JK kiboko...... Kawapa live madaktari

Honey K

JF-Expert Member
Sep 14, 2008
629
72
Kumbe mkulu kaongea na umma?!!!!! Nimeikuta hii kwenye wall ya FB ya vuvuzela wa CCM,

"Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la heri. Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo." Rais JM Kikwete, 01/07/2012.
 
Nchi ya Maneno.Watu Wa maneno. Maneno maneno kila raia maneno.. Mafundi kweli Wa maneno..

Kwani Maneno yanasaidia kuponya wagonjwa?. Watu wanakata roho huku ati, watu wanaotakiwa kufanyiwa operations hawajui hatma zao Na Hali zao zinazidi kudorora.. Hapa watu walioshiba ugali Na Kauzu wanapiga domo tu..

Sikilizeni enyi mbweha.. Hatutaki maneno tena, Kama mnaona madai ya madaktari ni chachu tupilieni mbali wao Na madai Yao kwenye dustbins.. Na muajiri madaktari wengine Na raia tuendelee kupata matibabu ..

Mambo ya maneno ni upuuzi .. Upuuzi mtupu, huyu namlipa sana, sijui yule kidogo, ah ni majungu tu yote hayo.. ilihali wananchi maskini ya mungu tusio Na hatia tunakwisha Kwa kukosa stahiki ya tiba..

Sina Shaka kesho wahandisi nao watalianzisha.. Mhandisi kuanza Na 420,000 Na baada ya makato anakwenda hom Na 320,000 aiseee.. Hata house-girl Wa hapa masaki wanamzidi kipato mhandisi.. Erb mpo au mnachangisha michango ya stickers tu..
 
Safi sana JK kaongea kama rais hii ndio inatakiwa wakuheshimu.... Wakitaka wafanye wasipotaka waende private hospitals. Vile vile narudi ushauri wangu wa siku zote SERIKALI IJITOE KATIKA KUHUDUMIA HIZI HOSPITALI NI ITIKADI YA KIJAMAA NA ISHAPITWA NA WAKATI. BADALA YAKE IHUDUMIE MGONJWA ASIYEWEZA KUPATA HIYO HUDUMA YA AFYA.... WAKIMALIZA SHULE HAO MADAKTARI WAKATAFUTE KAZI URAIANI WAONE CHA MOTO!!!!
 
Lema alisema hawa polisi wetu hata wapokee mishahara ya miaka hamsini awafikii mshahara wa majimarefu wa miaka 5 du!! yani mchawi na injinia mkali nani
 
Safi sana JK kaongea kama rais hii ndio inatakiwa wakuheshimu.... Wakitaka wafanye wasipotaka waende private hospitals. Vile vile narudi ushauri wangu wa siku zote SERIKALI IJITOE KATIKA KUHUDUMIA HIZI HOSPITALI NI ITIKADI YA KIJAMAA NA ISHAPITWA NA WAKATI. BADALA YAKE IHUDUMIE MGONJWA ASIYEWEZA KUPATA HIYO HUDUMA YA AFYA.... WAKIMALIZA SHULE HAO MADAKTARI WAKATAFUTE KAZI URAIANI WAONE CHA MOTO!!!!

Kaongea kama rahisi sio rais
 
Mh atakuwa na mattizo yeye natkiw kusem madai ni y ukweli au la na kuangalia nmn ya kutatua. Asiingize siasa za jazba kwenye sheria za kazi na afya za watu
 
Kuna mambo ya kuchezea lakini si taaluma za watu,maneno ya mipasho,si njia mbadala wala si njia sahihi ya kumaliza au kutatua matatizo yaliyopo.nawashangaa sana na ntazidi kuwaona wapuuzi wale wote wanaoshabekia kauli dhaifu kama hii.madhara yake mtaja yaona soon,maana huwa ni wagumu kufikiri kabla ya kutamka,mkitamka mkaona ghalama ya kutamka mnaanza kuhangaika kufuta kauli.
 
Kumbe mkulu kaongea na umma?!!!!! Nimeikuta hii kwenye wall ya FB ya vuvuzela wa CCM,

"Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la heri. Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo." Rais JM Kikwete, 01/07/2012.

hivi ile package ya demands za ma-dr inazungumzia mshahara peke yake au kuna mengine?mbona wanataka kutuona watanzania ni malofa kiasi hichi,
 
Hapo fanya mil 12X12=mil144 haraf fanya 144X5=mil 720 haf gawanya kwa mshahara wa polisi yeyote unaemjua hata mwema ulipata jibu tafakali usichukue hatua mpaka 2015
 
Kweli raisi kasema msilazimishe maji kupanda mlima tanzania yenyewe hali ni ngumu hizo za kujazia watu zatoka wapi cheers
 
Nimepruvu kikwete nouma haya madaktari kazi kwenu si mnajifanya mnalinga na elimu yenu na vipaji alivyowapa mungu. Mjomba kawamwaga liveee mwenye nguvu ya kujitegemea bila mshahara aache kazi tuone sasa na mbwembwe zenu
 
Wewe husomi katiba ya nchi hujishughulishi na kujua haki za kila raia kama zilivyoainishwa katika katiba ya JMT, Pia hujasoma tamko rasmi la itikadi ya JMT. Maoni yako yanafuata kwa kikamilifu na kwa utiifu mkubwa maneno na maoni ya watu unaowaamini kwa mwonekano wao,nafasi zao katika jamii pia elimu yao bila kujali wanafuata katiba ya nchi au la.

Katiba ya JMT katika sehemu ya Kichwa cha habari inaongelea wazi ni aina gani ya siasa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafuata
-SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________

KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
YA MWAKA 1977
____________
YALIYOMO
_____________
Ibara Kichwa cha Habari

UTANGULIZI

SURA YA KWANZA

JAMHURI YA MUUNGANO, VYAMA VYA SIASA, WATU NA
SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA

Safi sana JK kaongea kama rais hii ndio inatakiwa wakuheshimu.... Wakitaka wafanye wasipotaka waende private hospitals. Vile vile narudi ushauri wangu wa siku zote SERIKALI IJITOE KATIKA KUHUDUMIA HIZI HOSPITALI NI ITIKADI YA KIJAMAA NA ISHAPITWA NA WAKATI.(Bila shaka wewe ndo umepitwa na wakati) BADALA YAKE IHUDUMIE MGONJWA ASIYEWEZA KUPATA HIYO HUDUMA YA AFYA.... WAKIMALIZA SHULE HAO MADAKTARI WAKATAFUTE KAZI URAIANI WAONE CHA MOTO!!!!
 
Tumekusikia jk lakini mbona husemi serikali ime offer shilingi ngapi???? Wewe una lalama kiasi walichoomba wenzako sema na nyie mnatoa ngapi....kwa kauli yako hiyo basi waajiri wa sekta binafsi watajaa kiburi sana kwani watasema maneno kama yako jk na hatutakuwa na paku lalamika
 
Kumbe mkulu kaongea na umma?!!!!! Nimeikuta hii kwenye wall ya FB ya vuvuzela wa CCM,

"Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la heri. Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo." Rais JM Kikwete, 01/07/2012.

Hiki ni kiini macho kwa mtanzania asieelewa ukweli juu ya madai ya madaktari, madaktari wanataka kuboreshwa kwa mazingira ya kufanyia kazi. Yeye JK anaropoka kwa kua akikohoa anapelekwa USA kutibiwa hivyo hajui kua hata Oxygen machine hakuna pale MNH, Hatambui kua mama zetu wanalala watatu kitanda kimoja, Hajui kua daktari analipwa 10'000/= akiwa zamu kukesha, Hajali kua hata Scanning machine iko moja tu Tanzania......

Wewe usikubaliane na mtazamo mfinyu wa JK aliempa Ukuu wa wilaya Nancy Nkui mrembo kutoka UDSM 2010 kwa personal attachments. Mi sitaki kuamini ukweli wa madai ya madaktari haujui!!!!!
 
Nchi ya Maneno.Watu Wa maneno. Maneno maneno kila raia maneno.. Mafundi kweli Wa maneno..

Kwani Maneno yanasaidia kuponya wagonjwa?. Watu wanakata roho huku ati, watu wanaotakiwa kufanyiwa operations hawajui hatma zao Na Hali zao zinazidi kudorora.. Hapa watu walioshiba ugali Na Kauzu wanapiga domo tu..

Sikilizeni enyi mbweha.. Hatutaki maneno tena, Kama mnaona madai ya madaktari ni chachu tupilieni mbali wao Na madai Yao kwenye dustbins.. Na muajiri madaktari wengine Na raia tuendelee kupata matibabu ..

Mambo ya maneno ni upuuzi .. Upuuzi mtupu, huyu namlipa sana, sijui yule kidogo, ah ni majungu tu yote hayo.. ilihali wananchi maskini ya mungu tusio Na hatia tunakwisha Kwa kukosa stahiki ya tiba..

Sina Shaka kesho wahandisi nao watalianzisha.. Mhandisi kuanza Na 420,000 Na baada ya makato anakwenda hom Na 320,000 aiseee.. Hata house-girl Wa hapa masaki wanamzidi kipato mhandisi.. Erb mpo au mnachangisha michango ya stickers tu..
Usiombe tugome sisi wahandisi, kata maji, umeme, barabara ndo usiseme!! Tengeneza maguruneti masafa marefu na mafupi basi ilimradi mjue kuna wahandisi!! ERD kichaka cha wezi upande wa professional ya uhandisi.
 
Safi sana JK kaongea kama rais hii ndio inatakiwa wakuheshimu.... Wakitaka wafanye wasipotaka waende private hospitals. Vile vile narudi ushauri wangu wa siku zote SERIKALI IJITOE KATIKA KUHUDUMIA HIZI HOSPITALI NI ITIKADI YA KIJAMAA NA ISHAPITWA NA WAKATI. BADALA YAKE IHUDUMIE MGONJWA ASIYEWEZA KUPATA HIYO HUDUMA YA AFYA.... WAKIMALIZA SHULE HAO MADAKTARI WAKATAFUTE KAZI URAIANI WAONE CHA MOTO!!!!
Those days are over ndugu yangu!! Hata marekani ameshashtuka kupeleka viwanda nje ya nchi matokeo yake wananchi wanakosa kazi, maisha yanakuwa hayaendi, watawala wanakuwa hawana amani tena, nchi unayopeleka viwanda kwa ajili ya cheap labour na production cost ndo zinapiga hatua balaa kiuchumi. Ushabiki mbaya, njaa mbaya jamani!! Ninauhakika ukija kuisoma hii post yako baada ya madhara yatakayotokea kutokana na kauli za kukatisha tamaa za kiongozi mkuu wa nchi, ujiuliza mara mbili mbili.
 
Back
Top Bottom