yote anayoyafanya......na ndo maana haijamfukuza.
  ...........changanya na zakwako!!!
  1+1=11
   
 5. m

  magee Senior Member

  #5
  Jun 26, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  nimemnukuu mkulu hapo juu jamani..........ana haki ya kusema hivi,ni kweli watu wengi hawaijui ccm na ndo maana wako tayari kuipigia kura tena kifupi nimemsoma mkuu anachosema ni kuwa ccm inapenda yote anayoyafanya......na ndo maana haijamfukuza.
  ...........changanya na zakwako!!!
  1+1=11
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Wacha usanii wewe JK.

  CCM ingekutimua kama ilivyomtimua mwenyekiti wake yupi hapo nyuma? CCM ina rekodi gani ya kutimua mwenyekiti wa taifa? CCM ina rekodi gani ya kumbadilisha mgombea urais baada ya term moja? Si kuna kiongozi wa juu mooja kasema juzikati hapa (Karume I believe) kwamba CCM haina utamaduni wa kubadilisha viongozi?

  Sasa hizi kamba za miguuni za kwamba CCM ingekutimua zimetoka wapi? Si tumeona kina Nyerere walivyoiendesha CCM kama familia, completely with changing rules of engagement during the game to favor Mkapa, sasa unataka kutuambia CCM ni institution?

  CCM si institution, ni watu, na mtu mwenye nguvu kuliko wote ni wewe JK, in essence wewe ndiye the embodiment of CCM personified, sasa CCM gani hiyo ambayo ingekufukuza? Ungejifukuza mwenyewe? I mean huwezi hata kupata mpinzani wa nomination ya CCM from within CCM.

  What a joke.
   
 7. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  This man is naive and has no sense of honesty .. Hata mtoto mdogo atakuwa ashamed na shallow arguments kama hizi
   
 8. R

  Ramos JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ukisema wanashutumiwa, utakuwa umewatendea haki zaidi...
   
 9. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  "Wale waliokuwa wakijiuliza maswali nadhani majibu wameyapata…kinachofanywa na hao vijana ni kukusanya fomu ambazo viongozi wamezifanyia kazi kwa kutafuta wadhamini, hivyo kazi ya wanafunzi sio kutafuta wadhamini wao wananiletea wadhamini ambao wamepatikana," alisema.Hapa sijaelewa, Hivi Ridhuani ni mwanafunzi wa chuo kipi? I mean majuzi tumeshuhudia akikabidhiwa cheti cha uwakili..kwamba yeye ni mfanyakazi.
  Really confused with these statements
   
 10. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Jk ni mwenekiti wa CCM taifa ana nguvu kuliko hata CCM yenyewe. Sasa anaposema kuwa CCM ingemtimua kama angeboronga huku si kudaganya hazarani? au ndo kukosa maneno ya kusema. Au anaposema kuboronga anakuwa na maana gani? kwa maana nanayoijua mimi JK hana haki ya kusimama hazarani na kusema hajaboronga. ni mambo mangapi ameharibu ambayo yanaonyesha hayuko makini? Kwa kifupi kauli yake hii ni ya kisiasa zaidi. na tutaskia mengi sana kipindi hiki hadi octoba
   
 11. R

  Ramos JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hivi zaidi ya kukanusha habari za waandishi, Salva huwa ana kazi gani ikulu? Inakuwaje anatudanganya kuwa suala la mgombea binafsi halijaanza kushughulikiwa... ina maana wanatuambia watakurupuka tu na kuibua mtu yeyote siku ya mwisho? Salva awe makini na majibu yake hasa kwenye masuala yanayogusa maslahin ya taifa kama hili....
   
 12. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hili ni tusi la leja leja kwa wanaCCM, poleni.
   
 13. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hivi huyu JK huwa ankurupuka tu na kuanza kuongea au huwa anafikiri kwanza! aaaa nimekumbuka huyu ni mkwere bana halafu watu aliokuwa anaongea nao wana uwezo wa kufikiri na kutunza kumbukumbu kama wake na alijua tu hatomuhoji! KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI (!)....wote KIGUMUUUUUU!
   
 14. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Huyu Slva naye, zamani kabla ya kuhamia ikulu nilikuwa namwona ana akili kweli. Lakini tangu aende ikulu sijui amekuwaje hata simwuelewi, ni kama uwezo wake wa kufikiri umepungua vile. Ni hisia zangu tu.
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  This guy is just a fraud!
   
 16. Bourgeoisie

  Bourgeoisie JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Salva hawezi tena kuwa na akili ya kuwatetea wananchi kama ilivyokuwa mwanzo maana kwa sasa anaona tayari yuko peponi, akutetee ili aikose?
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Salva kashawahi kutetea wananchi? Lini? Wapi?
   
 18. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #18
  Jun 27, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  KATIKA CCM CCM NI RAIS MWENYEWE WENGINEO NI BENDERA KUFUATA UPEPO NANI ATAKAE MTIMUA MUNGU WA CCM TANZANIA UKITAKA KUIBA BILA KUSUMBULIWA ,KUKWEPA KODI KWA WAFANYABIHASHARA NA KUFANYA MAMBO BILA KUSUMBULIWA JIUNGE NA ccm CCM NI KICHAKA CHA KILA MAOVU UFISADI,RUSHWA N.K KUNAWATU WANAOINGIA ccm SIO KWA KUPENDA BALI BILA KUJIUNGA NA ccm MLANGO UMEFUNGWA HAYA YANAMWISHO MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 19. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  I am amazed,since when did con-men have any sense of honesty?
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jamani lakini ukweli ni kwamba JK hakuboronga ndani ya chama. Kawatajirisha karibu wote tofauti na Mkapa ambaye alikuwa na kundi lake. Kila aliyeingia madarakani CCM ameondoka Tajiri..Sasa utaboronga vipi ikiwa umewatajirisha wanachama wako..

  Kwa hiyo binafsi sioni makosa ktk kauli yake, aliweka ahadi ya kuwa na mabillionea 100 wamefika zaidi ya 150.. nani mwenye record kama yake?..
   
Loading...