JK kufanya uamuzi mzito 2013

JK kufanya uamuzi mzito 2013

engineerm

Senior Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
106
Reaction score
19
Kuhusu Rais Jakaya Kikwete, alisema mwaka huu atafanya uamuzi mzito utakaoungwa mkono kwa asilimia 100 na kwamba uamuzi huo utaishangaza dunia.

Gazeti la mtanzania leo,

Ni uamuzi gani huo wana jf?
 
mbona hii inashabihiana sana na ile taarifa ya Hutaki Unaacha na mtoa habari!!!
au labda mbwembwe tu anataka kuongeza mke wa 8

Wakuu naombq mnisaidie kuweka links za thread za hutaki unaacha
 
Nafikiri kama yuko seriou huenda akafanya moja wapo kati ya haya(UTANI):
1/Ataamua kujiuzuru urais kwa sababu nchi imemshinda

2/Atashinikiza kurudishwa kwa pesa na wanyama waliotoroshwa nje ya nchi na wahusika kunyongwa.

3/Itatangaza kufutwa rasmi kwa CCM kwa sababu kinakumbatia ufisadi siku zote.
 
Ni kweli. Ataishangaza dunia ima kwa kutofanya uamuzi wowote mzito na wa maana au kufanya uamuzi mwepesi na wa hovyo badala ya uamuzi mzito. Tushamzoea na sanaa zake. Ni ajabu kuwa na rais ambaye hawezi kuwa makini hata dakika moja. Yetu mecho.
 
Pengine atamrudisha Lowassa kuwa waziri mkuu! kwa hilo mimi ningemuunga mkono maana Pinda amedhihirisha kiatu alichokivaa ni kikubwa sana kwake kiasi kwamba miziziology haimsaidii...
 
Tunazipata taarifa rasmi kabla ya tukio tu. Jf makini km ataishangaza dunia kwa yanayoendelea kwa kina nchale kila kona nchale.
 
Ataamua kujinyonga ili tufanye uchaguzi kabla ya 2015
 
Kuhusu Rais Jakaya Kikwete, alisema mwaka huu atafanya uamuzi mzito utakaoungwa mkono kwa asilimia 100 na kwamba uamuzi huo utaishangaza dunia.

Gazeti la mtanzania leo,

Ni uamuzi gani huo wana jf?

huujui mkuu...alishafanya siku nyingi...katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015, mtake msitake ndiyo hivyo.
 
Atafanya uamzi mgumu kukifuta chadema maana ni chama cha kikanda na udini na ni chama kinacho ongoza kuwashawishi watu wa kusini ili waandamane kwa ajili ya gesi
 
jk atafanya uamuzi mgumu wa kumpa Deo kisandu kofia ya urais.
Dont forget this CHADEMA kuweni makini sana, kilicho nyuma ya pazia hiki hapa!=

Wapendwa wanaJF,


2. JK ajiuzulu urais mnamo mwaka 2013 hivi ili chini ya Bilal na kwa muda mfupi mabadiliko makubwa yafanyike na CHADEMA waweze kujumuishwa katika serikali hasa Dr Slaa ili kujipanga kukimaliza CHADEMA kwa urais zaidi. Ingawa JK alihofia hii technique kwa maana ya Bilal but hii naona ina mkono wa “wafanyabiashara” wakubwa wa mataifa Fulani ambao wanataka biashara zao ziende vizuri kama JK ataondoka madarakani kwani akiendelea hataweza kumweka mtu wao ili aendelee kulinda 'maslahi Fulani'

Thank you.
 
Ataitangazia dunia kuwa kweli 2010 hakushinda Urais na 2005 yeye na washirika wake walitoa fedha Serikali wakaonga sana kupata ushindi, na sasa dhamila yake imemshitaki na anahamua kuachia madaraka kabla ya 2015
 
JK kufanya uamuzi mzito ni kama duara la mraba, haliwezekaniki katika ulimwengu huu.

Uamuzi wowote atakaofanya hata kama unatakiwa uwe mzito utarahisishwa naye.
 
JK kufanya uamuzi mzito ni kama duara la mraba, haliwezekaniki katika ulimwengu huu.

Uamuzi wowote atakaofanya hata kama unatakiwa uwe mzito utarahisishwa naye.

Huwa natamani kila unapoandika hapa JF uni-tag, msomaji vitabu-i like u
 
Unajua maana ya Kichuli?

Atafanya uamzi mgumu kukifuta chadema maana ni chama cha kikanda na udini na ni chama kinacho ongoza kuwashawishi watu wa kusini ili waandamane kwa ajili ya gesi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom