Elections 2010 JK - Ni matusi kudai sijali wafanyakazi!!! Mh!

Kwa nini utafute kukumbukwa kwa mema wakati ni wajibu wa msingi? Hii inamaanisha kuwa you had your shot lakini hutaka kufanya yaliyo mema na leo unakurupuka huko kwenye kampeni zako unakuja kutuambia unataka eti kukumbukwa kwa mema!
sana sana tutakukumbuka kwa
Ushikaji
Rais mtembeza bakuli
Mfuga mafisadi
Ahadi tele bila utaekelezaji (eti train na mabasi ya kwenda kasi) yaletwe na nani? CCM hii tunayoijua?
By the way hebu naomba kukumbushwa mradi wowote mkubwa wa barabara ambao umeanzishwa awamu hii ya nne na umetekelezwa kwa ukamilifu?
 
Mimi nadhani si lazima aseme yeye... ndio maana tuna wasomi wa hali ya, all we need ni hawa wachumi wetu wa vyuo vikuu wafanye hiyo analysis na ndio itumike na wapinzani ku-counter punch rather than kusubiri yeye afanye.. HE WILL NEVER DO THAT BECAUSE IT WILL BE LIKE SHOOTING YOURSELF MIGUUNI

mimi nadhani kauli ya Rais katika kila jambo ina uzito wa pekee kuliko kauli za viongozi wote. Kipindi kama hiki cha kampeni Rais hana budi kuweka sawa kumbukumbu ambazo zitakisaidia chama chake kupata ushindi hasa kuelekea uchaguzi mkuu. Wakati huo huo viongozi wengine washiriki katika kutoa ufafanuzi kupitia kampeni za ubunge na udiwani.
 
Anayo haki JK kulambisha maneno alambishayo. Wafanyakazi mmekuwa mkipiga makelele daima dumu, anajua mnataka kubembelezwa na kaamua aropoke aropokayo kwenu, anajua mtampa kura zenu tu. SI mnajua mbwa mkali hapigi makelele bali anang'ata silently? Ukiona mbwa anakubwatukia sana na kukuonyesha meno yake yote mdomoni ujue anakutishia tu, hana lolote la kukufanya. Debe tupu hamjui linavyotika? Mlevi anapiga makelele mengi ili kujihami tu, hata bila kumgusa utamkuta anajifanya kukupiga teke lakini anapiga hewani na kudondoka pasipo kuguswa.

Wafanyakazi mweleweni JK, mnapaswa kumjibu kwa vitendo kwa kumrudi siku ya uchaguzi kama kweli mko serious. Mnajidai watu wa vijijini ndio watakaompatia kura nyingi kwa ujinga wao, sasa tudhihirishieni kama nyie mlio wasomi mtacheza role model wajinga wajifunze kwenu. Kelele za mpangaji hazimzuii mwenye nyumba kulala usingizi, kama vile kelele za vyura kudai maji yote ni yake hazimzuii tembo kunywa maji yale, hata kama chura ataamua kukojolea na kunyea humo humo ili kukomoa.

Wake up wafanyakazi, kulialia hakuleti tija. Will you?

kelele za vyama vya upinzani kuitumia mitandao kuomba kura za wafanyakazi ni ndoto ya mchana. Wafanyakazi weredi wameliona hilo sasa wanahitaji sera kwani santuli/CD ya wimbo wa Kikwete alizikataa kura za wafanyakazi umechuja/tumeuchoka.
 
kelele za vyama vya upinzani kuitumia mitandao kuomba kura za wafanyakazi ni ndoto ya mchana. Wafanyakazi weredi wameliona hilo sasa wanahitaji sera kwani santuli/CD ya wimbo wa Kikwete alizikataa kura za wafanyakazi umechuja/tumeuchoka.

Ndoto za Mchana hizi!...Hakuna anayeweza kubadilishwa na Maneno ya kitoto ya JK anayoongea sasa...The fact is, wafanyakazi walikejeliwa, na vitabu vya zama hizo viliandika, na bahati mbaya sana hawezi kuvifikia vitabu hivyo kufuta alichotamka!
Lakini pia hali ya maisha inaeleza vizuri zaidi kuwa hakufanya, na hataweza kufanya jipya!
 
nimemsikia jana mpaka nimetaka kucheka..anakana kuwa hakusema hazitaki kura za wafanyakazi..hahaaaa JK kazi unayo maneno yako ya kuropoka ropoka sasa ngoma ndo hiyo...we si uliwaita wafanya kazi mbayuwayu

Ni kweli katika hotuba yake kwa Wazee wa Dar es salaam hakukataa kura za wafanyakazi. Alikuwa anafafanua kuwa mpango wa TUCTA ukitekelezwa serikali itayumba kwenye uwekezaji katika maeneo mengine ya uchumi kama vile kutengeneza barabara, afya, maji na elimu. Kwa Rais muongo angeweza kudanganya kwamba anakubaliana na madai ya TUCTA kisha akaongopa zaidi kwamba atapandisha kwa awamu mbili ile ya sasa na ingine mwezi Januari 2011. baada ya hapo uchaguzi ukipita anagoma kuongeza mshahara. ni bora kuambiwa ukweli kuliko uongo. Katika siasa hakuna jambo jepesi kama kutoa ahadi kwa wapiga kura hiyo ndiyo salaam namba moja. Kutoa ahadi ni rahisi lakini kutekeleza ni kitu kingine ndipo hapo utaamua kusuka ama kunyoa kujua kwamba anachoahidi Dr Slaa au Lipumba atakitekeleza au la ....siri iko moyoni mwa mgombea. Wafanyakazi kazi kwenu kosa moja linaweza kuwagharimu miaka fikiri mara mbili kabla hujaamua nani utampa kura yako.
 
Ndoto za Mchana hizi!...Hakuna anayeweza kubadilishwa na Maneno ya kitoto ya JK anayoongea sasa...The fact is, wafanyakazi walikejeliwa, na vitabu vya zama hizo viliandika, na bahati mbaya sana hawezi kuvifikia vitabu hivyo kufuta alichotamka!
Lakini pia hali ya maisha inaeleza vizuri zaidi kuwa hakufanya, na hataweza kufanya jipya!

IMEMFIKA PABAYA MKUU NA NDIO MANA "SUKARI" INAMSHUKA JUKWANI...


Kampeni za kuhamasisha wafanyakazi kumnyima kura JK zasambazwa Send to a friend 0diggsdigg

Daniel Mjema,Moshi
KAULI ya Rais Jakaya Kikwete kuwa hahitaji kura za wafanyakazi wa sekta ya umma nchini wapatao 350,000 inazidi kumgharimu kufuatia hatua ya uhamasishaji inayofanywa kupitia mtandao wa Internet pamoja na fulana kutompigia kura Rais Kikwete kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Fulana hizo tayari zimeanza kusambazwa mitaani huku wengine wakisambaza taarifa hizo kwa kasi kupitia barua pepe kwa wafanyakazi mbalimbali wa serikali na wasomi, miongoni wakiwepo wa vyuo Vikuu.

Fulana hiyo yenye rangi ya kijani ambayo ni rangi rasmi ya chama cha mapinduzi(CCM) pia zilionekana zikiwa zimevaliwa na wafuasi wa Chadema, kwenye mapokezi ya kuingia Jijini Dar es Salaam, jana.


Fulana hizo zina picha ya Rais Kikwete akiwa amevalia suti nyeusi akinyoosha mkono na juu yake kukiwa na maneno: "sihitaji kura za Wafanyakazi."


Akihutubia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika wiki ya kwanza ya Mei, mwaka huu, Rais Kikwete alisema kwamba serikali haina uwezo wa kupandisha mishahara wa kima cha chini hadi Sh 315,000 kama Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi (Tucta) inavyoshinikiza.


