JK: Ni Marufuku kipengele cha Dini kwenye Sensa

JK: Ni Marufuku kipengele cha Dini kwenye Sensa

Umasikini ni wetu. Hatuhesabiwi mbona mnatulazimisha wakorintho

umaskini ni wa watazani wote isipokuwa watu wachache wanaokula rasilimali zetu.Kujua idadi ya watanzania kutasaidia

kiasi fulani kwa serikali katika mikakati yake ya maendeleo
 
yani serikali gani inayotaka kulet maendeleo???hiii ambayo hata panado hospitali hakuna? wanafunzi wnakaa chini na mengi kedekede?
waislamu nawasihi mkahesabiwe, Allah anampenda mtu anayependa kujaji kwa akili na maarifa aliyo mpa ple anaposem .........falaaa yaa kiluuna.......
 
Mwacheni Baba wa Taifa apumzike kwa amani

muambie huyo mama aliyemtaja kwenye tv, sisi wengine tunasherehesha kilichozungumzwa tu kwenye tv na hao wenye mamlaka ya kuwalazimisha wenzao jambo lolote alimradi akili zao zimekubaliana, ila ukweli mimi binafsi ni mwislamu na sitahesabiwa. SIHESABIWWWWWIIIIIIIIIIII!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! AAAAAAAAARRRRRRRRRRRGGGGGGGGGGGHHHHHHHH!!!!
 
kuna watu wengine vichwa vyao vipo kama nazi iliyoliwa na mwezi vile.ni wawekezaji wangapi Tanzania tunao na sehemu husika ya huo uwekezaji haifaidiki na huo uwekezaji ikiwemo nchi yenyewe?
tunashudia takribani sehemu nyingi ambazo hao wawekezaji hapa Tanzania wapo wanatuachia majanga kama si vilema vya kudumu. sasa haya kama ndio maendeleo big up!
 
Ni upuuzi wa serikali zaid na zaid. Watanzania tumeishi kwa kupendana, aman na upendo kama ndugu siku zote.

Ulafi wa kulazimisha kuendelea kusalia madarakani kwa ccm ndo kumetufikisha hapa tulipo.

1. Urais na hayo madaraka wameyapata, sasa waje watupatanishe baada ya kutujengea kuchukiana na kutugawa kwa misingi ya din zetu.

2. Maisha bora kwa kila mtanzania ni sera iloshindwa na umaskin wakutupwa kwa watanzania umewafanya kuchananyikiwa.

Ponda amekuwa na ushawishi kwa waliowachache waislam, matokeo ya kushindwa kwa ccm na sera zake za kipuuzi- upandikizaji wa siasa za chuki hasa kupitia udin, kikwete yanamtokea puan maana aliona kalibu bila kutathimin matokeo ya kuhubili kwa makusudi udin majukwaan.

Ni vigum sana ponda kuwashiwish watu wenye shughuli za kufanya, uelewa mzuri na hekima kugomea sensa.

Ponda kupata wafuasi ni matokeo ya umaskin wa vitu viwili. Kipato dun na uelewa mdogo miongon mwetu.
Elimu dun itolewayo na sera mbovu za ccm zinampa kiburi na ahuen ponda kupata wafuasi.
 
Hadanganyiki mtu! Mlizoea kuwahadaa Waislam, sasa wameerevuka!
Tanzania sio nchi inayofuata misingi ya kidini,sensa ni kwa maendeleo ya watanzania wote wala sio kujua et tz kuna wapagani wangap?wakristo wangap?wala waislamu wangap?.Tuache polojo kwenye mambo ya msingi,TUSIMAME PAMOJA KUJENGA TAIFA LETU TOKA MIKONONI MWA MAFISADI
 
Tatizo lao Wameshajiwekea Akili za Kutoelimishwa..

1. Wasipohesabiwa hakuna Msaada wowote watapata hata kama kuna Njaa na Ukame maana Serikali haiwajui.. Hata kama watatumiwa Mahindi hayatatosha

2. Miradi ya Maji na kupeleka Dawa kwao hakuta kuwa na Misaada hiyo

3. Hakuna Shule ya Serikali itajengwa maana Hawana idadi ya Watoto Wanaosoma

4. Hakuna huduma za Bure zitatolewa kwa Wazee maana hawatapata idadi yao

5. Hakuna Kituo cha Watoto yatima ama Walemavu kitafunguliwa iwe kwa Serikali au Binafsi maana hawatajua idadi yao

6. Hakuna Uwekezaji wowote utafanywa maana Wawekezaji wanaangalia na Eneo husika kwa Kuangalia sensa ya Eneo hiyo kwanza

7. Hakuna Pembejeo za Kilimo zitapelekwa maana hawajui wakulima ni Wangapi


FUTENI UJINGA KWANZA. Maana sijasikia Sheikh akiwaambia haya. Ila Anawaambia tu Mgome.

YOU CAN TAKE IT or NOT
Na vile vijiji ambavyo havina Mahospitali, Shule, pembejeo za kilimo, sehemu za kulea wazee na yatima kabla ya uhuru mpaka leo viligomea sensa ya mwaka gani mpaka yakawakuta hayo?
 
..nifanyapo mambo mengi ya kijamii huwa najaza fomu nyingi sana zenye kipengele cha DINI. k.v. fomu za kujiunga na asasi mbalimbali, fomu za mikopo, fomu za kuomba passport n.k. Hivi sasa kuna kundi la watu linadai kipengele hiki kiwekwe katika dodoso la sensa. kwangu, sikuona lolote baya ktk hilo hadi pale WENYE AKILI ZA PLUTO a.k.a. waona mbali walipoanza kubisha kwa kani za ziada kuwa kikiwekwa kitahatarisha amani.

kimsingi, jibu likisadifu swali matata huondoka. na kinyumeche ni sahihi; kwamba, jibu lisiposadifu swali/hoja matata huongezeka. Majibu ya kishabiki kuhusu hoja/ombi hilo ndiyo yaliongeza zaidi matata katika akili yangu huru. Mafyongofyongo yanisongayo ni haya:

1. Kujibu kuwa kipengele hiki kilikuwepo na 'kiliondolewa kwa hekima ya Mzazi wa Taifa'; kwamba, aliona mbali... Jibu hili kwa hakika, halitoshi. Dunia ni WATU, SIRI na MATUKIO! Matukio hutukia kwa kuzingatia MIKTADHA. Yeye alifanya hivyo kwa kusukumwa kwa miktadha ya wakati huo. Mbona kuna mengi yamefanywa ilhali Mzazi wa Taifa hakuyafanya? Rejea wizi wa mali za umma, ujenzi wa daraja la Mkapa na mengineyo meeengi! Ni kumkosea adabu Mzazi wa Taifa iwapo tutakuwa tunamtumia kuhalalisha SIRI zetu. WAJIBUNI VEMA, WAELIMISHENI VEMA, WAONDOLEENI UKAKASI WALIONAO JUU YA HOJA YAO YA KIPENGELE CHA DINI KUWAMO SENSANI. Kunyamazisha jambo kwa kitisho na kebehi ni sawa na KUFICHA KAA LA MOTO CHINI YA MAJANI MAKAVU!

2. Nasikia kutakuwa na kipengele cha kujua/kuchambua uwapo na idadi za nyumba za ibada (nakiri kuwa sina hakika, nasikia tu). Lakini watumiaji wa nyumba hizo za ibada ni DHAMBI NA HARAMU kujulikana! KAMA KWELI HILI LITAKUWA HIVI, basi waandazi wa madodoso wana mengi ya kufafanua hapa kuliko kujibu kishabiki. Huu ni zaidi ya UJUHA!

3. Kumekuwapo na takwimu nyingi zihusuzo idadi ya watu kwa dini zao. Nyingine hutolewa na ogani za serikali yenyewe na nyingne hutolewa na asas binafsi (zikiwemo za kidini). Rejea nyaraka za sekta ya utalii, waraka wa ofisi ya waziri mkuu, n.k. Sasa kuna tatizo gani kurasimisha?... Ukila na kipofu, c vema kumshika wala kumgusa mkono! Ukifanya hivyo, hautatofautiana na KICHAA... kwa hili, naamini vichaa wapo wengi. Bado wauguzi wa Mirembe wana kazi nzito!

