Elections 2010 JK - Ni matusi kudai sijali wafanyakazi!!! Mh!

Ohh wamekwisha anza!!!...mnyonge mnyongeni haki yake mpeni...nadhani kauli ya JK kila mwenye masikio alisikia na kila mwenye akili timamu alitafsiri kwa upeo wa akili yake . sasa nashangazwa na watu timamu walio makini kulishwa maneno na kutaka jamii iamini kile wanachokiamini wao..ni busara kila mtu apewe nafasi achuje pumba na mchele ni upi. si busara kutaka wote wafanane mitazamo juu ya kauli ya JK coz kila mtu anajua kutafsiri kilichosemwa hivyo si HAKI kumshawishi mtu asimpe kura mgombea yeyote (hata JK) kwa kuwa tu yeye binafsi hakufurahishwa na kitu fulani au kauli fulani (kama mjadala huu ulivyo). nakumbuka alisema yuko radhi kuzikosa kura za wafanyakazi na Mgaya akasema JK kazikataa kura za wafanyakazi...nasi sote tumeingia kwenye malumbano juu ya kauli hizi za JK na Mgaya...kwanini tusitumie busara zetu kuamua mambo?(mf kumpa au kumnyima kura mgombea)...kama hatuwezi basi ijulikane kabisa kuwa hapa kuna namna fulani ya kampeni dhidi ya JK na chama chake..iwekwe wazi ili wachangiaji wajue mada hizi zinatumika kupigia debe chama fulani coz nimeona watu wanachangia kwa ku-base judgement zao kwenye tafsiri moja tu ya kauli ile ( tafsiri ya Mgaya) wakti ambapo kabla mgaya hajazungumza mtazamo huo haukuwepo je ndio kusema watu hawakuelewa kama alivyoelewa mgaya toka mwanzo mpaka alipozungumza? hii inanipa hofu kuwa kuna mengi tutajikuta tunaamua kwa kusikia flani kasema basi nasi tunachukua mtazamo huo kama wetu na kujikuta tunaafanya maamuzi yasiyo sahihi...tubadilike kila mtu awe na mtazamo wake juu ya jambo husika kwa kulifanyia uchunguzi wa kina na ndipo ufanye uamuzi.
So,kila mtu achague kiongozi amtakaye kwa kumsikiliza na kushawishika na sera zake na si kwa kuambiwa na mtu mwingine kama wengine wanavyojaribu kuwaambia wafanyakazi wasimpe kura JK...all in all, maisha yako si ya mwenzako so waweza kushawishi kundi fulani lisimpe kura na mwishowe wakampa nadhani itauma zaidi kwani kura huwa ni siri so huwezi jua, pia unaweza kushawishika kumbe aliekushawishi hana shida kama zako..(ofkoz hatulingani hata kama wote tuna shida)... kila mtu atumie haki yake ya kuchagua kiongozi amtakaye yeye na si kuchagua kwa kuwa wanaJF wachache wameamua huo ndio uwe msimamo wa JF na wafanyakazi walio JF.

Sio wafanyakazi wote wenye kuweza kunyambua kila linalosemwa na sio wote wanaweza kukotoa hesabu za kisanii za serikali hivyo hapa JF watu hatumpigii debe Dr Slaa Professa Lipumba au JK bali tunajaribu kuchambua kila mmoja anasema nini ili mwenye macho afumbuke asiyenayo aendelee kukaa tu kwenye kiza.
 
Dubo una akili za kujitegemea. Kumkataa Kikwete au kumkubali iwe ni akili yako sio kushinikizwa na wanablog wenzetu. Hapa tujadili hoja sio kwamba mchague fulani na usimchague fulani. Hizo ni kampeni za kipuuzi na hazifai. Wapo marafiki zangu wengi tu huko serikalini wanasema kuliko kumpa kura Dr Slaa ama Lipumba ni heri waendelee kumbana KIKWETE na serikali yake kuongeza maslahi yao. Wao wanaamini kwamba sio kwamba Kikwete hajafanya jambo lolote kwao huo ni uongo wa mchana bali kile alichowapa hakitoshi kulingana na hali halisi jambo ambalo linazungumzika. Wanakiri kwamba mkwele huyu kajitahidi sana sana kurekebisha mambo, hasa kupandisha vyeo vya wafanyakazi waliokuwa wamesahaulika miaka ya huko nyumba, kuajiri zaidi, kuwainua wanawake serikalini, kukusanya kodi kutoka milioni 195 hadi milioni 450 kwa mwezi na kumaliza mpasuko wa zanzibar.

