JK katika Mazishi ya Rwegasira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK katika Mazishi ya Rwegasira

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bibikuku, Apr 6, 2011.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Aprili 6, 2011, ameungana na mamia ya waombolezaji katika kumzika Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania (TRAWU) Bwana Sylvester Raphael Rwegasira yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.

  Rwegasira aliyekuwa na umri wa miaka 52 alifariki dunia ghafla asubuhi ya Jumatatu wiki hii kwenye Hospitali ya Dar Group alikokuwa amekimbiziwa kutokana na matatizo ya ugonjwa wa moyo.

  Pamoja na Rais Kikwete kwenye mazishi hayo walikuwa ni viongozi wa Serikali kutoka Wizara za Uchukuzi, na Kazi na Ajira na viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini.

  Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Kazi na Ajira, Mheshimiwa Gaudencia Kabaka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira, Bwana Erick Shitindi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bwana Omari Chambo.

  Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wameongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa TRAWU, Bwana Bakari Kiswala na Mwenyekiti wa Taifa wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Bwana Omari Ayubu.

  Akizungumza kwa ufupi sana katika mazishi hayo baada ya kuwa ameombwa na Bwana Kiswala, Mheshimiwa Rais Kikwete ametoa pole kwa familia ya marehemu, kwa watumishi wenzake katika sekta ya usafirishaji wa reli na kwa TUCTA akisema kuwa marehemu alikuwa mtetezi wa kweli kweli wa wafanyakazi nchini.

  “Poleni nyote kwa msiba huu mkubwa. Napenda kuwahakikishieni kuwa msiba wenu ni msiba wetu pia,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

  “ Najua fika kuwa huu ni wakati mgumu kwa familia, lakini vile vile ni wakati wa subira na uvumilivu kwa sababu kila binadamu lazima apitie katika njia hiyo. Kama kuna jambo ambalo kila mmoja wetu ana uhakika nalo basi ni kufikiwa na mauti.”

  Wakati msiba huo ulipotokea Rais Kikwete alituma salamu za rambirambi kwa familia ya Marehemu Rwegasira kupitia kwa Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Omar Nundu ambako alimwelezea marehemu kama kiongozi shupavu na mtetezi asiyeyumba wa haki za wafanyakazi.

  Rais Kikwete alikuwa amepanga kukutana na kuzungumza na viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini kuhusu masuala mbalimbali kuhusiana na haki za wafanyakazi leo, Jumatano, Aprili 6, lakini Rais aliahirisha kikao hicho kufuatia msiba huo. Kikao hicho kitafanyika baadaye.

  Mwisho.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.

  06 Aprili, 2011
   
 2. koo

  koo JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mnafiki mkuba huyo anajidai kusikitika wakati ndiye alikua mpinzani mkubwa wa mpiganaji wetu
   
 3. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Unafiki haulipi, ni sawa na mbio za panya sakafuni. Tangu aingie madarakani amehudhuria misiba mingapi..... Nadhani atakuwa amweka rekodi ya marais wote kwa kuhudhuria misiba.

  Mimimnadhani Waziri angetosha sana kumwakilisha akendelea na mambo mengine.
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  Upinzani hauna maana msizikane, unafikiri Mbowe, Slaa na kususia kwao hata hotuba ya Rais na ikitokea Kikwete akitangulia mbele ya haki, Allah ampe umri mrefu, Mbowe na Slaa watasusia kumzika?

  Upinzani ni hapa duniani tu, ndio tunajidai, na kutamba, na kususa, na kejeli, tukisha iaga hii dunia hakuna cha upinzani.

  Mnafik mkubwa ni wewe usiyeyajuwa haya.
   
 5. M

  MENDE JEURI Senior Member

  #5
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 181
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mnaanza kupotoka sasa kwa kupoteza maana ya utu
   
 6. B

  Blessing JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakweli Mnafiki Mkubwa sana. HAPENDI MTU HUYO. Rais kani huyo !!! Yani atumtaki kabisa huyo anatutia kichefuchefu. Hana toa Hotuba gani wakati he was against him because ya UFISADI zao.

  Hoooooooo !!!! Kikwete uoni hata aibu !!!! Usikute mmemtoa kafara mzee ya watu.
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa mnafiki sana tena mkubwa amemsumbua sana kwenye suala la trc kulipwa stahiki zao....ili waanze upya mkataba baada rites kuondoka!!!amewapiga mkwara sana sana....nahisi aatafurahi zaidi....Mgaya....maana nae hampendi personal sio sababu ya kazi yake!!mnafiki mkubwa
   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  Hivi, wewe wa nchi gani? hata kiswahili kinakupiga chenga!
   
 9. only83

  only83 JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ....Kweli rais wetu ana matatizo fulani....leo akiwa kwenye msiba wa marehemu Rwegasira na akatakiwa kutoa salamu za rambirambi nimeshuhudia TABASAMU la nguvu.....mpaka watu tuliokuwa nao tukiangalia taarifa ya habari kupitia TBC1 kupandwa na hasira.....Huyu jamaa hajui wapi panatakiwa TABASAMU na wapi tunatakiwa kuonyesha HUZUNI....Au kuna ishu nyuma ya pazia?

  source:TBC1 news Bulletin
   
 10. m

  mohermes Senior Member

  #10
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  m mwenyewe nimeshangaa.Ndo nimeamjni ule usemi alousema khs tabasamu lake..
   
 11. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mbona kawaida yake huyu kwani hata wakati wa msiba wa mzee wetu Rashi Kawawa alikuwa anacheka cheka tu msibatu he iz not serious kbs ni wakuonea huruma!!!
   
 12. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mtoto umleavyo ndivyo anavyo .... ..... ..... .
   
 13. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Boflo?!
   
 14. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,493
  Likes Received: 1,223
  Trophy Points: 280
  I believe kuna mkono wa mtu kifo cha huyu RWEGASIRA
   
 15. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  mhhh kwa wanaongalia kennedy blog tanzania nadhani ataiweka kesho manake huwa anarekodi news ndio hapo ntakuwa na la kusema kama kweli alitabasamu.
   
 16. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35

  Sidhani kama kuna mkono wa mtu ktk hili.Mi naamini kabisa kuwa ni mapenzi ya Mungu.Muda wake wa kutangulia mbele ya haki ulifika kama ulivyofika kwa wengine waliotangulia.
  Pia jamani wana JF wakati mwingine tunamuonea rais wetu kwa kumlaumu sana kwa kila jambo analofanya.Mi nadhani ni jambo jema kwa rais wetu kuhudhuria misiba na kutoa rambi rambi kama raia wengine.Yeye pia ni binadamu na ana hisia kama zetu hivyo kumwita mnafiki kwa kuhudhuria misiba na kumtaka aendelee na shughuli nyingine kama vile hamna kilichotokea ni kumuonea kabisa.
  Wakati milipuko ya Gongo la mboto ilipotokea naye akasafiri baadhi ya wana JF walipondea uamuzi wake wa kuondoka wakati kuna maafa yametokea.Lakini leo hii baadhi yetu tunamuita mnafiki kwa kuhudhuria msiba.Tunataka afanye nini jamani ili tumkubali kuwa anatujali?
  Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Rwegasira angelikuwa KAKA yangu, si NAWAFUKUZA ADUI zake wote wasifike kwenye MAZISHI.............

  Kama mtu nilikuwa sipendani naye nikiwa mzima, NIKIFA basi wala asinuse kwenye Mazishi yangu.........

  Ndugu zangu wakimruhusu, siku wakifika mbele ya haki, ni MAKONZI tu.
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  misiba mingapi amehudhuria bila waraka kwa umma??

  sipendi unafiki wala marketing at the expense of marehemeu!!
   
 19. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #19
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ni kweli hata kama ni maadui lakini utu ni kitu muhimu sana kwa hilo jk nampongeza
   
 20. c

  chetuntu R I P

  #20
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama kawaida yako mkuu
   
Loading...