BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,792
- 287,994
...Nchi ina utajiri wa kutisha...Dhahabu, Almasi, Tanzanet, misitu ardhi yenye rutuba ya hali ya juu lakini wanaofaidika ni wageni na mafisadi walio Serikalini na marafiki zao huku nchi ikishindwa kuwa na pesa hata za kujiendesha. Majirani zetu Botswana dhahabu yao wanagawana pasu kwa pasu na wawekezaji (50%) sie tunawaachia wachukuaji wachukue 97% ya mapato yote yanayotokana na dhahabu yetu ikiwafaidisha shareholders wao na wale walio katika managament positions za makampuni ya wachukuaji huku nchi ikikosa hata pesa za kulipa mishahara kwa Wafanyakazi wake!!!!