Mie sikatai JK kuna mazuri amefanya but kuna mabaya mengi pia amefanya. Unasema amepandisha vyeo (kwa mujibu wa maneno yako) but hivyo vyeo vimepanda sekta gani? Kuna sekta nyengine watu walikuwa wakilia lia mfano Sekta ya afya au umesahau? Ameongeza mshahara hivi wewe nikuulize swali wakati Mkapa anaondoka madarakani mkate ulikuwa unanunua bei gani? au Nauli ilikuwa bei gani? Sasa hivi ni bei gani? Watanzania wengi sasa wanakula mlo moja kwa siku ndio unayaita maendeleo ya nchi haya? Umesema ameajiri zaidi lakini kinachofanyika serikalini ni kwamba ameongeza mzigo wa gharama wa serikali kwa kuajiri watu wengi zaidi kufanya kazi ambayo ingelifanywa na mtu mmoja. Mfano afisa forodha mikoani unakuta ilikuwa kazi ya mtu mmoja sasa hivi unawakuta vijana wanasinzia tu mkoani wote maofisa forodha ndio ameongeza ajira kwa kuajiri watu wasiochangia katika serikali badala yake kuliongezea taifa gharama za uendeshaji???? Kodi imekusanywa zaidi nikuulize unajua kodi imepanda kiasi gani kipindi hicho? Kuhusu mpasuko wa zanzibar ndio kabisa JK hayumo tusimpe sifa asiyostahili
 
Kweli kabisa maneno yako "mfa maji haachi kutapatapa" mimi nilikuwa mfanyakazi zamani nawaungeni mkono kuwa msimamo wenu huo huo mpeni kura mwenye imani na uchungu wa wafanyakazi sio propaganda kama za msanii wetu na dharau kubwa na kejeli hana lolote

Iliwahi kusemwa hapa JF kwamba ndani ya CCM kuna mpasuko mkubwa na wanachama kadhaa watajitokeza kumpinga kikwete ili asipewe kipindi cha pili na baadhi yetu tukadiriki kutaja majina ya akina Sumaye, Lowassa, Mwandosya, Malecela na wengineo. Kikwete hakupata upinzani wowote ndani ya chama chake na siku ya kuteua mgombea urais ndani ya chama kikongwe cha CCM Kikwete akaibuka na ushindi mnono wa asilimia 99.
 
Usitake kuzuga watu hapa huo ujanja wako feki, eti unamchimba Dubo asishirikiane na mke wake kupiga kura mbona wewe unashirikiana na wafanyakazi wa serikalini, toa ujanja mbuzi wako, kura zetu hazipati bosi wako si amezikataa na tumeshaambiwa kama mtu hataki pilau ya nini umlazimishe. Wewe na Dubo lenu moja kutetea uongo wa JK ila elewa hapa huwa hatusomi maandishi pekee tunasoma hadi akili ya mwandishi.

wewe hutetei uongo Dr Slaa?
 
Na wewe kama umeishiwa kalale utamjuaje huyu ni chadema au CUF, ina maana wewe kwa kumtetea Kikwete umekuwa CCM. Usi generalize mambo humu wewe toa hoja basi kama umeshindwa kutetea uongo wa rais wako mwache mwenyewe aendelee kujitetea.

Na wewe unarudia kosa la mwenzio mbona na wewe umekuja juu kama vile Dr Slaa ni chaguo lako? acha kila mmoja atetee wa kwake kama ndio hivyo. Unadhani JF ni ya Chadema tu na wa vyama vingine wamo humu ndani.
 
Wewe naomba nikuite dubu kwanza wewe na mkeo mkipigia kura tutawajuaje kama sio ndio nyie vibaraka mnaopokea posho kila siku za vikao vya extraordinary halafu mnadai mlifanya mkutano muhimu sana. Kawaida binaadamu ana tamaa sidhani kama nyie mtataka hizi posho ziondoke hivyo lazima mumpigie kura JK. Na swali je kama mnampigia kura JK so what? Inatusaidia nini labda itatusaidia zaidi mkitueleza JK amewafanyia kipi mpaka mkashawishika kumpigia kura!!!!!

Tutajuaje na wewe kama sio kibaraka wa Dr Slaa unayetegemea kunufaika na Urais wake kama ilivyo kwa mwenzako unayedai ni kibaraka wa kikwete?
 
