JK, Mukama watua Dodoma, utata mtupu mawaziri 8

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Japo nimeiweka kama tetesi lakini muda wowote atakuwa kaingia Dodoma na tutarajie lolote. Safari hii hakuna cha "Wazee wa Dar".

Nitakuja na updates baadae kidogo

Updates:
JK amewasili Dodoma lakini ngoma bado nzito. Katibu wa CCM, Wilson Mukama naye amefika Dodoma. Hakuna kujiuzulu, ngoma bila bila. Taratibu za CCM, hakuna atakeyejiuzulu, Kamati ya wabunge CCM ilichemka kuwalazimisha mawaziri wanane kujiuzulu, wamekuza sana na kupoteza seriousnes, ikaonekana kila mtu aliamua kutumia nafasi hiyo kwa maslahi ya kisiasa na baadhi wanaonekana kama wanatafuta nafasi za uwaziri.

Kwa ufupi JK ameona pia kwamba huo ni mtego kwake na kwamba wanakoelekea wanataka 'kichwa' chake na si Pinda wala mawaziri, huo ni mwanzo tu. Kwa sasa mawaziri wachache sana kati ya wanane waliandika barua za kujiuzulu, wengi waliandika maelezo ya kujitetea na kutaka Rais awaondoe ikiwa atabaini walikosea katika uwajibikaji wao. Wametoa nafasi ya kuchunguzwa.

JK anaondoka kesho kueelekea Dar na baadae Malawi kwenye mazishi.
More updates baadae.
 
Guys huyu jamaa amalise mnuda wake haondoke maaana imekuwa too much.we kaa tayari tujuze
 
Nashangaa watu wanamsifia nini huyu mtu. Yeye ndiye kawachagua hao watu, yeye ndiye serikali yake imeonyesha udhaifu wa ajabu. Cha ajabu mambo yanapokuwa mabaya, anajifanya yeye kama outsider! JK is not going to be the solution to our problems, because he "himself" is part and parcel of the major problem.
 
Mkuu, hata ungekuwa wewe ndio JK ungesifiwa hivyohivyo. Aliyeishika ngoma kubwa ndiye mwenye sifa zaidi ngomani. Kule kwetu ukwereni ndivyo tunavyoamini.
 
Japo nimeiweka kama tetesi lakini muda wowote atakuwa kaingia Dodoma na tutarajie lolote. Safari hii hakuna cha "Wazee wa Dar".

Nitakuja na updates baadae kidogo

Anaenda Dom kufanya nini? Alikuwa wapi miaka yote kuushughulikia utendaji mbovu wa Baraza lake la Mawaziri? Kazi imemshinda maana ameshindwa kwa miaka chungu nzima kuwawajibisha Mawaziri wake hadi Wabunge wa Magamba walipoona umuhimu wa kufanya hivyo....Arudi Ikulu tu kufunga virago vyake kisha kulitangazia Taifa kwamba kazi ya kuongoza nchi imemshinda hivyo anaachia ngazi ili kupisha Serikali ya muda.
 
Munaharibu kwa kuacha mada. Tutarajie nini? Je, atabadili baraza ama atalivunja? Kuvunja ni hatari kwake maana PM atakayemchagua atahitaji kura za wabunge, na upepo si mzuri ndani ya Bunge, akikosa ni hatari.
 
Matokeo ya Failures zote sasa hivi ni yeye KIKWETE,Alafu nashangaaa kwa nini asingepigiwa yeye kura ya kutokuwa na Imani.Ila kwa kufunika matatizo anaweza.Hili nalo litapita
 
am not expecting anything labda siasa tu, he tends to pour cold anywhere he goes!!!
 
Anaenda Dom kufanya nini? Alikuwa wapi miaka yote kuushughulikia utendaji mbovu wa Baraza lake la Mawaziri? Kazi imemshinda maana ameshindwa kwa miaka chungu nzima kuwawajibisha Mawaziri wake hadi Wabunge wa Magamba walipoona umuhimu wa kufanya hivyo....Arudi Ikulu tu kufunga virago vyake kisha kulitangazia Taifa kwamba kazi ya kuongoza nchi imemshinda hivyo anaachia ngazi ili kupisha Serikali ya muda.

Mkuu BAK,

Nnji hii tatizo ni KIKWETE.Jiulize tu amebadili baraza la mawaziri mara ngapi? Ina maana mara zote hizo anawapata watu Ma bogus?
 
Back
Top Bottom