JK: Hatutaki Rais mzee 2015

Lakini wakiamua kuondoa hilo waondoe pia ulazima wa kuwa na shahada ya kwanza kwa mgombea wa Urais! Kwanini ni lazima mtu awe na shahada kuwa rais? kwani Urais ni kazi ya usomi?

Lakini Mwanakijiji, hilo la shahada si ni la CCM tu au katiba ya jamhuri ndiyo inaelekeza hivyo?
 
Sababu za kushusha umri zimeelezwa vizuri sana na kaka yetu January Makamba. Amesema wazee wameshindwa kuleta mabadiliko na wameishia kuleta uchawi tu Ikulu. Hapo labda alikuwa anamlenga Baba Mwanaasha.
 
Sababu za kushusha umri zimeelezwa vizuri sana na kaka yetu January Makamba. Amesema wazee wameshindwa kuleta mabadiliko na wameishia kuleta uchawi tu Ikulu. Hapo labda alikuwa anamlenga Baba Mwanaasha.

Sawa,

Waelimisheni wananchi hilo basi ili wananchi wenyewe wafanye maamuzi.

Hizi habari hazina tofauti na za kuanza kusema "tunataka Spika mwaka huu awe mwanamke", kumbe nia si kupata Spika mwanamke, bali kumzuia Sitta.

Hapa napo JK anataka kumzuia Lowassa lakini anakuja na zengwe. Kam humpendi Lowassa si umblast tu? Mbona Nyerere alimblast?

Tatizo la Kikwete ni mtu spineless, hawezi kufanya kitu direct, anataka kuleta mizunguko mingi tu, sasa in the process anataka kuvunja katiba.

Nchi za watu wanaofuatilia sheria rais analazimishwa kuomba radhi kwa wazee wa nchi.
 
Sasa kama ni kweli - alisema hivyo - na anaamini hivyo kwanini yeye mwenyewe na makamu wake wasijiuzulu sasa ili kutuondolea kutawaliwa na RAis Mzee?

We are in the mess because we said the same in 2005. Tulisema rais kijana atatufaa, lakini sasa niaona ni bora tuwe na hoja za rais anayefaa kuliko rais kijana au mzee.
 
January Makamba na Zito Kabwe hawanivutii, ninawaonya leo watanzania wenzangu, itakua afadhali mlivyokosea kumteua na hatimaye kumchagua ****** kwa vigezo mlivyovitumia, kuliko majuto mtakayosababishiwa na mmoja wa vijana hawa. Hoja ya ujana ni sawa tu na hoja ya uzuri wa sura (kwa wanaouona) iliyovuma na hatimaye kutupatia mkuu wa nchi anayejumuishwa kwenye genge la uhalifu dhidi ya wananchi wake. Hivi vihoja ni hatari, na wa kulaumiwa hapa ni CCM, kipo katika hali ya kufani kinatapatapa ili angalau kiishi kitambo kidogo, kimekwisha tufanyizia hasara kubwa, tunaonekana kukipa nafasi kimalizie silaha zake kilizoziweka kwa pigo la mwisho. hawa vijana kabwe na makamba, ikiwa wanaamini ujana ndiyo suluhisho la kiuongozi kuelekea uchumi tunaouota, watuapie kwa kusema "kamwe sitagombea urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania" wawaache vijana wengine kugombea, kinyume chake hata baada ya maziko ya ccm tutashindwa kusimamia mali zetu tunavyotarajia, kikwazo kitakuwa Nyoka kijana wa ccm January ama Zitto Kabwe (mimi na makamba hatukukutania barabarani) hutaweza kuhoji mali za chenge, hutahoji ubaya wa ubinafsishaji na mamikataba mabovu ya madini, gesi, mafuta ············· eeh! kikwete alituahidi angeipitia upya mikataba ya madini kwa lengo la kuiboresha, kiko wapi? Hapo sijui mtakuja kutamani rais mtoto!!!!!! mtanzania mwenye akili timamu ndiyo sifa pekee inayo accommodate mengine mazuri yote.
 
Siasa za Tanzania ngonjera nyingi. Kama maigizo ya shule za msingi. Leo speaker anatoka na kusema wabunge ni "masikini" kesho raisi mzee anasema wazee wasi gombee uraisi. Duh!
 
Kwa hiyo jk anamaanisha kuwa kushindwa kwake kunatokana na umri wake? Sijaona bado mantiki ya kuwaondoa wazee. Kuna vijana ovyo kuliko hata yeye. Tunataka rais mwenye uwezo na sio rais kijana. Mbona nape ni kijana bana?
 
Binafsi naamini katika kutumia kigezo kinachomfanya mtu aweze kupigiwa kura kuwa Mbunge ndio hichoo hicho kitumike kumpima anayetaka kuwa Rais. Miaka 18, anajua kusoma na kuandika, hajawahi kufungwa kwa muda uliowekwa na ana akili timamu. Wananchi wataamua wenyewe hayo mambo mengine. Kama tunaruhusu watu wa miaka 18 kuwa wabunge kwanini wasiweze kuwa Rais?
 
Huyu jamaa anafikiria kutupa Rais ? Hiki ni kituko cha karne. Tutachagua raisi kwa vigezo na si umri tu
 
Wazee wa CCM nao ni raia wa Tanzania wenye haki za kikatiba za Mtanzania, sasahaoni hii kauli ni unconstitutional?

Leo tutasema hatutaki wazee kesho nani? Wachagga?

Kiranga kwani umesahau kwamba alisema anataka spika mwanamke na kuwanyima wanaume haki ya kuwa maspika na kweli tukapewa bi mkora? Kwa uwezo wake wa kufikiri its possible kwamba ameyasema hayo na believe me you baada ya kusema ***** huo huenda alishangiliwa sana sana. Inasikitisha kwa kweli kwamba kuna watu wako kwenye post za hadhi ya juu kabisa lakini yanayowatoka vinywani mwao unatamani uzibe masikio kwani ni aibu tu.
 
...Kuongoza nchi kunamshinda anaanza kufikiria wagombea Urais wa magamba 2015!!!!! Nchi ina matatizo chungu nzima hataki kuyazungumzia ila ameona umuhimu wa kuzungumzia wagombea wa 2015!!!! Kweli LAIS tunaye!!!
 
Sasa kama ni kweli - alisema hivyo - na anaamini hivyo kwanini yeye mwenyewe na makamu wake wasijiuzulu sasa ili kutuondolea kutawaliwa na RAis Mzee?

Mkuu nakumbuka mwaka kama 2010 au 2009 wakati anahutubia kongamano la vijana Rais alisema kuwa Baraza la Mawaziri atakaloliunda baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 halitakuwa na wazee. Alisema katika Baraza hilo hakutakuwa na mtu atakaye mzidi umri!
 
Uchaguzi wa 2010 umedhihirisha nini? Tusidanganyane hapa. Ukweli ni kuwa Chadema ina safari isiyo na mwisho kabla ya kuchukua urais.
Usipende kukata au kukatisha watu tamaa, Sata, rais wa sasa wa Zambia alipogombea mara ya kwanza alipata chini ya 5% ya kura zote, mara ya pili about 30%, now mara ya 3 yupo Ikulu, so chochote chaweza kutokea 2015, let's keep our fingers crossed kwamba uchaguzi utakuwa huru na wa haki
 
Wivu tu eti hataki wazee, kama yeye aligombea akiwa kijana ametufanyia nini cha maana? Na kugombea ni haki ya kila mtu na wala si kikwete atakayeamua
 
Back
Top Bottom