JK kukiri hali ya fedha serikalini ni mbaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK kukiri hali ya fedha serikalini ni mbaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, Feb 4, 2012.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,516
  Likes Received: 19,940
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]JK akiri hali ni mbaya serikalini[/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Saturday, 04 February 2012 09:06[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  0digg
  [​IMG]
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati wa maadhimishO ya Siku ya Sheria yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam jana.Kushoto ni Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman.Picha na Zacharia Osanga​
  James Magai
  RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwa katika kipindi hiki Serikali iko katika hali mbaya kifedha kiasi kwamba inashindwa kutekeleza shughuli katika idara mbalimbali kwa wakati. Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa salaamu za maadhimisho ya Siku ya Sheria zilizofanyika nje ya Viwanja vya Mahakama Kuu Dar es Salaam. Kauli hiyo ya Kikwete ilitokana na kilio cha Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman kuwa Mahakama nchini imekuwa ikishindwa kutekeleza majukumu yake kwa mafanikio kutokana na ama kucheleweshewa pesa au kupewa chini ya mahitaji.

  Jaji Othman alisema fedha zilizoidhinishwa na Bunge mwaka 2011/2012 kwa ajili ya Mfuko wa Mahakama ni Sh 20bilioni, lakini katika kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba 31 walitegemea kuwa na Sh 10bilioni, lakini wamepewa Sh6,327,796,972 tu. Akijibu kilio hicho, Rais Kikwete alikiri kuwepo kwa uhaba wa fedha serikalini, lakini akabainisha kuwa hali hiyo imetokana na hatua ya kulipia malimbikizo ya madeni ya nyuma.

  “Sehemu kubwa ya mapato ya Serikali katika hii nusu ya kwanza, imetumika kwa ajili ya kulipia malimbikizo ya madeni ya nyuma,” alisema Rais Kikwete bila kufafanua madeni hayo yaliyolipwa na kuongeza kuwa hata wizara nyingine nazo hazikuweza kupewa pesa kama zilivyostahili kwa mara moja. Alisema karibu madeni hayo yatamalizika kulipwa na kwamba mpaka sasa zimebakia kama Sh 40bilioni tu.

  Pia Kikwete aliihakikishia Mahakama kuwa ataipatia kiasi chote cha fedha iliyoidhinishwa na Bunge huku akikiri kuwa hata kiasi hicho pia bado ni kidogo. “Itabidi hata tupunguze sehemu nyingine, kuna maeneo mengine wana bajeti ya matrilioni ambazo sidhani kama katika kipindi hiki cha miezi sita zitaweza kuwa zimetumika zote kwa mara moja,” alisema Rais Kikwete.

  Jaji Mkuu Othman akifafanua zaidi ucheleweshaji wa pesa za matumizi ya Mahakama alisema kuwa inakuwa ni vigumu kuweza kupata mafanikio ya wazi na kwamba hali hiyo inachangia kukwamisha uendeshaji wa Mahakama.

  “Tunashindwa kuwalipa wafanyakazi haki zao wanazostahili kwa sababu ya ukosefu wa stahili za uhamisho, pia inakuwa vigumu kuwahamisha mahakimu na wafanyakazi wengine," alisema.

  Hivi sasa kuna mahakimu wa Mahakama za Mwanzo 75 na wafanyakazi wa kada nyingine 500 ambao wamekaa kwenye vituo vya kazi kwa zaidi ya miaka kumi. Hili linapunguza motisha, ufanisi na tija,” alisema Jaji Othman.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,516
  Likes Received: 19,940
  Trophy Points: 280
  step down. umepewa nch i na wewe unakuja kulalamika?
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,811
  Likes Received: 83,208
  Trophy Points: 280
  Tatizo la pesa Serikalini tulianza kulijadili hapa jamvini tangu mwezi August/September 2011 miezi miwili/mitatu baada ya bajeti ya 2011/2012. Baada ya miezi mitano/sita baadaye ndio Kikwete anatamka hadharani kwamba Serikali ina ukata wa kutisha. Huu usiri wa miezi yote hii ulisababishwa na nini? unamsaidia nani? Siyo Siri Kikwete na Serikali yake wameshindwa kazi hivyo wanastahili kujiuzulu haraka sana.
  ~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

  JK akiri hali ni mbaya serikalini

  Saturday, 04 February 2012 09:06


  James Magai
  Mwananchi

  RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwa katika kipindi hiki Serikali iko katika hali mbaya kifedha kiasi kwamba inashindwa kutekeleza shughuli katika idara mbalimbali kwa wakati. Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa salaamu za maadhimisho ya Siku ya Sheria zilizofanyika nje ya Viwanja vya Mahakama Kuu Dar es Salaam. Kauli hiyo ya Kikwete ilitokana na kilio cha Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman kuwa Mahakama nchini imekuwa ikishindwa kutekeleza majukumu yake kwa mafanikio kutokana na ama kucheleweshewa pesa au kupewa chini ya mahitaji.