4. Sensa yakadiriwa kutumia TAKRIBANI sh. 140 bn. Kwa wasiojua thamani ya pesa hizo, ni kwamba, zaweza kujenga viwanja takriban vitatu mithili ya ule wa taifa uliopo temeke. Hizo ni pesa nyingi sana. Naamini serikali ilipaswa kuwa makini zaidi katika jambo hili la sensa kuliko umakini uoneshwao na watendaji wake katika kukabiliana na hoja na changamoto zake. Rejea majawabu ya Ndugu Wassira katika hotuba ya majumuisho ya kikao cha viongozi wa dini mbalimbali kule Dodoma, majawabu ya Daktari Albina Chuwa juzi kati kituo cha runinga cha TBC1 na hoja nyinginezo. Nakiri kuwa kumekuwapo hoja nyingi dhaifu na za kudeka kutoka kwa watu na taasisi mbalimbali dhidi ya sensa. Hata hivyo, hili la kipengele cha dini kuwamo dodosoni nadhani halijapewa majawabu mujarabu. Mchwa akikaribia kuangamizwa, huoteshwa mbawa! (Shaaban Robert, KUSADIKIKA). Je, sensa imekuja kuotesha mbawa baadhi ya watanzania?

5. Kwa dhati na yakini, sijui kabisa madhara ya kuhusishwa kwa kipengele cha dini sensani. TAFADHALI NAOMBA MNIJUZE MADHARA YATAKAYOTOKEA. Ukiona njia hii ya kielektroniki yakukwaza, nijuze kwa ujumbe wa ndani (inbox), barua pepe: atponeraman@gmail.com AU 0784 959784.

ni mimi Mtanzania mwenzenu niliye gizani.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mbona kwenye kupiga kura serikali hawasema lazima kupiga kura...kama watu hataki kuhesabiwa muache.
 
Mkuu Ritz ni aje? Kwenye hili nilidhani utakuwa unapigia debe chama lako

Mbona kwenye kupiga kura serikali hawasema lazima kupiga kura...kama watu hataki kuhesabiwa muache.
 
Last edited by a moderator:
Mbona kwenye kupiga kura serikali hawasema lazima kupiga kura...kama watu hataki kuhesabiwa muache.

Ukiacha kupiga kura unakuwa umeacha kutumia haki yako. Ukikataa kuhesabiwa sensa ni mpinga maendeleo na kudumaza nchi. Sote tufunguke na tutoe ushirikiano mzuri katika sensa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu na Wananchi wake.
 
Kwani nchi hii ina waislamu na wakristo tu?

Ponda anataka ijulikane wakristo ni wangapi na waislamu ni wangapi. Mbona hasemi na banyan na kocni ni wangapi?

Mnapotaka kujua idadi yenu, tayari juzi mmetutamkia kuwa Mufti na Shekhe mkuu pamoja na wale makadhi aliowachagua ni MAKAFIR (sio waislamu). Ni imani yangu kuwa wana wafuasi na si wachache ni wengi. Sasa swali langu mimi ni hili; Ikiwa leo mtahesabu waislamu, Mufti and Company wahesabiwe kama waislamu au makafir?

Akili nzuri ukiwa nayo
 
Dawa yao hawa ni ndogo. Andaeni pilau siku ya sensa, watajitokeza kuhesabiwa woooooteeeee.

Mkuu una akili kama mchwa. Yaani hii kitu hii

View attachment 62805
Kwa hii hamna atakayegoma kuhesabiwa, hata kama ingekuwa unacharazwa bakora 2 kabla ya kuhesabiwa. CCM wanajua hii mbinu na imefanikiwa sana ktk mikoa ya pwani na Tabora.

Nakuaminia mkuu wa kaya, kweli unawajua wanao
 
Aisee babaangu mi nadhani waanze kuhesabiwa mafisadi kwanza ndio 2fate sisi maskini
mi siku ya sensa nitabeba familia yangu kwenda porini kulima na kijificha nawaunga mkono wote watakaogoma
 
Back
Top Bottom