Sidhani kama kuna mkono wa mtu ktk hili.Mi naamini kabisa kuwa ni mapenzi ya Mungu.Muda wake wa kutangulia mbele ya haki ulifika kama ulivyofika kwa wengine waliotangulia.
Pia jamani wana JF wakati mwingine tunamuonea rais wetu kwa kumlaumu sana kwa kila jambo analofanya.Mi nadhani ni jambo jema kwa rais wetu kuhudhuria misiba na kutoa rambi rambi kama raia wengine.Yeye pia ni binadamu na ana hisia kama zetu hivyo kumwita mnafiki kwa kuhudhuria misiba na kumtaka aendelee na shughuli nyingine kama vile hamna kilichotokea ni kumuonea kabisa.
Wakati milipuko ya Gongo la mboto ilipotokea naye akasafiri baadhi ya wana JF walipondea uamuzi wake wa kuondoka wakati kuna maafa yametokea.Lakini leo hii baadhi yetu tunamuita mnafiki kwa kuhudhuria msiba.Tunataka afanye nini jamani ili tumkubali kuwa anatujali?
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
sheria zao lazima ahudhuria msiba la sivyo litamkuta yeye! haya habari ndiyo hiyo!