Ndoto za Mchana hizi!...Hakuna anayeweza kubadilishwa na Maneno ya kitoto ya JK anayoongea sasa...The fact is, wafanyakazi walikejeliwa, na vitabu vya zama hizo viliandika, na bahati mbaya sana hawezi kuvifikia vitabu hivyo kufuta alichotamka!
Lakini pia hali ya maisha inaeleza vizuri zaidi kuwa hakufanya, na hataweza kufanya jipya!
IMEMFIKA PABAYA MKUU NA NDIO MANA "SUKARI" INAMSHUKA JUKWANI...
Kampeni za kuhamasisha wafanyakazi kumnyima kura JK zasambazwa Send to a friend 0diggsdigg
Daniel Mjema,Moshi
KAULI ya Rais Jakaya Kikwete kuwa hahitaji kura za wafanyakazi wa sekta ya umma nchini wapatao 350,000 inazidi kumgharimu kufuatia hatua ya uhamasishaji inayofanywa kupitia mtandao wa Internet pamoja na fulana kutompigia kura Rais Kikwete kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Fulana hizo tayari zimeanza kusambazwa mitaani huku wengine wakisambaza taarifa hizo kwa kasi kupitia barua pepe kwa wafanyakazi mbalimbali wa serikali na wasomi, miongoni wakiwepo wa vyuo Vikuu.
Fulana hiyo yenye rangi ya kijani ambayo ni rangi rasmi ya chama cha mapinduzi(CCM) pia zilionekana zikiwa zimevaliwa na wafuasi wa Chadema, kwenye mapokezi ya kuingia Jijini Dar es Salaam, jana.
Fulana hizo zina picha ya Rais Kikwete akiwa amevalia suti nyeusi akinyoosha mkono na juu yake kukiwa na maneno: "sihitaji kura za Wafanyakazi."
Akihutubia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika wiki ya kwanza ya Mei, mwaka huu, Rais Kikwete alisema kwamba serikali haina uwezo wa kupandisha mishahara wa kima cha chini hadi Sh 315,000 kama Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi (Tucta) inavyoshinikiza.
Kwa sababu hiyo, akasema kama shinikizo ni kwamba lazima awaongezee hadi kufikia kiwango hicho ndipo watamchagua tena katika uchaguzi wa mwaka huu, ni heri wasimpe kura zao.
Uchunguzi wa kina wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa barua pepe hizo zinazolenga kupunguza kura za Rais Kikwete zilianza kusambazwa miezi miwili iliyopita ambapo kila aliyetumiwa ujumbe huo, unaonyesha karibu watu milioni moja wamekwishaupata.
Barua pepe hizo zinazosambazwa kwa kasi zimedai kuwa tangu rais atoe kauli hiyo alipozungumza na wazee wa Dar Es Salaam Mei 3 mwaka huu, hajawahi kusikika akibadili kauli yake hiyo au kuwaomba radhi wafanyakazi.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati kukiwa na vuguvugu la mvutano mkubwa kati ya serikali na Tucta ambao walikuwa wanahamasisha wafanyakazi nchi nzima kugoma.
"Na hadi leo sijasikia kama amebadili kauli yake ile au kuomba radhi wafanyakazi wa Tanzania. Mimi najiuliza maswali haya: Je, wafanyakazi wana haja ya kumchagua mtu aliyewakana?" wanahoji wanaosambaza ujumbe huo.
Ujumbe huo ambao unaonyesha baadhi ya anuani za wasomi wa vyuo vikuu unaendelea kuhoji: "Je, kuna haja ya kumchagua mtu ambaye kwa kauli yake ameonyesha kutokujali mchango wa wafanyakazi katika ujenzi wa taifa hili?"
Kupitia ujumbe huo, wafanyakazi wanahamasishwa kumchagua mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Wilbroad Slaa ambaye sasa anatumia kauli hiyo ya Rais kama moja ya silaha zake katika mikutano ya hadhara ya kuomba adhaminiwe.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa Mwananchi Jumapili, kila aliyetumiwa ujumbe huo kwa njia ya barua pepe naye alitakiwa awatumie watu kati ya 50 na 100.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa, wanabashiri kuwa kauli hiyo ya Rais pamoja na kukubalika kwa Dk Slaa miongoni mwa wapiga kura na wananchi, huenda ikaiathiri ndoto ya Rais Kikwete ya kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.
Endapo wafanyakazi wote watashikilia msimamo wa kutomchagua, kura atakazopoteza Rais Kikwete kutoka kwa wafanyakazi zitakuwa zaidi ya 350,000 hasa ikizingatiwa kila mfanyakazi ana familia na ndugu wanaowategemea.
Katika mikutano yake ya hadhara mikoa mbalimbali nchini anakopita kutafuta wadhamini, Dk Slaa amewaomba wafanyakazi wampe kura hizo 350,000 ili akomeshe kiburi na jeuri ya Rais Jakaya Kikwete kwa wafanyakazi.
Rais Kikwete anahesabika kuwa Rais wa kwanza barani Afrika aliyechaguliwa kwa kura nyingi zaidi ukilinganisha na Marais wa Nchi nyingine za Kiafrika ambapo matokeo yake yanaelezwa kuwa yalivunja rekodi.
Katika uchaguzi uliofanyika Disemba 2005, Rais Kikwete alipata kura 9,123,952 sawa na asilimia 80.28 ya kura halali 11,365,477 akifuatiwa kwa mbali na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF aliyepata kura 1,327,125.
Kauli ya hivi karibuni kabisa ya Rais Kikwete wakati akichukua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ni kwamba wana CCM hawapaswi kudharau vyama vya siasa vya upinzani.
Kampeni za kuhamasisha wafanyakazi kumnyima kura JK zasambazwa
Picha na Saidi
YouTube - Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wazee wa Dar III (MichuziBlog)
YouTube - JK akiwachimba mkwala Tucta
YouTube - SEHEMU YA PILI YA HOTUBA YA RAISI JAKAYA MRISHO KIWETE KWA WAFANYAKAZI