JK - Ni matusi kudai sijali wafanyakazi!!! Mh! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK - Ni matusi kudai sijali wafanyakazi!!! Mh!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mdondoaji, Aug 23, 2010.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  RAIS Jakaya Kikwete amesema ni matusi anapoambiwa kwamba hajali maslahi ya wafanyakazi nchini, wakati serikali yake imekuwa ikiboresha maslahi ya wafanyakazi mwaka hadi mwaka na kusisitiza kuwaheshimu wafanyakazi hao na itaendelea kuboresha stahili zao.

  Aidha, amewaahidi mazuri zaidi Watanzania katika miaka mitano ijayo, akisema anataka kukumbukwa kwa mema katika uongozi wake, na si zaidi ya hayo.

  Rais Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiomba kura za wananchi wa Jiji la Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, ambako maelfu ya wakazi wa jiji hili walifurika kumsikiliza katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya mkoani Mwanza, ikiwa ni siku ya pili tangu azindue kampeni juzi jijini Dar es Salaam.

  Mgombea huyo wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema anaona hatendewi haki juu ya suala la maslahi ya wafanyakazi kwa sababu tangu aingie madarakani Desemba 2005, Serikali yake ya Awamu ya Nne imekuwa ikiboresha maslahi ya wafanyakazi mara kwa mara kadri uwezo unaporuhusu.

  “Tumekuwa tukiboresha maslahi ya wafanyakazi tangu tuingie madarakani. Maslahi ya umma na sekta binafsi yamekuwa yakiboreka na tumeweka taratibu za kisheria na kuunda kamati za kisekta kushughulikia masuala ya maslahi.

  Kuna watu walikuwa wanalipwa shilingi elfu orobaini na nane sasa wanalipwa zaidi ya shilingi themanini elfu,” alisema Kikwete na kuongeza: “Tulipoingia tulikuta kima cha chini ya mshahara ni shilingi elfu sitini na tano, tukapandisha hadi shilingi sabini na tano; kisha shilingi laki moja, na baadaye laki moja na nne na majuzi kimefika shilingi laki moja na thelathini na tano.

  Kwa kweli tumeboresha maslahi hayo kila mara uwezo unaporuhusu. “Kwa hiyo, nikiambiwa mimi sijali maslahi ya wafanyakazi, ni matusi, naona sitendewi haki.”

  Rais Kikwete alisema tofauti kati ya Serikali na Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi (TUCTA) ni suala la kutaka kima cha chini kiwe Sh 315,000; jambo alilosisitiza kwamba kwa uwezo wa serikali sasa, haiwezekani.

  “Mwenye grosari hawezi kulipa shilingi laki tatu, atakwambia nenda kajiajiri mwenyewe, vivyo hivyo kwa mwenye baa. Ndiyo tulichosema kwa Tucta, msemakweli mpenzi wa Mungu, hatukiwezi, mapato hayatoshi, leo hii ukilipa hivyo, utapata wapi fedha za ruzuku kwa wakulima, dawa, kununua vivuko,” alisema Rais Kikwete.

  “Ndio maana tumesema si haki, haiwezekani… na ndipo msuguano wetu na Tucta. Tumewaambia haiwezekani. Lakini sasa wameyapindua, wanasema sizitaki kura za wafanyakazi.

  Lakini wanasahau kauli zao za Dar es Salaam wakati wa Mei Mosi mwaka huu…walisema watamchagua kiongozi atakayewalipa shilingi laki tano na elfu kumi na tano. Na mabango yao yaliandikwa hivyo. Mla kunde anasahau, lakini mtupa maganda, hasahau.”

  Rais Kikwete alisema kwamba kauli yake aliyoitoa haikuwahi kukataa kura za wafanyakazi, bali alieleza kuwa kama sharti ni hilo la kuongeza kima cha mshahara na kufikia Sh 315,000, “basi kura hizo tumezikosa.”

  “Nilieleza kuwa kama sharti ni kuweka kima hicho cha chini, basi kura hizo tumezikosa. Hatutaweza kulipa kiwango hicho. Leo mbaya mie, wazuri wao, kweli akutukanaye hakuchagulii tusi.

  “Tunawaheshimu wafanyakazi, ni watu muhimu, tutaendelea kuwaongeza maslahi kwa kadri ya uwezo wetu wa mapato na wajibu wa serikali. Hatuna ugomvi nao wala kinyongo.

  Kura hata moja kwangu ni muhimu, siwezi kuikataa, lakini kama sharti ni hilo, kura hizo tumezikosa. Watatupa wengine.

