JK kuwaleta usher na trey songz Tanganyika

JK kuwaleta usher na trey songz Tanganyika

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
55,030
Reaction score
59,684
Rais Jakaya Kikwete amesema atawaleta nchini wasanii nyota wa muziki kutoka Marekani kwa ajili ya kuja kutoa burudani na kuzungumza na wasanii wa muziki na filamu nchini Julai mwaka huu.

Kikwete maarufu kama JK, aliyasema hayo wakati akihutubia wasanii, viongozi wa Serikali na vyama vya siasa pamoja na maelfu ya wananchi waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa usiku wa kuamkia jana.

Alisema ziara yake iliyopita nchini Marekani, ambayo alikutana na msanii aliyezoa tuzo saba za Kilimanjaro Music mwaka huu, Nassib Abdul 'Diamond Platnumz', ilikuwa na mafanikio makubwa.
More ...
http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=68979
 
Na chenyewe ni kipaumbele cha serikali yetu tukufu!! walete tuoshe macho
 
Ndiye Rais tuliye naye, hatuna namna , kusema ukweli mambo kama hayo kwa kiongozi kama rais hapaswi kuyahangaikia, akahangaikie matokeo mabaya shuleni, huduma za msingi za watanzania na mengineyo
 
zitakua zetu hapo............


Yaleyale!!! Watoto wanakaa sakafuni mashuleni, wagonjwa wanalala wawiliwawili kwa kitanda kimoja, miji na vijiji havina maji salama, kisa serikali haina fedha.

Wabunge wanalipwa Tshs 300,000 kwa siku sawa na mshahara wa Mwl kwa mwezi, gym ya wabunge kwa Tshs 2.8 billion,

Fedha ya kuleta wasanii toka nje just for kuserebuka inatoka wapi na ni raia wangapi wa kipato kidogo wananufaika na burudani huku huduma za jamii zikiwa duni?
 
Msanii lazima afanye kazi na wasanii wenzie,bravo mzee wangu kwa kuishi maisha yako halisi.
Nielewe nikuelewe.....!
 
Back
Top Bottom