Kwa sababu hiyo, akasema kama shinikizo ni kwamba lazima awaongezee hadi kufikia kiwango hicho ndipo watamchagua tena katika uchaguzi wa mwaka huu, ni heri wasimpe kura zao.



Uchunguzi wa kina wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa barua pepe hizo zinazolenga kupunguza kura za Rais Kikwete zilianza kusambazwa miezi miwili iliyopita ambapo kila aliyetumiwa ujumbe huo, unaonyesha karibu watu milioni moja wamekwishaupata.

Barua pepe hizo zinazosambazwa kwa kasi zimedai kuwa tangu rais atoe kauli hiyo alipozungumza na wazee wa Dar Es Salaam Mei 3 mwaka huu, hajawahi kusikika akibadili kauli yake hiyo au kuwaomba radhi wafanyakazi.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati kukiwa na vuguvugu la mvutano mkubwa kati ya serikali na Tucta ambao walikuwa wanahamasisha wafanyakazi nchi nzima kugoma.


"Na hadi leo sijasikia kama amebadili kauli yake ile au kuomba radhi wafanyakazi wa Tanzania. Mimi najiuliza maswali haya: Je, wafanyakazi wana haja ya kumchagua mtu aliyewakana?" wanahoji wanaosambaza ujumbe huo.

Ujumbe huo ambao unaonyesha baadhi ya anuani za wasomi wa vyuo vikuu unaendelea kuhoji: "Je, kuna haja ya kumchagua mtu ambaye kwa kauli yake ameonyesha kutokujali mchango wa wafanyakazi katika ujenzi wa taifa hili?"

Kupitia ujumbe huo, wafanyakazi wanahamasishwa kumchagua mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Wilbroad Slaa ambaye sasa anatumia kauli hiyo ya Rais kama moja ya silaha zake katika mikutano ya hadhara ya kuomba adhaminiwe.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Mwananchi Jumapili, kila aliyetumiwa ujumbe huo kwa njia ya barua pepe naye alitakiwa awatumie watu kati ya 50 na 100.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa, wanabashiri kuwa kauli hiyo ya Rais pamoja na kukubalika kwa Dk Slaa miongoni mwa wapiga kura na wananchi, huenda ikaiathiri ndoto ya Rais Kikwete ya kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.

Endapo wafanyakazi wote watashikilia msimamo wa kutomchagua, kura atakazopoteza Rais Kikwete kutoka kwa wafanyakazi zitakuwa zaidi ya 350,000 hasa ikizingatiwa kila mfanyakazi ana familia na ndugu wanaowategemea.

Katika mikutano yake ya hadhara mikoa mbalimbali nchini anakopita kutafuta wadhamini, Dk Slaa amewaomba wafanyakazi wampe kura hizo 350,000 ili akomeshe kiburi na jeuri ya Rais Jakaya Kikwete kwa wafanyakazi.

Rais Kikwete anahesabika kuwa Rais wa kwanza barani Afrika aliyechaguliwa kwa kura nyingi zaidi ukilinganisha na Marais wa Nchi nyingine za Kiafrika ambapo matokeo yake yanaelezwa kuwa yalivunja rekodi.

Katika uchaguzi uliofanyika Disemba 2005, Rais Kikwete alipata kura 9,123,952 sawa na asilimia 80.28 ya kura halali 11,365,477 akifuatiwa kwa mbali na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF aliyepata kura 1,327,125.

Kauli ya hivi karibuni kabisa ya Rais Kikwete wakati akichukua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ni kwamba wana CCM hawapaswi kudharau vyama vya siasa vya upinzani.

Kampeni za kuhamasisha wafanyakazi kumnyima kura JK zasambazwa
2dwatk2.jpg



Picha na Saidi

YouTube - Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wazee wa Dar III (MichuziBlog)

YouTube - JK akiwachimba mkwala Tucta

YouTube - SEHEMU YA PILI YA HOTUBA YA RAISI JAKAYA MRISHO KIWETE KWA WAFANYAKAZI
 
Mimi na mke wangu ni wafanyakazi wa uma na kura zetu ni kwa JK.

