JK maji ya shingo, awaasa wagombea wa ccm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK maji ya shingo, awaasa wagombea wa ccm

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kiwi, Sep 4, 2010.

 1. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  [​IMG] Aonya wakibweteka wapinzani watashinda
  [​IMG] Awataka wajibu kero za wananchi
  [​IMG] Awaagiza Ilani wamwachie yeye  [​IMG]

  Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, ameonya kuwa kama wagombea ubunge na udiwani kupitia chama chake watabweteka, kuna uwezekano kwa wapinzani kuibuka na ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.


  Alitoa angalizo hilo jana alipokuwa akizungumza na viongozi wa chama hicho ngazi ya mashina, matawi, kata zilizopo katika jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam.


  Alisema wagombea ubunge na udiwani kupitia CCM, wanapaswa kutambua kuwa uchaguzi ni kama vita, ambayo chama na wagombea wanawajibika kutumia nafasi zilizopo kwa umakini ili kupata ushindi.


  Rais Kikwete alisema viongozi na wagombea ubunge na udiwani wa chama hicho wanapaswa kuzungumzia kero za wananchi badala ya kusoma Ilani ya Uchaguzi katika kampeni zao.


  Alisema ilani hiyo itakayotekelezwa kati ya 2010 na 2015, inazungumzia zaidi mambo ya kitaifa yasiyogusa moja kwa moja mahitaji ya watu katika baadhi ya maeneo hapa nchini.
  Alisema wagombea ubunge na udiwani wa CCM, wana wajibu wa kuwafahamisha wananchi jinsi serikali ilivyotatua na jinsi inavyoendelea kushughulikia kero za kijamii.
  “Viongozi wenzangu, shida za wananchi tunazijua kwa kuwa tuko madarakani katika serikali ya awamu ya nne tuliposhinda mwaka 2005, tulikuta matatizo na tukaahidi kuyashughulikia. Tumeshughulikia mengi, yapo ambayo tunaendelea kuyashughulikia na mengine bado, ni wajibu wetu kuwafahamisha wananchi ili watuelewe,” alisema.


  Alisema viongozi na wagombea wanapaswa kurejea katika mashina, matawi, kata, majimbo na ngazi nyingine za kichama, ili kuangalia matatizo husika na kutoa taarifa sahihi kwa wananchi.


  Rais Kikwete alisema kila eneo katika nchi lina matatizo yake, ambayo si lazima yafanane na eneo jingine na kwamba kushinda au kushindwa kwa wagombea wa CCM, kutatokana na namna walivyoshughulikia kero zilizopo. “Usitegemee ujenzi wa daraja la Mkapa kule Rufiji, likampa ushindi mtu aliye Bukoba, si rahisi na huwezi kuzungumzia changamoto zinazolikabili jiji la Dar es Salaam katika upande wa msongamano wa magari wakati unagombea Bukoba... ni vitu ambavyo haviendani,” alisema.


  Rais Kikwete alisema wagombea ubunge na udiwani wa CCM watasaidiwa na jinsi walivyoshughulikia matatizo ya jamii na kusoma ilani ya chama hicho katika kampeni zao.
  Aliwataka wagombea wanapokuwa kwa wananchi, wawaeleze ni kwa nini wanapaswa kuichagua CCM na kwa nini wawachague wao (wagombea wa CCM). “Na sio kuchagua tu, bali muwaeleze wananchi kwa nini wanapaswa kuichagua CCM kwa kura nyingi, kwani hilo nalo ni la msingi kwa uimara wa chama,” alisema.


  Alisema CCM inahitaji kura nyingi zitakazokiwezesha kupata nafasi 100 za wabunge wa viti maalum. “Wabunge hao wanatokana na jinsi chama kilivyopata kura nyingi, hivyo wafahamisheni wananchi wawaelewe kuhusu jambo hili,” alisema.


  Pia, Rais Kikwete aliwataka wagombea walioshinda kura za maoni kuwafuata makada walioshindwa ili kupanga mbinu za ushindi kwa pamoja. Alisema suala la kuondoa tofauti kati ya walioshinda na walioshindwa, linawagusa wagombea ubunge na udiwani na si viongozi pekee. “Najua binadamu tunatofautiana kupona majereha, wapo ambao inawachukua muda mfupi na wengine inawachukua muda mrefu, lakini mwisho wa siku sisi wote ni wana CCM,” alisema.


  Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha na viongozi mbalimbali wa chama na serikali.


  Wakati huo huo, Rais Kikwete amesema hakuna mkazi wa Kigamboni atakayepoteza haki zake katika mradi wa ujenzi wa mji wa kisasa katika eneo hilo. Alisema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa kuzindua kampeni za ubunge na udiwani katika jimbo la Kigamboni jana.


  Alisema watendaji wanaohusika katika mradi huo, wanatakiwa kuhakikisha kuwa kila mtu analipwa kwa mujibu wa thamani ya nyumba anayomiliki na bila kuzungushwa. Rais Kikwete, alisema viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, wanapaswa kutoa maelezo sahihi kwa wananchi kuhusu ujenzi huo, ili waondokane na dhana kwamba lengo ni kulimikilisha eneo hilo kwa wawekezaji.


