CHADEMA kuweni makini sana, kilicho nyuma ya pazia hiki hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA kuweni makini sana, kilicho nyuma ya pazia hiki hapa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hutaki Unaacha, Jun 15, 2012.

 1. Hutaki Unaacha

  Hutaki Unaacha Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wapendwa wanaJF,

  Kwanza niwaombe radhi kwa kukaa kimya kwa muda mrefu baada ya kutoa part II na kuahidi kuendelea kutoa part III ambayo ingekuwa ya mwisho. Ninajisikia vibaya kwa kukaa kimya bila kuwajulisha chochote. Mnisamehe kwa hilo. Ninafahamu wengi mtanielewa nikisema kwamba nimeacha kwa sasa kuendelea na ile series mpaka pale muda mwafaka utakapowadia tena. Kuna mipango mingi ambayo nilitaka kuielezea ya ndani zaidi (hasa kama ningefikia kwa Apson na Edward) ambayo kwa namna moja nyingine ingekuwa na matokeo ya aina mbili tu yaani kutengeneza mwanzo wa njia ya kuelekea kwenye ukombozi wa taifa letu au uvunjifu wa amani kubwa ambayo haikuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu (nime-consider taifa kwanza ingawa ya kwangu ni tofauti na intelijensia ya mwema). Muda ukifika nitaleta habari yote ikiwa kamili na kwa hili sitakaa muda mrefu kama ambavyo huwa nafanya. Naomba tena mnielewe kwa hilo na kusema ukweli nawaomba radhi sana tena sana kwa hili.

  Lakini kuna hili ambalo imebidi nisiliache na kwa haraka haraka na mpangilio mbovu naomba nilitoe hasa kwa CHADEMA na rafiki zake. Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa. JK anakiri na ameendelea kukiri kwamba EL ameharibu mipango yake mingi sana. Analalamika sana jinsi ambavyo EL ameharibu strategies zake za kumweka mtu wake Ikulu. Kwa bahati mbaya sana JK amekuwa akishinikizwa na baadhi ya "washika dini" kumweka muislam kwenye urais wa 2015 kwa muda mrefu sasa. Niseme wazi kuwa sina shida na Islam na hata wakiongoza consecutively kwa miaka 400. Tatizo naliona pale ambapo dini inakuwa sifa. Na wapo waislamu wengi ambao hawaipendi tabia hii maana baadhi wanasema inawadhalilisha. Najaribu kutoa habari tu. Sitaki tuingie kwenye malumbano ya dini. I love my country. Mtu wa mwisho ambaye EL amemharibu ni Nundu..JK ameumia sana. Sikuwahi kumwona JK akiumia kiasi hiki baada ya mpendwa wake wa 2015 (Nundu) kuharibiwa. Nafahamu wengi watashangaa kumwona JK akihangaika kumweka Nundu 2015 akiwakilisha CCM. Nataka niseme wazi kuwa, yeye ndiye alikuwa anaandaliwa. Ninao ushahidi wa wazi kabisa. Nahodha, Hussein, Asharose (ambaye ame-underperform na "kufukuzwa" na Ban) etc wameonekana hawawezi kushindana na EL ndani ya CCM. Hata Emmanuel, Membe etc ambao labda wangeweza kutumika kushawishi kanisa hawawezi kushindana na EL ndani ya CCM.

  Kwa ufupi sana, ripoti iliyomfikia JK kutoka state department ilimnyong'onyeza JK pale ilipobainika wazi kuwa hakuna mwanaCCM ambaye atamshinda EL 2015. Baada ya kuona hakuna namna nyingine, mwezi uliopita JK na EL wamekutana karibu mara 4 na "kusameheana" ili kujenga mtandao wa kuendelea kuwa na mtu wao 2015 as a president..Katika mkutano ule ambao Rostam hakuhudhuria labda kwa sababu ya ugonjwa wa baba yake mzazi (anamuuguza baba yake kwa sasa), lengo lilikuwa ni kupanga mipango ya nini kifanyike ili CHADEMA wasishinde urais 2015. Katika mikutano yao, imeonekana kwamba, ni vigumu kumshinda Dr Slaa kwa kura (kumbuka huyu katika uchaguzi wa 2010 alipata 47.3% kama matokeo halisi kabla ya uchakachuaji wa kishamba kufanyika). Kwa maana hiyo mambo/alternatives yafuatayo yaliazimiwa (hili ni muhimu sana na ushabiki uwekwe pembeni ili muweze kunusuru chama chenu na mikakati yenu);

  1. Ule mpango wa kuipasua CHADEMA (unaohusisha viongozi wa dini walio karibu na CHADEMA au Slaa na kuratibiwa na idara kwa usiri wa hali ya juu) usitishwe kwa muda ili kuona kama mipango mingine itafaulu.

  2. JK ajiuzulu urais mnamo mwaka 2013 hivi ili chini ya Bilal na kwa muda mfupi mabadiliko makubwa yafanyike na CHADEMA waweze kujumuishwa katika serikali hasa Dr Slaa ili kujipanga kukimaliza CHADEMA kwa urais zaidi. Ingawa JK alihofia hii technique kwa maana ya Bilal but hii naona ina mkono wa "wafanyabiashara" wakubwa wa mataifa Fulani ambao wanataka biashara zao ziende vizuri kama JK ataondoka madarakani kwani akiendelea hataweza kumweka mtu wao ili aendelee kulinda 'maslahi Fulani'

  3. Katiba ijayo iruhusu serikali tatu na by any means ilazimike kuwa EL awe rais wa Tanganyika, Dr Slaa/CHADEMA wa Muungano (asiye na nguvu yoyote) na Shein aendelee Zanzibar.

  4. Moja ya watu wenye nguvu ndani ya CHADEMA ashawishike kugombea kama independent candidate (sio Zitto) na malipo yake yawe competitive na campaign yake 2015 iwe sponsored kwa gharama yeyote ile.

  CHADEMA kuweni makini sana na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ambao wanaweza kuwaharibia your way to 2015. Muda umeniishia kwa leo maana nasafiri muda si mrefu otherwise nikipata muda tena nitawapa updates. Thank you.
   
 2. T

  The State Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Duh, Hutaki Unaacha akishakuja tu hali ya hewa nchini na JF huwa inabadilika kwa muda..Ngoja kwanza nikae chini ili nisome nikiwa nimepumzika..Mama watoto lete juice!
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  Kwamba JK atakubali kuachia madaraka kabla ya muda? Nitashangaa sana, he does not look like he can that easily leave that office...
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,329
  Trophy Points: 280
  Mkuu Hutaki Unaacha, karibu tena.

  Msamaha wako nimeuelewa na nimefarijika kukuona bado upo maana nilihisi watu wako wameisha kupotezea!.

  Tukija kwenye haya usemayo kuhusu Chadema na 2015, this is too good to be true!.

  Hata hivyo nasubiria!.
   
 5. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Anaweza, tena vizuri sana, Hataki shida yule ni muoga sana.
   
 6. Kocha

  Kocha JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 2, 2008
  Messages: 375
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Nashauri hizi habari zifanyiwe kazi ipasavyo na Intelijinsia ya CHADEMA, zisipuuzwe kwani itasaidia kuwa na uhakika wa ushindi 2015 inawezekana kuna ukweli ndani yake
   
 7. S

  STIDE JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Naiona Tanzania katika machafuko ya kisiasa!!
   
 8. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,034
  Likes Received: 23,789
  Trophy Points: 280
  Mambo ya kusadikika haya. Sijapata picha ya lolote kati ya haya kuwa litatekelezeka.

  Ngoja tu nisitake na niyaache
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ee Mungu linusuru Taifa lako.
   
 10. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  baadhi ya mipango uliyoongelea ni kweli
   
 11. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  kwani wakuu ule mkutano tulioambiwa ulifanyika kwa siri kati kub na jk unaweza kuwa classic info. ku-justify angalau kwa mbaaali maelezo ya Hutaki Unaacha?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hutaki unaacha, asante kwa nondo, sisi tunatafakari na kuangalia upepo uvumavyo.

  Kitu ninachokubali moja kwa moja ni Chadema kuweni makini, kila clue inayopatikana, kwa watu makini ni jambo la kufanyia kazi.
  Nani asiyejua kuwa kura za Dk Slaa zilichakachuliwa? CCM wanajua wazi kuchakachua kura za urais 2015 itakuwa kazi ngumu sana, na yawezekana matokeo ya uchakachuaji kura za urais 2015 yanaweza kuingiza nchi yetu kwenye historia na ukizingatia ICC imeshatinga Kenya, wanatutolea macho Tanzania.
   
 13. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Manao copy habari yote acheni hizo tabia mnakera kwa sababu tushaisoma nawe unairudisha kama ilivyo
   
 14. B

  Bhavick JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mungu tuokoe!
   
 15. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #15
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Hutaki unaacha hilo la mtu mwenye NGUVU ndani ya CHADEMA Kugombea kama private candidates nimelisikia baada ya CCM kuridhia mgombea Binafsi kwenye kikao kilichopita, ila huyo uliyesema siye watu wanasema ndiye anayeandaliwa kufanya hivyo.
   
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Haya twende kazi.
   
 17. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ngumu kumeza! CDM endeleeni na taratibu zenu, msiweke nguvu nyingi kufuatilia ukweli au uongo wa haya mambo. Tricked
   
 18. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Hivi jamani laana inachukuaga mda gani mpaka ianze kazi? Maana mhh
   
 19. S

  STIDE JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hutaki Unaacha, please kama ulivosema waipenda Tz, hebu onyesha uzalendo wako kwa kututafunia huyu alieandaliwa!! Ili tuwe nae makini. Please!!
   
 20. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Heee. ukiona hivo ujue miti yote inateleza. Ujanja huo nduo ulioiangamiza Cuf.
   
Loading...