  “Hata hivyo, naamini katika wafanyakazi wapo wanachama wazuri wa CCM, wapenzi wa CCM, wanaojua chuya au pumba na mchele. Hivyo, tunaamini na sisi CCM tutapata kura za kutosha, kuongoza nchi hii.”

  Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya miaka mitano iliyopita, aliwaambia maelfu ya wananchi hao wa Mwanza kwamba imetekelezwa kikamilifu na ushahidi ni ujenzi wa vivuko mbalimbali; barabara za lami za jiji hilo na zinazokwenda mikoa mingine; uwezeshaji wa wananchi na uwekezaji.

  “Kwa mtaji huo, nawaahidi mambo mazuri zaidi katika miaka mitano ijayo kwa kuwaachia nchi iliyo nzuri zaidi, kwani nataka Watanzania wanikumbuke kwa mema, sitaki nikumbukwe kwa lolote jingine,” alisema Rais Kikwete katika mkutano uliopambwa na burudani za aina mbalimbali hasa za muziki wa kizazi kipya.

  Source: Habari Leo.

  Mtazamo:


  Ijapokuwa mheshimiwa hatupendi sie wafanyakazi but at least awe muwazi na mkweli kwa wananchi wasioelewa nini kinaendelea. Anasema ametuongezea mshahara but ukiangalia mshahara umeongeza na kodi pia imeongezeka. Leo mshahara anausema ameuongeza hazungumzi kaongeza kodi kiasi gani? Pia anasema kuwa ameboresha maisha ya mfanyakazi but leo mfanyakazi analipwa 200,000 but hata nauli ya basi inamshinda kwasababu ya kukua kwa gharama za maisha.

  Anasema kuwa mwenye grosari anaweza kushindwa kulipa 350,000 kwa baamedi kwani baamedi na mfanyakazi wa serikali ni sawa? na kama ni hivyo basi ni kwanini hakupunguza kodi kwa wafanyabiashara ndogo na kuwapa subsidies ili waweze kulipa hicho kima cha chini. Kama anavyosema kuwa ndani ya wafanyakazi wapo wanaCCM wazuri na pia wapo wafanyakazi wazuri wanaomsikiliza kwa makini wakapambanua chuya na pumba zipi. Wakati bajeti ya safari zake Ulaya inalisha bajeti ya wafanyakazi serikalini na private sector. Wakuu wa idara za mawizara wanajinunulia malandcruiser yenye thamani ya kulisha wafanyakazi wasiopungua 20,000 wangelitazama zaidi katika kupunguza hizi gharama ili kuboresha maisha ya mfanyakazi. Kuliko kutwambia tumpe kura ili aboreshe maisha yetu miaka mitano ijayo. Kuna kipengele katika sheria kinasema mkataba bila consideration yeyote ni null and void ndio hizi statement za tumpe kura atatufanyia makubwa miaka mitano ijayo kwani anaweza kugeuka baadae tukabakia tunalia tu!!!! Nilikuwapo!!!
   
 2. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kura yako ni nini kwani?
   
 3. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Wafanyakazi msimamo wetu uko palepale wa kutompa kura CCM na JK wake.

  Anazidi kutuudhi, tuna mipango mingi ya kumnyima kura
   
 4. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ingefaa aeleze mshahara wa kima cha chini umepanda kwa asilimia ngapi, na bei ya bidhaa muhimu kama mafuta ya taa sukari unga nk. zimepanda kwa asilimia ngapi!
  Kwa kifupi huwezi kupandisha mshahara kwa zaidi ya 100% na bei ya bidhaa ipande kwa zaidi ya 300% halafu useme unajali wafanyakazi!
   
 5. f

  freddywm Member

  #5
  Aug 23, 2010
  Joined: Jun 13, 2007
  Messages: 17
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 5
  Na hizo dawa anazozungumzia mbona hakuna, ukienda kwenye zahanati na hospitali za wilaya, ni aibu, watu wa chini wanateseka sana jamani
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mimi nadhani si lazima aseme yeye... ndio maana tuna wasomi wa hali ya, all we need ni hawa wachumi wetu wa vyuo vikuu wafanye hiyo analysis na ndio itumike na wapinzani ku-counter punch rather than kusubiri yeye afanye.. HE WILL NEVER DO THAT BECAUSE IT WILL BE LIKE SHOOTING YOURSELF MIGUUNI
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Anayo haki JK kulambisha maneno alambishayo. Wafanyakazi mmekuwa mkipiga makelele daima dumu, anajua mnataka kubembelezwa na kaamua aropoke aropokayo kwenu, anajua mtampa kura zenu tu. SI mnajua mbwa mkali hapigi makelele bali anang'ata silently? Ukiona mbwa anakubwatukia sana na kukuonyesha meno yake yote mdomoni ujue anakutishia tu, hana lolote la kukufanya. Debe tupu hamjui linavyotika? Mlevi anapiga makelele mengi ili kujihami tu, hata bila kumgusa utamkuta anajifanya kukupiga teke lakini anapiga hewani na kudondoka pasipo kuguswa.

  Wafanyakazi mweleweni JK, mnapaswa kumjibu kwa vitendo kwa kumrudi siku ya uchaguzi kama kweli mko serious. Mnajidai watu wa vijijini ndio watakaompatia kura nyingi kwa ujinga wao, sasa tudhihirishieni kama nyie mlio wasomi mtacheza role model wajinga wajifunze kwenu. Kelele za mpangaji hazimzuii mwenye nyumba kulala usingizi, kama vile kelele za vyura kudai maji yote ni yake hazimzuii tembo kunywa maji yale, hata kama chura ataamua kukojolea na kunyea humo humo ili kukomoa.

  Wake up wafanyakazi, kulialia hakuleti tija. Will you?
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwa watu ambao ni wepesi wa kusahau, hizi kauli za kulia lia (kama vile anatongoza) tayari zimewaingiza mkenge!! Inaonekana jamaa ni mtaaalamu sana wa kupiga sound. Ila ingekuwa vizuri wanaompenda JK wakampatia hotuba yake ila ya Diamond aisikilize tena!

  Kweli mtaka cha uvunguni sharti ainame. Si angefanya hivyo siku zote au ile jeuri imeenda wapi? Mhhh kazi ipo kweli kweli

  This time, siyo "maisha bora kwa kila Mtanzania"? Kweli siasa ni mchezo wa kipuuzi. Unasahau hata nyimbo ulizotunga mwenyewe!!!:becky::becky:
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kama angeangalia namna bidhaa zilivyopanda bei wala asingepiga kelele kuwa kaongeza mishahara ya kima cha chini.
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mimi nashauri Mgaya na viongozi wa TUCTA wanyamaze tu wasijibizane naye wao wameshamaliza jukumu ni letu wafanyakazi tutakutana na JK kwenye sanduku la kura.

  Najua JK kuzikataa kura za wafanyakazi lime mtachi sana sasa anatafuta pa kutolea hasira na tageti ni Mgaya ajibu halafu aagize vyombo vya sheria vimkamate ili kuwatisha wafanyakazi.

  Lakini whatever the case JK will never succeed on this case na kadri anavyojitetea ndivyo anavyopandisha machungu ya wafanyakazi na ndivyo anavyozidi kuzipunguza kura.
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  nimemsikia jana mpaka nimetaka kucheka..anakana kuwa hakusema hazitaki kura za wafanyakazi..hahaaaa JK kazi unayo maneno yako ya kuropoka ropoka sasa ngoma ndo hiyo...we si uliwaita wafanya kazi mbayuwayu
   
 12. L

  Luiza Gama Senior Member

  #12
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hoja ya mishahara ya watumishi. Si tu wa serikali, hapo wanaongelewa wafanyakazi wote wa Tanzani. nadhani unakielewa chombo cha TUCTA .sijui, kuna watanzania wangapi wana uwezo wa kuwalipa watumishi wao wa ndani angalau sh 150,000/=.JK ni mkweli nia na kiu ya kuboresha maslai ya wafanyakazi anayo na amekuwa akifanya hivyo mara kadhaa tokea aingie madarakani.Mwenye masikio na asikie. JK hajatusi hata kidogo. Na watanzania wa leo ni waelewa hawaburuzwi kifikra wamemuelewa sana.UOTE=Mdondoaji;1041489]RAIS Jakaya Kikwete amesema ni matusi anapoambiwa kwamba hajali maslahi ya wafanyakazi nchini, wakati serikali yake imekuwa ikiborzwesha maslahi ya wafanyakazi mwaka hadi mwaka na kusisitiza kuwaheshimu wafanyakazi hao na itaendelea kuboresha stahili zao.ha

  Aidha, amewaahidi mazuri zaidi Watanzania katika miaka mitano ijayo, akisema anataka kukumbukwa kwa mema katika uongozi wake, na si zaidi ya hayo.

  Rais Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiomba kura za wananchi wa Jiji la Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, ambako maelfu ya wakazi wa jiji hili walifurika kumsikiliza katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya mkoani Mwanza, ikiwa ni siku ya pili tangu azindue kampeni juzi jijini Dar es Salaam.

  Mgombea huyo wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema anaona hatendewi haki juu ya suala la maslahi ya wafanyakazi kwa sababu tangu aingie madarakani Desemba 2005, Serikali yake ya Awamu ya Nne imekuwa ikiboresha maslahi ya wafanyakazi mara kwa mara kadri uwezo unaporuhusu.

  "Tumekuwa tukiboresha maslahi ya wafanyakazi tangu tuingie madarakani. Maslahi ya umma na sekta binafsi yamekuwa yakiboreka na tumeweka taratibu za kisheria na kuunda kamati za kisekta kushughulikia masuala ya maslahi.

  Kuna watu walikuwa wanalipwa shilingi elfu orobaini na nane sasa wanalipwa zaidi ya shilingi themanini elfu," alisema Kikwete na kuongeza: "Tulipoingia tulikuta kima cha chini ya mshahara ni shilingi elfu sitini na tano, tukapandisha hadi shilingi sabini na tano; kisha shilingi laki moja, na baadaye laki moja na nne na majuzi kimefika shilingi laki moja na thelathini na tano.

  Kwa kweli tumeboresha maslahi hayo kila mara uwezo unaporuhusu. "Kwa hiyo, nikiambiwa mimi sijali maslahi ya wafanyakazi, ni matusi, naona sitendewi haki."

  Rais Kikwete alisema tofauti kati ya Serikali na Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi (TUCTA) ni suala la kutaka kima cha chini kiwe Sh 315,000; jambo alilosisitiza kwamba kwa uwezo wa serikali sasa, haiwezekani.

  "Mwenye grosari hawezi kulipa shilingi laki tatu, atakwambia nenda kajiajiri mwenyewe, vivyo hivyo kwa mwenye baa. Ndiyo tulichosema kwa Tucta, msemakweli mpenzi wa Mungu, hatukiwezi, mapato hayatoshi, leo hii ukilipa hivyo, utapata wapi fedha za ruzuku kwa wakulima, dawa, kununua vivuko," alisema Rais Kikwete.

  "Ndio maana tumesema si haki, haiwezekani… na ndipo msuguano wetu na Tucta. Tumewaambia haiwezekani. Lakini sasa wameyapindua, wanasema sizitaki kura za wafanyakazi.

  Lakini wanasahau kauli zao za Dar es Salaam wakati wa Mei Mosi mwaka huu…walisema watamchagua kiongozi atakayewalipa shilingi laki tano na elfu kumi na tano. Na mabango yao yaliandikwa hivyo. Mla kunde anasahau, lakini mtupa maganda, hasahau."

  Rais Kikwete alisema kwamba kauli yake aliyoitoa haikuwahi kukataa kura za wafanyakazi, bali alieleza kuwa kama sharti ni hilo la kuongeza kima cha mshahara na kufikia Sh 315,000, "basi kura hizo tumezikosa."

  "Nilieleza kuwa kama sharti ni kuweka kima hicho cha chini, basi kura hizo tumezikosa. Hatutaweza kulipa kiwango hicho. Leo mbaya mie, wazuri wao, kweli akutukanaye hakuchagulii tusi.

  "Tunawaheshimu wafanyakazi, ni watu muhimu, tutaendelea kuwaongeza maslahi kwa kadri ya uwezo wetu wa mapato na wajibu wa serikali. Hatuna ugomvi nao wala kinyongo.

  Kura hata moja kwangu ni muhimu, siwezi kuikataa, lakini kama sharti ni hilo, kura hizo tumezikosa. Watatupa wengine.

  "Hata hivyo, naamini katika wafanyakazi wapo wanachama wazuri wa CCM, wapenzi wa CCM, wanaojua chuya au pumba na mchele. Hivyo, tunaamini na sisi CCM tutapata kura za kutosha, kuongoza nchi hii."

  Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya miaka mitano iliyopita, aliwaambia maelfu ya wananchi hao wa Mwanza kwamba imetekelezwa kikamilifu na ushahidi ni ujenzi wa vivuko mbalimbali; barabara za lami za jiji hilo na zinazokwenda mikoa mingine; uwezeshaji wa wananchi na uwekezaji.

  "Kwa mtaji huo, nawaahidi mambo mazuri zaidi katika miaka mitano ijayo kwa kuwaachia nchi iliyo nzuri zaidi, kwani nataka Watanzania wanikumbuke kwa mema, sitaki nikumbukwe kwa lolote jingine," alisema Rais Kikwete katika mkutano uliopambwa na burudani za aina mbalimbali hasa za muziki wa kizazi kipya.