  Alisema kauli nyingi za uzushi zilishatolewa kuhusu mradi huo, ikiwemo ya kumhusisha (Kikwete), kwamba alitarajia kuiuza ardhi ya Kigamboni kwa Rais mstaafu wa Marekani, George Bush. “Niliyasikia maneno hayo, lakini nikayapuuzia kwa sababu nilijua yalikuwa ni uzushi mtupu,” alisema. Rais Kikwete alisema anaunga mkono wazo la ujenzi huo kwa vile litapunguza msongamano wa wakazi wa Kigamboni kwenda maeneo ya katikati ya jiji kwa ajili ya kutafuta mahitaji yao.


  Pia, Rais Kikwete alisema mipango inafanyika kuifanya hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuwa na hadhi ya kimataifa, ili itoe huduma wagonjwa wanatoka nje ya nchi. Alisema Taifa limemudu kutibu magonjwa kama moyo, na kwamba jitihada sasa zinaelekezwa katika kufanikisha tiba ya ubongo na mishipa ya fahamu.


  Rais Kikwete alisema ujenzi wa daraja la Kigamboni utafanyika hivi karibuni na kwamba hivi sasa jumla ya wakandarasi sita wamejitokeza kuomba zabuni. Alisema mkandarasi atakayeshinda atashirikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya ujenzi.


  Kuhusu tatizo la maji jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema serikali itahakikisha linashughulikiwa na kuwa historia katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
  CHANZO: NIPASHE

  Naona JK anatapatapa hajui ashike lipi aache lipi. Kweli maji yamefika shingoni.
   
 2. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ahaaaa ulikuwa wapi au huo si ndi UFISADI SISI WAKAZI WA KIGAMBONI TUMEONA YALIYOTOKEA KIBAMBA
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kachelewa sanaaaa.yeye alidhani watu wanachagua sura
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Si uongo, kwa mara ya kwanza wanaavoid kusema ushindi wa kishindo, tsunami etc wameona hali si njema sana. Chadema tunaomba pressure iongezeke jamani wapelekwe kwenye kona mpaka refa atupe taulo.

  MHH ila ile lingine uchaguzi si vita hata kidogo, uchaguzi ni tendo la wananchi kwa ridhaa yao bila ushawishi wa fwedha, chakula, dansi nguo wanachagua kiongozi wanayedhani atawaletea maendeleo kwa kipindi kingine. Kama raisi unaequate uchaguzi na vita ni kwenda a little bit too far. Ukichukua hii na kauli za nyuma kuwa ushindi ni lazima inatuletea wasiwasi wapenda amani.

  Naomba hilo kama alisema kweli alirekebishe.

  By the way sheria zetu za uchaguzi zinasemaje kuhusu hate speech??????
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Yes JK, ni muhimu kuwakumbusha wananchama, vita vya kupambana na wahuni sio mchezo
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hakuna wahuni ila ni vyama vya siasa vinavyotambuliwa na serikali na vina wanachama lukuki Tanzania nzima na kumbuka kuwa uchaguzi haujawahi na hautakuwa vita, uchaguzi ni njia ya kistaarabu ya kuwaondoa mliowachoka na kuwaingiza madarakani wale wanaoweza kutekeleza matakwa ya wananchi. Inakuwa vita paletu wale wanaotakiwa kuondoka wanakataa hapo inakuwa ni kinyume na matakwa ya wananchi, na wananchi wanaweza kuamua utashi wao uprevail.
   
 7. B

  Bull JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ndio uongozi wenye dira
   
 8. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #8
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  hizi ni rasharasha mwaka huu watavua bukta jezi
   
 9. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Maji ya shingo ndiyo kitu gani?
   
 10. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  JK ni jemedari mzuri na anajua jinsi ya kupiganisha vita, sasa amekaa na wakuu wa kamandi mbali mbali na kuwachora mchoro wa nn kifanyike ktk kushinda vita hii.

  hiki ndio chama makini kisichoumauma maneno ktk medani ya mapambano. kilicho mbele ni ushindi wa kishindo
   
 11. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ...They are no where in Baghdad...changanya na zako
   
 12. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  ===========

  Hapa inabidi tuchanganye na zetu. JK amenukuliwa mara nyingi akiufananisha uchaguzi na vita:
  -Dodoma siku anarudisha fomu alidai yeye alikuwa anafundisha jeshini
  -Kagera, Mwanza na Kigoma aliwatisha wananchi kwa kutumia mifano ya vita ya Rwanda na Burundi
  -DSM tena kikao cha ndani, ametamka uchaguzi ni vita.

  This is a hate speech per exellence in form and shape. Wapinzani tumia hii kama PO yenu.
   
 13. e

  emalau JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Na hii sijui tuipeleke kwa tendwa au kwa makame?
   
Loading...