Dubo una akili za kujitegemea. Kumkataa Kikwete au kumkubali iwe ni akili yako sio kushinikizwa na wanablog wenzetu. Hapa tujadili hoja sio kwamba mchague fulani na usimchague fulani. Hizo ni kampeni za kipuuzi na hazifai. Wapo marafiki zangu wengi tu huko serikalini wanasema kuliko kumpa kura Dr Slaa ama Lipumba ni heri waendelee kumbana KIKWETE na serikali yake kuongeza maslahi yao. Wao wanaamini kwamba sio kwamba Kikwete hajafanya jambo lolote kwao huo ni uongo wa mchana bali kile alichowapa hakitoshi kulingana na hali halisi jambo ambalo linazungumzika. Wanakiri kwamba mkwele huyu kajitahidi sana sana kurekebisha mambo, hasa kupandisha vyeo vya wafanyakazi waliokuwa wamesahaulika miaka ya huko nyumba, kuajiri zaidi, kuwainua wanawake serikalini, kukusanya kodi kutoka milioni 195 hadi milioni 450 kwa mwezi na kumaliza mpasuko wa zanzibar.
 
Tunajua umetumwa. Au wewe ni MS nini?
dubo
user-online.png
Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join Date Mon Aug 2010
Posts 43
Thanks : 5
Thanked 6 Times in 5 Posts
Rep Power0

Wote wanaokuwa na hoja hasa za kulinda hadhi ya jamiiforums kwa maana ya kutosimama upande katika masuala magumu ya kitaifa mnasema wametumwa hizo ni fikra nyepesi. Lakini wale wanaotetea Chadema,CUF na wagombea wake hawajatumwa...mmmmmmh. Hapa jamvini ukisimama tu kumtetea kikwete umetumwa kuweni na fikra mbadala kwamba humu ndani kila mtu ana mgombea wake basi
 
Poa tu, kwani kuna mtu kakuzuia? Mpatie hata huyo mama... kipenda roho...:eyeroll2::A S 8:

Wanaokosa hoja utawajua tu ndio sababu CCM hawana matusi humu ndani. Chadema na CUF utawajua tu kwa lugha za kutukana humu mtandaoni. Wafanyakazi mpo, wanaosema kikwete aliwatukana na wao wanatukana humu ndani lakini wanadai tuwape nchi. Kikwete katangaza kufanya kampeni za kistaarabu na wafuasi wake fanyeni hivyo. mkitukanwa msijibu kwa matusi toeni hoja zitawarudisha Ikulu.
 
