Endeleaaa
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 1,485
- 738
Juzi jumatatu 15th march 2010. Rais JK aliwaapisha katibu Mtendaji na manaibu wake wanne wa tume ya Mipango. Japo hii habari haikupata media coverage kubwa lakini hiki kitengo kinaonekana ni nyeti kwa taifa hili kuliko tume yoyote iliyowahi kuundwa na Rais. Chombo hiki ndio kitakuwa mshauri mkuu wa Rais katika mustakabali wa kiuchumi wa Taifa letu. Sijaelewa kwanini media zote za nyumbani na hata wakulu wa humu JF hatujaifuatilia hii habari kwa undani lakini binafsi nadhani kuna haja watanzania tuwajue hao brain ya Rais ni akina nani na kama kweli ni uteuzi muafaka katika kitengo hicho.
Mwenye CV zao akituwekea humu itakuwa jambo zuri sana.
Mwenye CV zao akituwekea humu itakuwa jambo zuri sana.