  Jaji Othman alisema fedha zilizoidhinishwa na Bunge mwaka 2011/2012 kwa ajili ya Mfuko wa Mahakama ni Sh 20bilioni, lakini katika kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba 31 walitegemea kuwa na Sh 10bilioni, lakini wamepewa Sh6,327,796,972 tu. Akijibu kilio hicho, Rais Kikwete alikiri kuwepo kwa uhaba wa fedha serikalini, lakini akabainisha kuwa hali hiyo imetokana na hatua ya kulipia malimbikizo ya madeni ya nyuma.
  “Sehemu kubwa ya mapato ya Serikali katika hii nusu ya kwanza, imetumika kwa ajili ya kulipia malimbikizo ya madeni ya nyuma,” alisema Rais Kikwete bila kufafanua madeni hayo yaliyolipwa na kuongeza kuwa hata wizara nyingine nazo hazikuweza kupewa pesa kama zilivyostahili kwa mara moja. Alisema karibu madeni hayo yatamalizika kulipwa na kwamba mpaka sasa zimebakia kama Sh 40bilioni tu.

  Pia Kikwete aliihakikishia Mahakama kuwa ataipatia kiasi chote cha fedha iliyoidhinishwa na Bunge huku akikiri kuwa hata kiasi hicho pia bado ni kidogo. “Itabidi hata tupunguze sehemu nyingine, kuna maeneo mengine wana bajeti ya matrilioni ambazo sidhani kama katika kipindi hiki cha miezi sita zitaweza kuwa zimetumika zote kwa mara moja,” alisema Rais Kikwete.
  Jaji Mkuu Othman akifafanua zaidi ucheleweshaji wa pesa za matumizi ya Mahakama alisema kuwa inakuwa ni vigumu kuweza kupata mafanikio ya wazi na kwamba hali hiyo inachangia kukwamisha uendeshaji wa Mahakama.
  “Tunashindwa kuwalipa wafanyakazi haki zao wanazostahili kwa sababu ya ukosefu wa stahili za uhamisho, pia inakuwa vigumu kuwahamisha mahakimu na wafanyakazi wengine," alisema.

  Hivi sasa kuna mahakimu wa Mahakama za Mwanzo 75 na wafanyakazi wa kada nyingine 500 ambao wamekaa kwenye vituo vya kazi kwa zaidi ya miaka kumi. Hili linapunguza motisha, ufanisi na tija,” alisema Jaji Othman.
   
 4. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Yetu macho maana ikiwa ni hivyo hali itazidi kuwa mbaya.
   
 5. M

  Makupa JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  unatumia nini kufikiri wewe, kama akina Obama nao wanalalamika kuwa hali za nchi zao kiuchumi ni mbaya sembuse kanchi ketu kachanga
   
 6. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Zile zilizochotwa za EPA hazijarudishwa??
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Pole baba, Mungu atajaalia. As long as tuliweza kumudu kusherehekea miaka 50 ya uhuru kwa mbwembwe, na tukiweza kusherehekea sikukuu ya chama chetu chenye kushika hatamu! Hakutaharibika neno. Tunangojea khanga na kofia (mngetushonea madera kabisa manake hata buku tatu ya mashono ni issue pevu!)
   
 8. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  You dont seem to understand what is at stake!
  Legacy ya JK kwa sasa haina hali nzuri sana,kiuchumi mambo si mazuri kwa mtu wa kawaida.
  Inflation ni karibu 20%, interest rates kwenye mabenki inakarivbia 30%(inabidi uwe mwenda wazimu kukopa benki zetu)
  Kwa bahati mbaya sana ahadi ni nyingi kuliko uwezo wetu, austerity hakuna!
  It is a late realisation kuwa kuongoza nji hii si hotuba nzuri tu na kukagua magwaride.
  Strategic economic policies na kujifunga mkanda kitaifa ndiyo vitu watu wanavotaka kusikia.
   
 9. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  pesa nyingi wanazitumia kutafuta watu waliowatangaza wao kuwa wamekufa.......ni lazima nchi iishiwe pesa..watanzania amkeni..muondoeni huyo ni mzigo kwa taifa lenu
   
 10. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  hebu nipe mipango ya maendeleo iliyonayo nchi yako kwa mwaka 2012-2013 katika nyanja za elimu na kilimo kama kweli unaielewa nchi yenu!!! taifa lenu halina muelekeo.....
   
 11. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180

  Invincible ignorance!!!
   
 12. y

  yaya JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, uchanga wa nchi huru kama Tz unaisha katika umri wa miaka mingapi tangu kupata uhuru?
  Juzi tu kulikuwa na sherehe za kukata kwa shoka kuonesha ukomavu wa nchi hadi makomandoo wakavunja tofali kwa vichwa, bado Tz ni nchi changa tu?
   
 13. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  umoja wenu ndio silaha yenu......maneno aliyoyatoa huyo rais wenu ni aibu sana kwa taifa ..ninyi ndio mna jukumu la kuhakikisha mnakuwa na taifa lenye ustawi...lakini kwa sasa hakuna.....tafuteni shujaa wenu mwingine mwalimu alishatangulia
   
 14. kitonsa

  kitonsa JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Sasa kama vipaumbele vyenyewe ni vazi la taifa kwa nini nchi isifilisike?
   
 15. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  uwezo wa raisi wenu ni mdogo sana tena sana....hata anapokuwa katika vikao hajui anachoongea...labda niwape hii muone hii juzi alipokuja DAvos muone jinsi anavyojibu maswali na asivyojua lugha......watanzania mmekuwaje siku hiz...rudisheni hadi ya taifa lenu!!!
  Swali.What are going to be the forces of change to improve the performanceof Africa which has already shown that it is making a difference;whether is education that has to be improved, or whether it isinfrastructure, or development of IT, whether it is regionalcooperation or whether it is greater trade with the rest of theworld, or whether it is development of new industries, or whether istrade regulation....(Gordon Brown)
  JIBU (MH JK)
  Indeed one can say there is transfo, transformation taking place inAfrica
  There is a lot ample evidence to that fact, emh
  When you look at the socio-economic lives of our people and ournations in education, in healthcare, infrastructure development, inagriculture, in manufacturing and so forth and so, but much more needto be done, this is the bottom line. Of course, there are times whenAfrica is portrayed as there is nothing happening, but i would saythe contrary. Ther is a lot of happening.
  But much more needs to be done. And why, because we are strating fromlow levels of development
  At independence, 50 years ago, Tanzania , the GDP per capital was 35dollars. There was only three tarmac roads the length of 190kilometers. And we are country with 85,000 kilometers of roadsnetwork. So this,we started from low levels of development, diseases,deprivations of all sorts of.....we have plenty. But also we are partof the global economy, so whatever is happening in some parts of theworld definitely affects us.


  A few years ago, we had global economic financial crisis and we hadreversals to our growth. Now we have a lot of anxiety with theEurozone crisis I hope it is going to be fixed quickly so that if, ifit doesn't , then there is going to be a many problems. There isevidence of growth, high levels of growth. I think this, the fastestgrowing continent now. But plengesare still there. So more needs to be done, eehh to be very precisein my view one Africa must stay the course in pursuit of soundeconomic policies. Because it it sound economic policies which hasenabled many of our countries to attain micro-economic stability. Thehigher lev highl....low inflation rates high levels of growth.So weshould stay the course in pursuit of sound economic policies. Weshould invest more in education;primary, secondary, tertiary,technical training in order to build the human resource, because atthe end of the day it is the man or woman who is going to make thingshappening and not the machines. You can have the machines if you donthave a competent people to use the machines then nothing can happen.So education is, is critical, as, as, as a major impet.We should invest more in the transformation of agriculture. To meagriculture is a priority because seventytwenty percent of our people live in rural areas andagriculture is their mainstay, but issubsistenceagriculture, people live from hand tomouth, they cannot feed themselves.they dont have enought cash cropsto be able to earn more to transform their lives better


  We need to develop manufacturing sector. Wecannot continue to be primary producers – produce raw materials forthe others to go and make goods, finished goods and then come back. Iwas saying my Blake proffesor of economics at the university taught m, we used to have a good phrase, we produce what we dont consume andconsume what we dont produce---Ahha aahhhhaaa...we produce for theothers so that the others produce for us to consume. This thing can'tcontinue.Thats why may ensuring that the manufacturing sector isgrowing faster in Africa is also critical. We have abundantresources, mineral resources, agricultural resources, naturalresources but what is lacking is vibrant manufacturing sector whichAfrica should look at.