Ohh wamekwisha anza!!!...mnyonge mnyongeni haki yake mpeni...nadhani kauli ya JK kila mwenye masikio alisikia na kila mwenye akili timamu alitafsiri kwa upeo wa akili yake . sasa nashangazwa na watu timamu walio makini kulishwa maneno na kutaka jamii iamini kile wanachokiamini wao..ni busara kila mtu apewe nafasi achuje pumba na mchele ni upi. si busara kutaka wote wafanane mitazamo juu ya kauli ya JK coz kila mtu anajua kutafsiri kilichosemwa hivyo si HAKI kumshawishi mtu asimpe kura mgombea yeyote (hata JK) kwa kuwa tu yeye binafsi hakufurahishwa na kitu fulani au kauli fulani (kama mjadala huu ulivyo). nakumbuka alisema yuko radhi kuzikosa kura za wafanyakazi na Mgaya akasema JK kazikataa kura za wafanyakazi...nasi sote tumeingia kwenye malumbano juu ya kauli hizi za JK na Mgaya...kwanini tusitumie busara zetu kuamua mambo?(mf kumpa au kumnyima kura mgombea)...kama hatuwezi basi ijulikane kabisa kuwa hapa kuna namna fulani ya kampeni dhidi ya JK na chama chake..iwekwe wazi ili wachangiaji wajue mada hizi zinatumika kupigia debe chama fulani coz nimeona watu wanachangia kwa ku-base judgement zao kwenye tafsiri moja tu ya kauli ile ( tafsiri ya Mgaya) wakti ambapo kabla mgaya hajazungumza mtazamo huo haukuwepo je ndio kusema watu hawakuelewa kama alivyoelewa mgaya toka mwanzo mpaka alipozungumza? hii inanipa hofu kuwa kuna mengi tutajikuta tunaamua kwa kusikia flani kasema basi nasi tunachukua mtazamo huo kama wetu na kujikuta tunaafanya maamuzi yasiyo sahihi...tubadilike kila mtu awe na mtazamo wake juu ya jambo husika kwa kulifanyia uchunguzi wa kina na ndipo ufanye uamuzi.
So,kila mtu achague kiongozi amtakaye kwa kumsikiliza na kushawishika na sera zake na si kwa kuambiwa na mtu mwingine kama wengine wanavyojaribu kuwaambia wafanyakazi wasimpe kura JK...all in all, maisha yako si ya mwenzako so waweza kushawishi kundi fulani lisimpe kura na mwishowe wakampa nadhani itauma zaidi kwani kura huwa ni siri so huwezi jua, pia unaweza kushawishika kumbe aliekushawishi hana shida kama zako..(ofkoz hatulingani hata kama wote tuna shida)... kila mtu atumie haki yake ya kuchagua kiongozi amtakaye yeye na si kuchagua kwa kuwa wanaJF wachache wameamua huo ndio uwe msimamo wa JF na wafanyakazi walio JF.

mwenye kuelewa na akuelewe ni uchambuzi mfupi lakini mzuri kwa wale wenye akili timamu ni lazima kujua malengo ya washiriki wa JF. Mwanzilishi wa JF ana lengo zuri lakini kuna watu wanatumia jukwaa hili kuendesha kampeni mbaya dhidi ya baadhi ya wagombea na hasa Kikwete. Mimi naamini kwamba mtazamo mbaya dhidi ya kikwete umeanza kumpandisha chati kikwete kwani tulioanza kushtuka tupo wengi humu ndani.
 
"Mfa maji haachi kutapatapa". JK ameshaona kachemka mbaya na kauli yake, si kweli kuwa kashau ila amegundua kuwa Slaa anatumia kauli yake kummaliza kitu ambacho sisi kama wafanyakazi kimetuudhi sana.Kisha bado anatufananisha wafanyakazi na baamedi kweli, hii si dharau jamani?, yaani sisi tunafanya kazi grosari? aghaaaa sipati picha ya rais kiazi kama huyu.Mi nasema WAFANYAKAZI HATUDANGANYIKI, kura zote kwa yule aliyetamka mapema kuwa anatujali sisi wafanyakazi.Lakini malipo hapa hapa duniani, si tunamuachia Mungu.

"Mungu tusaidie tuepukane na serikali hii ya CCM, maana inatunyanyasa na kututesa waja wako" Amen.


Kweli kabisa maneno yako "mfa maji haachi kutapatapa" mimi nilikuwa mfanyakazi zamani nawaungeni mkono kuwa msimamo wenu huo huo mpeni kura mwenye imani na uchungu wa wafanyakazi sio propaganda kama za msanii wetu na dharau kubwa na kejeli hana lolote
 
watampa tu ingawa anawatusi kila siku

Mkuu nimeona signature yako, kama yangu vile!! Munishi 'mwimbaji wa nyimbo za injili wakati huo' alisema wazi kwenye moja ya nyimbo zake; Wakubwa wakapiga Marufuku kanda hiyo isisambazwe. Kazi ipo mwaka huu....
 
kelele za vyama vya upinzani kuitumia mitandao kuomba kura za wafanyakazi ni ndoto ya mchana. Wafanyakazi weredi wameliona hilo sasa wanahitaji sera kwani santuli/CD ya wimbo wa Kikwete alizikataa kura za wafanyakazi umechuja/tumeuchoka.
Eti mitandao tumeichoka wakati wewe toka asubuhi umo humu JF.
 