Wafanyakazi tutampa Kikwete kura zetu. Tunasubiri tu vilio humu jf pamoja na kampeni chafu dhidi ya kikwete. hatudanganyiki
Kibaraka wa CCM sema mimi nitampigia kura Kikwete sio tutampigia...Ukweli ni kwamba performance ya Kikwete kwenye uchumi wa TZ ni extremely poor, inflation ambayo ni moja ya kigezo imepanda sana toka aingie madarakani (toka 7%-14%). Dar tu haina maji safi na salama, infact maji tu hakuna!! Purchasing power ya mtz imeshuka sana, watu masikini wameongezeka, wizi na rushwa ndo usiseme ikiwa na maana kuwa serikali yake haina strong institutions ya kuondoa tatizo hilo!!
Wewe mpigie kura ila mie hapana kwa sababu i just do not see a better future with Kikwete as a president.
 
Wafanyakazi tutampa Kikwete kura zetu. Tunasubiri tu vilio humu jf pamoja na kampeni chafu dhidi ya kikwete. hatudanganyiki

Hivi hawa new member wanaotoa statement hizi ndio wanaojiandikisha humu JF kumtetea JK? Anyway safi karibuni but usiseme wafanyakazi sema wewe na akili zako mtampigia JK na sio wafanyakazi. Nakutakia kila la kheri
 
Wewe naomba nikuite dubu kwanza wewe na mkeo mkipigia kura tutawajuaje kama sio ndio nyie vibaraka mnaopokea posho kila siku za vikao vya extraordinary halafu mnadai mlifanya mkutano muhimu sana. Kawaida binaadamu ana tamaa sidhani kama nyie mtataka hizi posho ziondoke hivyo lazima mumpigie kura JK. Na swali je kama mnampigia kura JK so what? Inatusaidia nini labda itatusaidia zaidi mkitueleza JK amewafanyia kipi mpaka mkashawishika kumpigia kura!!!!!

Wapambe wa Rais mtarajiwa Dr Slaa wana matusi sina hakika tukiwapa nchi watatutukana kwa kiwango kipi. Hapo wako nje ya mamlaka ya dola wakipewa je? Ukiona binadamu anashindwa kuzuia hasira zake huko akiimba kwamba yeye ni mtu safi ogopa sana. sio rahisi kusonga mbele kimaendeleo kwa matusi. Wapiga kura kazi kwenu, mimi sidanganyiki. Ikulu ni mahali patakatifu sio pango la matusi.
 
KATUNI(255).jpg
Wafanyakazi tutampa Kikwete kura zetu. Tunasubiri tu vilio humu jf pamoja na kampeni chafu dhidi ya kikwete. hatudanganyiki

Changanya na za kwako. Ukiwa mzima huwezi kumpa aliyekutukana akijua huna umuhimu. Ukimpa basi ujue wewe sio mzima.
 
Mie sikatai JK kuna mazuri amefanya but kuna mabaya mengi pia amefanya. Unasema amepandisha vyeo (kwa mujibu wa maneno yako) but hivyo vyeo vimepanda sekta gani? Kuna sekta nyengine watu walikuwa wakilia lia mfano Sekta ya afya au umesahau? Ameongeza mshahara hivi wewe nikuulize swali wakati Mkapa anaondoka madarakani mkate ulikuwa unanunua bei gani? au Nauli ilikuwa bei gani? Sasa hivi ni bei gani? Watanzania wengi sasa wanakula mlo moja kwa siku ndio unayaita maendeleo ya nchi haya? Umesema ameajiri zaidi lakini kinachofanyika serikalini ni kwamba ameongeza mzigo wa gharama wa serikali kwa kuajiri watu wengi zaidi kufanya kazi ambayo ingelifanywa na mtu mmoja. Mfano afisa forodha mikoani unakuta ilikuwa kazi ya mtu mmoja sasa hivi unawakuta vijana wanasinzia tu mkoani wote maofisa forodha ndio ameongeza ajira kwa kuajiri watu wasiochangia katika serikali badala yake kuliongezea taifa gharama za uendeshaji???? Kodi imekusanywa zaidi nikuulize unajua kodi imepanda kiasi gani kipindi hicho? Kuhusu mpasuko wa zanzibar ndio kabisa JK hayumo tusimpe sifa asiyostahili

Kikwete ndiye aliyepandisha mishahara ya madakitari kutoka kima cha chini cha 224,000 hadi 480,000. Hivyo, alipandisha mara mbili (zaidi ya asilimia 100), kiasi hiki si cha kutosha lakini kinajibu nia njema ya Rais kwa wafanyakazi kwamba akipewa muda zaidi atafanya makubwa kwa sekta mbalimbali. Ni makosa kudhani sekta zote za serikali kima cha chini ni 135,000/=. Nenda TRA, Benki Kuu, Ewura, sumatra, tanroads na kwingineko kima cha chini sio hicho. Wapo wafanyakazi wa kutosha kumpa kura kikwete kwa imani kwamba maeneo ambayo hajayafikia kuongeza kima cha chini atafanya hivyo katika kipindi cha pili na alishasema hilo huko nyuma.
 
