Tumkosoe rais inapobidi, lakini tupunguze ushabiki usio na msingi kama huu wa kuona kwamba kila safari anayofanya eti anenda "kula nchi". Jamani, tuangalie pande zote.
hivi baadhi ya hivi vimikutano vya nje, Dr. Shein hawezi kuwakilisha?
Kithuku,
wewe ukiwa na akiba ya sh alfu hamsini benki, una watoto wawili ambao wanasoma sekondari kwa karo ya alfu ishirini kwa mwaka, na mama yako mzazi ni mgonjwa na anahitaji tiba kwa sh alfu kumi na tano.
Wakati unafikiria cha kufanya, mjomba wako tajiri anakupa mwaliko wa kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya binti yake. ifahamike kuwa huyu mjomba wako aliwahi kukunyang'anya mali zako zote miaka ya nyuma ila siku za karibuni amekuwa anakupatia mkopo wa sh mia tano kila mwezi...Gharama ya kwenda kwa mjomba wako ni karibu sh elfu arobaini.
je, ingawa kwenda kuiitika mwaliko wa mjomba wako ni sehemu ya majukumu yako, wewe utakwenda kwa mjomba wako au utatumia akiba yako kupeleka watoto wako shule na kujaribu kumtibia mama yako?
Mwafrika wa kike,
Salamu dada. Mfano wako unavutia sana. Nadhani unazungumza suala la vipaumbele hapa. Vema sana. Lakini katika muktadha wa safari hii anayofanya JK, sivyo. Wachangiaji wanadai ati kwa nini hakutuma mwakilishi? Sasa akituma huyo mwakilishi atasafiri bure? Kwa hiyo kama "mjomba" unayemzungumzia kanialika, na hela niliyo nayo ni kidogo, basi nisiende lakini nimtume mke wangu, mdogo wangu, wanangu n.k akaniwakilishe, kwani sasa huyu hatatumia gharama? Mantiki iko wapi hapa?
Na pili, kuna ushahidi kwamba anachoendea JK huko Ufaransa ni jambo dogo tu linaloweza kufananishwa na mfano uliotoa wa "sherehe ya kuzaliwa binti ya mjomba tajiri"? Je haendi kwa maslahi ya taifa? Je si wajibu wake kama rais kufanya safari hiyo? Ndizo hoja ninazohitaji kuona zikizungumziwa hapa.

when he was young he couldnt do good, now he cant do bad..... why are we mad ! ndio maana ya taito ya Muungwana, haiji kimchezomchezo, kama mliadhani kumuita Muungwana was just a name, there you go now !
Mwk,Kithuku,