  Source: Habari Leo.

  Mtazamo:


  Ijapokuwa mheshimiwa hatupendi sie wafanyakazi but at least awe muwazi na mkweli kwa wananchi wasioelewa nini kinaendelea. Anasema ametuongezea mshahara but ukiangalia mshahara umeongeza na kodi pia imeongezeka. Leo mshahara anausema ameuongeza hazungumzi kaongeza kodi kiasi gani? Pia anasema kuwa ameboresha maisha ya mfanyakazi but leo mfanyakazi analipwa 200,000 but hata nauli ya basi inamshinda kwasababu ya kukua kwa gharama za maisha.

  Anasema kuwa mwenye grosari anaweza kushindwa kulipa 350,000 kwa baamedi kwani baamedi na mfanyakazi wa serikali ni sawa? na kama ni hivyo basi ni kwanini hakupunguza kodi kwa wafanyabiashara ndogo na kuwapa subsidies ili waweze kulipa hicho kima cha chini. Kama anavyosema kuwa ndani ya wafanyakazi wapo wanaCCM wazuri na pia wapo wafanyakazi wazuri wanaomsikiliza kwa makini wakapambanua chuya na pumba zipi. Wakati bajeti ya safari zake Ulaya inalisha bajeti ya wafanyakazi serikalini na private sector. Wakuu wa idara za mawizara wanajinunulia malandcruiser yenye thamani ya kulisha wafanyakazi wasiopungua 20,000 wangelitazama zaidi katika kupunguza hizi gharama ili kuboresha maisha ya mfanyakazi. Kuliko kutwambia tumpe kura ili aboreshe maisha yetu miaka mitano ijayo. Kuna kipengele katika sheria kinasema mkataba bila consideration yeyote ni null and void ndio hizi statement za tumpe kura atatufanyia makubwa miaka mitano ijayo kwani anaweza kugeuka baadae tukabakia tunalia tu!!!! Nilikuwapo!!!
  [/QUOTE]
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Poa tu, kwani kuna mtu kakuzuia? Mpatie hata huyo mama... kipenda roho...:eyeroll2::A S 8:
   
 14. L

  Luiza Gama Senior Member

  #14
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usiwadanganye haoo
   
 15. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  sasa kwani lazima utuambie. utaachaje kumpigia JK wakati wote ni wale wale wakuangukaanguka
   
 16. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  ====
  Mbona mke wako kaniambia haimpi JK! Sasa amua wewe nani mkweli kati ya mke wako au mimi niliyeambiwa na mke wako.
   
 17. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  "Mfa maji haachi kutapatapa". JK ameshaona kachemka mbaya na kauli yake, si kweli kuwa kashau ila amegundua kuwa Slaa anatumia kauli yake kummaliza kitu ambacho sisi kama wafanyakazi kimetuudhi sana.Kisha bado anatufananisha wafanyakazi na baamedi kweli, hii si dharau jamani?, yaani sisi tunafanya kazi grosari? aghaaaa sipati picha ya rais kiazi kama huyu.Mi nasema WAFANYAKAZI HATUDANGANYIKI, kura zote kwa yule aliyetamka mapema kuwa anatujali sisi wafanyakazi.Lakini malipo hapa hapa duniani, si tunamuachia Mungu.

  "Mungu tusaidie tuepukane na serikali hii ya CCM, maana inatunyanyasa na kututesa waja wako" Amen.
   
 18. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Jakaya Mrisho Kikwete....

  Took him 5yrs to lean....

  Dah!!
   
 19. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Mie naamini wakati huu JK hata akiahidi kupeleka Watanzania wote Mbinguni bado kura watampa Slaa. Ahadi za JK ni za uongo. Na Watanzania wameshagundua hilo.

  JK ni kiongozi wa CCM. Chama ambacho kimehodhi madaraka miaka yote, na bila kuleta maendeleo. Watanzania ambao karibu wote hawapati hata maji safi ya kunywa wataendelea kuichagua CCM kwa kisa gani? Hakuna maji, hakuna umeme, hakuna Elimu, kisha unawaambia unafanya vizuri? Unataka wakueleweje?
   
 20. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Amepoteza mvuto na ukweli ni kwamba afya yake ina mgogoro. Akishinda, ya Nigeria yakitufika sitashangaa maana makamu wake naye hali ndo sijui ni mbaya zaidi.... :) :) tehe teheee:A S 8:
   
Loading...