JK na Tume ya Mipango

Endeleaaa

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
1,485
738
Juzi jumatatu 15th march 2010. Rais JK aliwaapisha katibu Mtendaji na manaibu wake wanne wa tume ya Mipango. Japo hii habari haikupata media coverage kubwa lakini hiki kitengo kinaonekana ni nyeti kwa taifa hili kuliko tume yoyote iliyowahi kuundwa na Rais. Chombo hiki ndio kitakuwa mshauri mkuu wa Rais katika mustakabali wa kiuchumi wa Taifa letu. Sijaelewa kwanini media zote za nyumbani na hata wakulu wa humu JF hatujaifuatilia hii habari kwa undani lakini binafsi nadhani kuna haja watanzania tuwajue hao brain ya Rais ni akina nani na kama kweli ni uteuzi muafaka katika kitengo hicho.

Mwenye CV zao akituwekea humu itakuwa jambo zuri sana.
 
Hii ni Tanzania bana.

Mambo ya rusha roho ndio yana umuhimu kwetu. Angalia tulivyoona kwamba sheria ya matumizi ya uchaguzi ati ni kitu kidogo.
 
Namfahamu Philip Mpango vizuri. Naamini atafanya kazi nzuri. Ni mtu makini na ni mtendaji mzuri.
 
Can't we talk about the institution kwa nini kila siku mtu mtu tu!!!

Ni kweli but sometime its hard kutofautisha kati ya Rais wa Tz na Kikwete.

Kwani hii tume si imekuwepo siku nyingi tu. Mi nadhani wanabadilisha badilisha majina leo inaitwa wizara akija president mwinine anaita tume.

Binafsi nadhani imefika wakati tuwe na set up ya wizara na idara ya kudumu. sio kila anayeingia anacheza na kubadilisha anavyojisikia. huyu anaongeza huyu anapunguza.

Tatizo kama la mgao wa umeme linaonesha kuwa hatuna mipango mizuri. hatufanyi detailed analysis ya priorities.

Binafsi sioni kama hi Tume ina jipya.
 
Ndugu, Hatukuwa na Tume ya Mipango. Tulikuwa na wizara ya mipango. si kweli kwamba Tume ya Mipango ilikuwepo before.
 
Can't we talk about the institution kwa nini kila siku mtu mtu tu!!!

Mkuu institution haijiongozi yenyewe; inaongozwa na watu, na ni vema kuwa na watu ambao ni qualified kuifanya hiyo kazi vizuri. Ni imani yangu kwamba wazo la kuangalia CV zao ni zuri ..... ninaamini hata JK aliangalia CV zao kabla ya kuwateua.
 
Ndugu, Hatukuwa na Tume ya Mipango. Tulikuwa na wizara ya mipango. si kweli kwamba Tume ya Mipango ilikuwepo before.

nachosema wanachofanya ni kucheza cheza na majina tu. Na nina uhakika 99.9% kabisa miaka ya nyuma kabisa Neno tume ya mipango liliwai kuwepo.

Au niambie majukumu ya tume ya mipango yatatofautiana vipi na iliyokuwa na wizara ya mipango? Sioni kama kuna tatizo la kuwepo au kutokuwepo kwa Tume ya mipango.

Hii tume ina fill loophole gani wizara ya mipango ilyoshindwa ?

Hata kabla ya kuundwwa hii tume kila wizara zina wakurugenzi wa mipango sera. There is nothing new here
 
Mkuu institution haijiongozi yenyewe; inaongozwa na watu, na ni vema kuwa na watu ambao ni qualified kuifanya hiyo kazi vizuri. Ni imani yangu kwamba wazo la kuangalia CV zao ni zuri ..... ninaamini hata JK aliangalia CV zao kabla ya kuwateua.

Binafsi tatizo mablo naliona ni Huu mfumo unakuta top decision post zote ni nafaszi za kuteuliwa. tena kuteuliwa bila kuomba kazi. This is wrong. Look kwenye wizara waziri( Anateuliwa) katibu Mkuu ( Anateuliwa) Wakurugenzi wa idara( wanateuliwa) atleast katibu au wakurugenzi wangekuwa wanaomba kazi.

katika mazingira hayo hata kama mtu ana CV nzuri kiasi gani hakuna efficiency ya utendaji.

kazi unayozawadiwa tu. na kazi unayozawadiwa baada ya kuomba na kufanyiwa usaili zina tofauti.
 
Dr Mpango alikuwa chuo Kikuu Dar anafundisha Economics and research bureau ya chuo kikuu Dar hivyo ni mtu safi kabisa
 
Kwa tume hii naona kama Rais amekuwa makini zaidi maana hao wadau hawakuteuliwa tu, kumekuwa na usaili na watu wamekuwa shortlisted na hizo nafasi nahisi wamepewa kulingana na professional zao.

Check hiyo attachment. Pia ipo kwenye website ya utumishi [http://www.utumishi.go.tz/govtdirectory/200911021725220.call 4 inter.pdf]
 
Attachments

  • president office.pdf
    69.4 KB · Views: 204
Dr Mpango alikuwa chuo Kikuu Dar anafundisha Economics and research bureau ya chuo kikuu Dar hivyo ni mtu safi kabisa

Kuwa chuo kikuu na kufundisha economics hakumfanyi mtu kuwa safi!! Those could be necessary but not sufficient conditions for such an appointment. Costa Mahalu aliyekuwa balozi wetu Italy alikuwa Dean wa Faculty of law pale UDSM na hivi sasa yuko kizimbani akishukiwa kwa ubadhilifu!!
 
Unajua nchi hii ina institution nyingi nyeti, ila wale walioshikilia hizo institution, duuh.Kwahiyo ni muhimu kujua nani anakwenda wapi ili kuona kama kuna la maana la kutegemea au ndio sound kwa kwenda mbele
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom