JK: Kupanda mlima kilimanjaro ili utokomeze maonevu ya watoto na wanawake ipo sawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Kupanda mlima kilimanjaro ili utokomeze maonevu ya watoto na wanawake ipo sawa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAGEUZI KWELI, Mar 5, 2012.

 1. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Jamani nimejiuliza kidogo, Rais wetu mpendwa sana Mtukufu JK amezindua kampeni za kupanda mlima kilimanjaro kuhimiza utokomezaji wa adhabu za watoto na wamama,
  Nimekubaliana na kampeni za kupambana na tohara za watoto na wakinana kupata mikong'oto.Swali ambali sijapata jibu,
  Swali, Hivi umati huu wooote ulioenda kupanda mlima kilimanjaro, ujumbe wake unamfikia je ngariba aliyepo kijijini ambaye hata kiswahili hakijui?Au je mmng'ati wa Balangda atajua je kampeni zilizozinduliwa na JK huko marangu wakati Radio haijui na tv haijui?
  Hivi kama serikali ingekuwa imeazimia kupambana na janga hili, hao waliokuja woooote si wangeenda kwenye vijiji ambavyo majanga haya hutokea ili kuongea na wananchi??
  Sasa mimi sijaelewa jamii inayolengwa itapata je ujumbe kwa kadamnasi iliyokuja toka nchi 35 na sijui kama si wamekuja kutalii kusingizia mapambano ya tohara na ubakaji na mengine kama hayo.
  Ni upeo wangu jamani ila kama kuna anayeweza nieleza kwa undani nikaelewa vema, basi na iwe hivyo.
  Sintashangaa siku moja wakaja wengine kupanda mlima kupambana na ngono zembe na kuhimiza ngono salama na Condom. it can be possible
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ukitaka kutokomeza uonovu kwa watoto, wamama, wababa, vijana, paka, kuku, vikapu etc unatunga sheria na kuisamia hiyo sheria kwa nguvu zote. Kupanda mlima ni utalii. period. Wakati umefika kwa viongozi wetu including rais kuacha kutuchezea akili na hoja za kikoloni. Tumesumbuliwa sana na kelele na 'malaria no more' na sasa wanahamia kwenye kupanda mlima, what next? Kama mtu anataka kupanda mlima Kilimanjaro na afanye hivyo lakini kwa hakika hakuna litakalo badilika kuhusu uonovu/ukatili ndani ya jamii.
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wacha ujinga wewe mleta mada. Unawafanya Musoma hawajui Kiswahili. Nyerere alitokea maeneo hayo hayo na alipokuja Dar kaja kiswahili anakijuwa. Ni nani alimfundisha? Wewe? Wacha dharau. Na hao wamasai wacha radio, wana madishi ya satalaiti ambayo hata wewe huna. Wacha kutukana watu kirejareja.
   
 4. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,164
  Likes Received: 1,167
  Trophy Points: 280
  Tanzania bila ukimwi......
   
 5. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Kama vyote vingekuwa vimeenea kwa jamii hiyo unayoisemea, them Tanzania ni nchi imeendelea sana basi, Every where people they knows what is happening around,Punguza jazba, Mangariba Musoma huko wanafanya Sherehe na kila mtu anajua, Wamasai nalo usikatae wamama wanakatwa (Emouo)Kupunguza makali ya msisimko, Unadhani nimeandika kitu nisichikijua? By the way, nalo uliloandika ni comment pia na ni accepted.
   
 6. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  2nae rais mtalii
   
 7. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  imekaa vyema hasa kwa wanaotangaza hapa JF kuwa ni mgonjwa
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Atakuwa ndiye Rais wa kwanza wa Tanzania akiwa madarakani kupanda mlima kilimanjaro inapendeza kama njia ya kukuza na kutangaza utalii wa mlima kilimanjaro. Picha za Rais zikitumika kama nembo ya kuutangaza mlima huo itakuwa mojawapo ya njia ya kuvuatia utalii
   
 9. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Nyerere alipopandisha koroboi juu ya mlima k'njaro limulike nchi nzima haikuwa na shida,kweli nimeamini kunya anye kuku akinya bata 'anendesha'.
   
 10. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Sioni tatizo kutumia Mlima Kilimanjaro au popote kama ishara ya uzinduzi. Kwa upande mwengine wamechagua pahali muafaka kama palivyochaguliwa "kuangaza nuru ya uhuru na ukombozi wa Afrika nzima", pamoja na kutangaza utalii. Hilo halinipi wasiwasi, wasiwasi wangu ni uendelezaji wa hizo kampeni na harakati; wasiwasi wa kuwa zimeanza hapo na zitaishia hapo hapo, kama ambavyo tumezowea kufanya Tanzani. Unakumbuka "Fagio la Chuma" lililokuwa alama ya kupambana na rushwa? Rushwa imezidi na hakuna kinachoendelea.

  Tunachotakiwa kufanya, pamoja na nia zuri ya uzinduzi huu, ni pamoja na uelimishaj jamii na ufuatiliaji wa dhamira yenyewe, pamoja na kutunga sheria na kuzisimamia.
   
 11. only83

  only83 JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mkuu analysis kama hizi za kisomi uwa watawala wetu hawaelewi..waache wapande mlima na kushuka wakati haina madhara chanya ya moja kwa moja kwa wanaofanya hivi vitendo.
   
 12. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  We Kijana shika adabu zako, nani kakwambia Musoma hatujui kishwahili?? Wewe hujui huyo aliyekikuza na kukilea kiswahili hadi kikaongewa nchi nzima alikuwa mwana wa Musoma??!!! Anyway we don't take any pride with that language of ubwabwa
   
Loading...