JK kufanya uamuzi mzito 2013

JK kufanya uamuzi mzito 2013

Atamkaribisha Bush na kumkabdhi kigamboni kabla ya katiba mpya.
 
Labda ya kufa na kufufuka hapo ntamkubali!!!


Kuhusu Rais Jakaya Kikwete, alisema mwaka huu atafanya uamuzi mzito utakaoungwa mkono kwa asilimia 100 na kwamba uamuzi huo utaishangaza dunia.

Gazeti la mtanzania leo,

Ni uamuzi gani huo wana jf?
 
kashindwa miaka yote 2013 atawezaje? he is fairly a total failure to say the least
 
kwani ile dossier au faili limekamilika na muda umetimia ili aweze kuchuakua uamuzi mzito
 
Kuhusu Rais Jakaya Kikwete, alisema mwaka huu atafanya uamuzi mzito utakaoungwa mkono kwa asilimia 100 na kwamba uamuzi huo utaishangaza dunia.

Gazeti la mtanzania leo,

Ni uamuzi gani huo wana jf?
Atakamkabithi Nchi nanihii!!! yule mama yule oh sorry yule mwanamuziki wa bongofleva baada ya kupona kabisa!!
 
Atafanya uamzi mgumu kukifuta chadema maana ni chama cha kikanda na udini na ni chama kinacho ongoza kuwashawishi watu wa kusini ili waandamane kwa ajili ya gesi

Atafanya maamuzi magumu kumpandisha Kichuli kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM na kumshusha Nepi
 
kila mwaka anasema atafanya maamuzi mazito....mbuzi kwa gunia!
 
KUTOKANA NA HAYO MAELEZO:-
Hali ya Kijamii:
Natabiri: kwamba katika Mwaka huu wa 2013 Ndoa nyingi zitavunjika. Watu wengi, wakiwemo Mawaziri na Viongozi Waandamizi wake kwa waume, watajikuta katika kashfa ya Ngono, Kufumaniwa au kufumania na kupigana kiasi cha baadhi yao kuuawa.
Natabiri; Kuwa maisha katika mwaka huu yatakuwa mazuri, lakini kwa Watanzania watakaojifunga mikanda kuelekea katikati ya mwaka 2013.
Natabiri: Maradhi ya watoto kuongezeka katika Mwaka huu wa 2013 na hasa ya kifua na kichwa. Wanawake wengi wajawazito watapoteza maisha kwa kujifungua na au kuzaa kwa matatizo makubwa ambayo hayajawahi kuonekana.
Natabiri: Ajali zitakuwa nyingi, kuchafuka kwa bahari kutakuwako kwa wingi na kutakuwa na hofu ya watu wengi kuuawa.
Natabiri: Kutokea kwa mioto mikubwa kwenye miji mikubwa, Njaa kuongezeka, ukosefu wa maadili, wafanyakazi kuwapiga mabosi wao, uongo mwingi kwa maana ya propaganda,
Natabiri: Umbeya utakua kwa kiwango kikubwa mwaka huu wa 2013, pamoja na masengenyo.
Natabiri vifo vya Mashujaa au wale watakojiona ni mashujaa.
Natabiri: wingu zito la vifo vya ghafla kwa watunzi wa hadithi na vitabu, Waandishi wa habari, Wanasiasa na Wasanii na muda huu itakuwa mbaya zaidi ya mwaka jana.
Hali ya Kisiasa:
Natabiri: Viongozi wengi wakiwemo Wabunge, Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wenyeviti wa vyama na Makatibu wao watatoa matamshi ya utatanishi na kusababisha khofu na mitafaruku mikubwa itakayowafanya watu kupigana.
Hata hivyo, hali hiyo itadumu kwa muda mfupi. Kwani baadhi ya viongozi watalazimika kukaa pamoja na kukubaliana mambo baina yao na kurejesha hali ya utulivu na amani.
Natabiri: Wabunge wengi katika Bunge la Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania wataungana katika masuala yatakayohusu Utaifa bila kujali itikadi zao za kivyama au kimajimbo. Hata hivyo, nyota zinaonesdha kuna baadhi ya wabunge wataanguka Bungeni wakati wa majadiliano.
Kinyota haionekani kuwa kutakuwa na athari lakini itapaswa kufanyika juhudi za ziada kuokoa maisha yao.
Natabiri Rais Jakaya Kikwete maarufu kama “JK” kufanya mambo ya ajabu na yasiyotabirika na ataungwa mkono kwa asilimia 100 na wananchi wote wa Bara na Visiwani.
Natabiri JK atatenda maamuzi magumu katika mwaka 2013 kiasi cha dunia kushangaa.
Natabiri: JK ataendelea kupata wasaidizi sadifu hasa kwa upande wa Uwaziri. Vile vile nyota za Mawaziri Harrison Mwakyembe, John Pombe Magufuli na Khamisi Kagasheki zitazidi kungara Mwaka huu na kuungwa Mkono na Wananchi
Natabiri JK ataunganisha nchi na kuwa moja yenye uimara wa Utaifa kuliko watangulizi wake. na atashirikiana zaidi na Wanasiasa na viongozi wa dini kuondoa mtikisiko wa uvunjifu wa amani uliokuwapo nchini mwaka jana.
Natabiri Chama kimoja cha siasa hapa nchini kuchochea kujitenga na kuunda Taifa lake. Hata hivyo, kusudio hilo halitafanikiwa. Kwani litapingwa na Watanzania wote kwa kauli na vitendo.
Natabiri:. Natabiri Tanzania kushinda kwa kishindo kwenye mgogoro wake na Malawi kuhusu Ziwa Nyasa bila kupigana vita.
Hali ya Kibiashara:
Natabiri: Mauzo ya bidhaa yataongezeka na kuongeza neema na watu kufaidika katika biashara. Pia mwisho wa mwaka huu wa 2013 mvua zitaongezeka na mazao yatakuwa mengi.
Natabiri: Wafanyabiashara wengi na hasa wajasiriamali kufanikiwa katika kazi zao.
Natabiri: Neema itawaangukia wajasiriamali wa aina zote hapa nchini kwa mwaka huu.
Natabiri wawekezaji wengi zaidi mwaka huu watajikita kwenye biashara ndogondogo kuliko ilivyokuwa katika miaka iliyopita.
Natabiri: Sakata la gesi ya Mtwara litatulia na kumalizika kwa amani katika mwaka huu wa 2013 kwa wananchi wote kuungana na kuunga mkono matumizi yake kwa faida zaidi ya Taifa badala ya jimbo au majimbo
Natabiri: Nchini Kenya ambao ni Majirani zetu Muungano wa CORD ukiongozwa na Raila Odinga kushinda uchaguzi wa Kenya ambao utakuwa wa amani na utulivu na kuwashinda Kina uhuru Kenyatta na Ruto na Muungano wao wa JUBILEE na ule wa Musalia mudavadi unaoitwaAMANI

Maalim Hassan Yahya Hussein
13/1/2013 Jumapili
 
Atamteua mwanae kuwa mbunge wa viti maalum na kumpa uwaziri wa Maliasili na Utalii ili wafanikishe mbinu zao chafu za kujilimbikizia mali OR else basi atarudisha kichwa chake halali na kuondoa kile alichotengenezewa cha coconut,,, ahahaaaaaaaaa
 
bado sijapata jibu kamili uamuzi gani huo wa kuishangaza dunia nzima?
 
nina mashaka huenda akaungana na mama Banda wa malawi
kukubali sera za Cameroon Tanzania ili tupate misaada
watakaomuunga mkono kwa asilimia 100 ni Marekani na Uingereza
uamuzi huu ndio utakaoishangaza dunia.
sawa na Nyerere alipolazimishwa na mapebari kuacha ujamaa na kungatuka
kama atataka kusaidiwa na WB na IMF.
ilikuwa lazima akubali hivo kuachia ubeberu ufanye kazi yake.
but JK ni mtu alielelewa kimaadili, lets wait and see
 
Back
Top Bottom