Mie sikatai JK kuna mazuri amefanya but kuna mabaya mengi pia amefanya. Unasema amepandisha vyeo (kwa mujibu wa maneno yako) but hivyo vyeo vimepanda sekta gani? Kuna sekta nyengine watu walikuwa wakilia lia mfano Sekta ya afya au umesahau? Ameongeza mshahara hivi wewe nikuulize swali wakati Mkapa anaondoka madarakani mkate ulikuwa unanunua bei gani? au Nauli ilikuwa bei gani? Sasa hivi ni bei gani? Watanzania wengi sasa wanakula mlo moja kwa siku ndio unayaita maendeleo ya nchi haya? Umesema ameajiri zaidi lakini kinachofanyika serikalini ni kwamba ameongeza mzigo wa gharama wa serikali kwa kuajiri watu wengi zaidi kufanya kazi ambayo ingelifanywa na mtu mmoja. Mfano afisa forodha mikoani unakuta ilikuwa kazi ya mtu mmoja sasa hivi unawakuta vijana wanasinzia tu mkoani wote maofisa forodha ndio ameongeza ajira kwa kuajiri watu wasiochangia katika serikali badala yake kuliongezea taifa gharama za uendeshaji???? Kodi imekusanywa zaidi nikuulize unajua kodi imepanda kiasi gani kipindi hicho? Kuhusu mpasuko wa zanzibar ndio kabisa JK hayumo tusimpe sifa asiyostahili
.

kuhusu suala la maridhiano Zanzibar hata maalimu Seif Shariff Hamad alishakiri na kumpa sifa hadharani kikwete kwamba zanzibar imefika hapo kutokana na kazi na mchango mkubwa wa Rais Kikwete. Wapatanishi wengi waliokomaa duniani hawahitaji kujitangaza lakini vikao vya faragha kati ya viongozi wakuu kitaifa vilifanyika kabla ya kile ulichokuja kukifahamu baadaye. Hebu jiulize kwa nini Rais OBAMA kampongeza sana kikwete kwa hatua hiyo. Hebu jiulize unafikiri Maalim Seif na Karume waliota ndoto ya kukutana Ikulu ya zanzibar bila watu fulani mahali fulani kuwakutanisha kwa siri ili kuinusuru zanzibar? Kumbuka suala la zanzibar lilishindikana katika vikao vya wazi kati ya Seif na Makamba. Usidanganyike kwamba Karume aliamka asubuhi na kumpigia simu maalim Seif kwamba njoo Ikulu ya Zanzibar.
 
Mnaoitwa wafanya kazi amueni la kufanya na rais wenu...maana nyie ndiyo mliokuwa mnaomba kuongezewa mishahara....nyie ndiyo mliokuwa mnasikia hotuba yake kwa hiyo wakisema rais hakusema hivyo mimi ntaripia tv ili watz wasikie tena....
 
Duh! Kwa hiyo wewe na mkeo mmeamua KUMPA JK!
Sio hao tu wengi watampatia kura kikwete huo ndio ukweli wenyewe. Tunaomkubali JK tutawakumbusha ushindi wake. sherehe ya ushindi wa Jk itafanyika kwa siku tatu hapa JF tutaomba wanachadema siku hiyo mjiondoe hewani kwa muda wa siku tatu mkituacha tukijipongeza.
 
Hivi hawa new member wanaotoa statement hizi ndio wanaojiandikisha humu JF kumtetea JK? Anyway safi karibuni but usiseme wafanyakazi sema wewe na akili zako mtampigia JK na sio wafanyakazi. Nakutakia kila la kheri

Hivi hawa members wa zamani hapa Jf ni wa Dr Slaa?
 
Kibaraka wa CCM sema mimi nitampigia kura Kikwete sio tutampigia...Ukweli ni kwamba performance ya Kikwete kwenye uchumi wa TZ ni extremely poor, inflation ambayo ni moja ya kigezo imepanda sana toka aingie madarakani (toka 7%-14%). Dar tu haina maji safi na salama, infact maji tu hakuna!! Purchasing power ya mtz imeshuka sana, watu masikini wameongezeka, wizi na rushwa ndo usiseme ikiwa na maana kuwa serikali yake haina strong institutions ya kuondoa tatizo hilo!!
Wewe mpigie kura ila mie hapana kwa sababu i just do not see a better future with Kikwete as a president.

wewe ni kibaraka wa nani hapa JF?
 
Back
Top Bottom