Dubo una akili za kujitegemea. Kumkataa Kikwete au kumkubali iwe ni akili yako sio kushinikizwa na wanablog wenzetu. Hapa tujadili hoja sio kwamba mchague fulani na usimchague fulani. Hizo ni kampeni za kipuuzi na hazifai. Wapo marafiki zangu wengi tu huko serikalini wanasema kuliko kumpa kura Dr Slaa ama Lipumba ni heri waendelee kumbana KIKWETE na serikali yake kuongeza maslahi yao. Wao wanaamini kwamba sio kwamba Kikwete hajafanya jambo lolote kwao huo ni uongo wa mchana bali kile alichowapa hakitoshi kulingana na hali halisi jambo ambalo linazungumzika. Wanakiri kwamba mkwele huyu kajitahidi sana sana kurekebisha mambo, hasa kupandisha vyeo vya wafanyakazi waliokuwa wamesahaulika miaka ya huko nyumba, kuajiri zaidi, kuwainua wanawake serikalini, kukusanya kodi kutoka milioni 195 hadi milioni 450 kwa mwezi na kumaliza mpasuko wa zanzibar.
Usitake kuzuga watu hapa huo ujanja wako feki, eti unamchimba Dubo asishirikiane na mke wake kupiga kura mbona wewe unashirikiana na wafanyakazi wa serikalini, toa ujanja mbuzi wako, kura zetu hazipati bosi wako si amezikataa na tumeshaambiwa kama mtu hataki pilau ya nini umlazimishe. Wewe na Dubo lenu moja kutetea uongo wa JK ila elewa hapa huwa hatusomi maandishi pekee tunasoma hadi akili ya mwandishi.
 
Wanaokosa hoja utawajua tu ndio sababu CCM hawana matusi humu ndani. Chadema na CUF utawajua tu kwa lugha za kutukana humu mtandaoni.
Na wewe kama umeishiwa kalale utamjuaje huyu ni chadema au CUF, ina maana wewe kwa kumtetea Kikwete umekuwa CCM. Usi generalize mambo humu wewe toa hoja basi kama umeshindwa kutetea uongo wa rais wako mwache mwenyewe aendelee kujitetea.
 
Mimi na mke wangu ni wafanyakazi wa uma na kura zetu ni kwa JK.

Wewe naomba nikuite dubu kwanza wewe na mkeo mkipigia kura tutawajuaje kama sio ndio nyie vibaraka mnaopokea posho kila siku za vikao vya extraordinary halafu mnadai mlifanya mkutano muhimu sana. Kawaida binaadamu ana tamaa sidhani kama nyie mtataka hizi posho ziondoke hivyo lazima mumpigie kura JK. Na swali je kama mnampigia kura JK so what? Inatusaidia nini labda itatusaidia zaidi mkitueleza JK amewafanyia kipi mpaka mkashawishika kumpigia kura!!!!!
 
Ni nyie waanachama wa chadema ambao hamtompa kura Kikwete,wengine 80% tuliobakia tumepenga na kuazimia kumpa kura mkwere amalizie kazi aliyoianza.Sasa nyie na huyo padre wenu mtaula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua!Ukichukia chukua sumu ujiueeeee!

Sawa mzee hiyo 80% umeitoa wapi au ni 80% of wafanyakazi 20,000 ambao wanapata posho za ajabu ajabu serikali kwa vigezo visivyo na msingi. Kama ni ratio hiyo basi 80% ya 20,000 ya wafanyakazi 400,000 unakuta wewe na hao majeuri wenzio ni kama 4% ya wafanyakazi wote. Nendeni tu ndio nyie vibaraka
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom