ukisema ni matusi kwa watanzania kwamba busara za kuongoza zinaanzia umri wa miaka 40 utakuwa umekosea. Je kama tukisema umri uwe ni miaka 35, wale wa chini ya 35 nao watasema ni matusi vile vile.
Kitu cha msingi hapa ni watanzania kukubaliana ni upi uwe umri wa mtu kuongembea urais. Tukishakubaliana kwenye katiba basi kila mtu atapibidi afuate hivyo.
Lakini lazima kuwa na sababu za msingi za kuchagua ni umri gani unafaa kwa mtu kuogombea urais. Kutoa tu hoja ya kuwa umri wa kugombea urais uwe miaka 35 au vipi bila sababu zenye mshiko itakuwa ni kama kupiga debe tu.
Kusuhu umri wa kupiga kura kuwa miaka 16, mimi hili napinga. Tunajua hapa tanzania mtu anatarajia kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi ya kiutu uzima anapokuwa na miaka 18. Labda tubalishile hii sheria ya jumla kwanza kuhusu umri wa mtu kufanya maamuzi ya kiutu uzima. Lakini tunajua nini itakuwa madhara yake. Umri wa miaka 16 bado ni umri wa kitoto, na inajulikana hivyo sehemu nyingi dunia.