  And in any cae, economies transit from beingpredominantly agricultural, then they go to manufacturing, and thenthey go to the service, to the service becoming the predominant one.So this is another important aspect. We have to developinfrastructure. Well, as I am saying we had only three, three, threeroads in the country with a demand of 85,000 kilometre square ofkilometers of roads. Without roads there is no development, there isno development withou electricity, there is no development withouttelecommunications. Africa cannot continue to be left behind in thedigital divide. Definitely we have , have , we have to catch up. Theother thing is regard intergration. If we , if we say we are going toproduce more and from agriculture, produce more from manufacturing,definetely markets are essential. Regional markets but alsointernational markets. For regional markets, of course there areregional economic groupings are an important factor. This is , thisis a, a song now in the whole of African continent. The regionaleconomic groupings everywhere and we have continuosly stregtheningthem. We are now looking at even merging them, eehh. In july we had ameeting in South Africa where we discussed the creating a grand freetrade area bringing together Southern Africa Development Community,East Africa Community, Commont Market for Southern and CentralAfrica. From Cape Town to Cairo.......I was saying in Addis Ababa,eeeh on South Africa the other day Cecil Rhodes Jones the colonisttalked of the eehhh, ...Great North Road from Cape Town to Cairo butthis was for colonial purposes. We are , we are doing it now for ourown, for our own good....hahahaha...hahaaa....this is an aspect. Butalso at international level now we need access to markets, thats whyto us in Africa early conclusions of DehaDeclarationAgenda the round is, is, is so critical, so that we can remove openup the markets, remove trade distorting subsisdies in the developedcountries so that we can have access to markets. I can say that forthe begining , ....let me say that to start with

  (akakatishwa naGordon Brown baada ya kuona haeleweki.................)

  Davos 2012 - Africa - From Transition to Transformation - YouTube
   
 16. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 4,543
  Trophy Points: 280

  Yaani ujifikiria namna hizo sherehe zilizofanywa kuanzia mwanzo wa mwaka jana hadi kilele chake,hakika unaona hii ni nchi ya majuha inayoongozwa na mfalme ****.

  Haingii akilini,nchi itumie pesa nyingi kiasi kile kwenye kila idara,wakala na taasisi za serikali na umma kuonyesha 'mafanikio' ya miaka 50 ya "uhuni". Halafu leo mfalme **** analalama serikali ina ukata!
   
 17. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180

  nchi yenu ni nzuri wa mipango lakini haitekelezi...huyo mnayemwita raisi kazi yake ni kuchukua orders toka kwa aliyemweka hapo!!...hana dira maono raisi wenu.....
   
 18. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sihitaji hata kusoma ulichoandika but.......naamini haihitaji kutumia akili kujua kwamba hali Ni mbaya serikalini....mambo vululu vululu, angalia tu tanesco, tizama Ishu ya migomo ya madaktari.....makashfa ya ufisadi yanayojitokeza kila siku....unachotaka Ni nini tena kujua hali Ni mbaya Huko serikalini?!
   
 19. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  rudisheni hadhi ya taifa lenu kwa kuuondoa utawala dhalimu kama huu......hawa watu hawana huruma na wananchi wake na huyo....wenyewe mnanona kinachoendelea kuhusu madakari ..kuweni kitu kimoja muwaondoe hapo walipo....kilichobaki kwako ni kuua watu hovyo na kutangaza wengine kuwa wamekufa kumbe wako hai na buheri wa afya.....can someone wake up this nation!?
   
 20. PAMBA1

  PAMBA1 Member

  #20
  Feb 4, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kama mkuu wa nchi kakubali hali Ni Ngumu wakati anaishi ikulu na analetewa Kila kitu je wale wa Tanzania masikini waliokuwa wanakula chakula cha mlo mmoja kabla ya yy kuona au kutanganza Hali Ni mbaya wanaishije huko waliko si ndo hawapati chakula kabisa huku mnawaletea mchakato wa vazi la taifa jamani Hawa watanzania wanalala na njaa huku wizara inahangaika kutumia pesa kupata vazi la taifa jamani tuendako Ni wap watanzania wezangu na hii nchi ya kisanii jamani vazi la taifa huku watu tunahali Ngumu kumbe tunathamani wakati wa kampeni tu hili watanzania tulikatae.
   
Loading...