JK: Hatutaki Rais mzee 2015

Uchaguzi wa 2010 umedhihirisha nini? Tusidanganyane hapa. Ukweli ni kuwa Chadema ina safari isiyo na mwisho kabla ya kuchukua urais.

safari ya aina hiyo haipo kawadanganye huko facebook,kwa mtu anayejua ni wapi anaenda lazima atafika mwisho wa safari,unachotakiwa kuthibitisha hapa ni kivipi cdm imepoteza au haijui huko iendako hadi safari hiyo isiwe na mwisho.katika kujibu remember to attach with evidence....
 
Kama kweli Kikwete ametamka hivyo, nafikiri atakuwa anazungumza kama mwenyekiti wa chama na kwa niaba ya chama chake lakini kama anazungumza kama Rais wa JMT atakuwa anakiuka misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (KJMT) ambayo aliapa kuilinda na kuiheshimu.


Sifa za mtu kugombea na kuchaguliwa kuwa Rais wa JMT ziko wazi ndani ya katiba na JK hana mamlaka ya kujifinyangia sifa nyingine nje ya hizo (Ibara ya 39 ya KJMT inaweka wazi juu ya sifa hizo).
 
Sasa kama ni kweli - alisema hivyo - na anaamini hivyo kwanini yeye mwenyewe na makamu wake wasijiuzulu sasa ili kutuondolea kutawaliwa na RAis Mzee?
Mkuu ina maana hujaisoma picha tu mpaka leo? Anzia kikao cha NEC ya CCM, then kurudiwa kwa uchaguzi wa mgombea Aru meru Mash. From there you might come up with something in your mind!
 
JK huwa hajui anaongea nini?alijinadi mwaka 2005 kuwa ni kijana matokeo yake ni mautumbo matupu..yaani ni bora kuchagua rais mzee kama mugabe akawa na akili kuliko kijana mwenye kazi ya kuchekacheka na kujipaka ma carolite...
 
PIa swala la kuwa na Afya njema ni muhimu kwa rais na sio umri tu, Kwani gharama za India ni kubwa sana. pia asiwe vasco dagama , budget yetu kiduchu

Nakubaliana na wewe kuwa afya njema kwa Rais wa nchi ni muhimu hivyo wagombea hawana budi kupimwa na kujulikana wazi kuwa afya zao hazina mgogoro; lakini pia niongezee kuwa hakuna uhusianao kati ya umri wa mtu nakuwa na afya duni kwani kuna vijana wenye afya zilizozorota na vijana wenye afya njema,pia wazee wenye afya njema na wengine wenye afya zilizozorota!! Zitto na Chami walikuwa India karibuni kwa matibabu na hao ndio mnaowaita vijana!! Juu ya hayo uadilifu pia kama afya, kuna vijana wasio waadilifu na wazee waadilifu; una habari ya dollar millioni moja alizoletewa January Makamba azitumie wakati wa uchaguzi 2010 ili apite ubunge lakini azirudishe pindi angechaguliwa kuwa waziri wa nishati!! Hapo sijazungumzia ya Zitto na hongo za Dowans!!
 
JK: Hatutaki Rais mzee 2015


na Nasra Abdallah

amka2.gif
WAKATI makundi ya urais yakijipanga kuwania kiti hicho mwaka 2015, bila kuyajali, Rais Jakaya Kikwete amesema wanaota urais wakiwa na umri kama wake, wasahau, Tanzania Daima Jumatano limedokezwa.
Kikwete alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kilichokutana juzi, pamoja na mambo mengine, kupitisha jina la mgombea ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilisema kuwa Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati akifungua kikao hicho.
Kwa mujibu wa habari hizo, Rais Kikwete alisema kuwa kinachotokea Arumeru Mashariki ni makundi yanayotaka urais na kusisitiza kuwa kama kuna mtu mwenye umri kama wake na anataka urais mwaka 2015, asahau kupata kiti hicho.
Alisisitiza kuwa wanaotajwa kutaka urais wakiwa na umri kama wake na hata kuzidi, huu si wakati wao bali wa vijana.
Mtoa habari wetu kutoka ndani ya kikao hicho, alisema kauli hiyo ya Rais Kikwete iliwanyong’onyeza baadhi ya makada wanaotajwa kutaka nafasi hiyo wakiwa tayari na umri mkubwa.
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Bombuli, Januari Makamba (CCM), amependekeza kuwa umri wa kugombea urais, ushushwe kutoka miaka 40 ya sasa hadi 35.
Ushauri huo uliungwa mkono pia na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ambaye alihoji kuwa kama Uganda wameweza kwa nini Tanzania mabadiliko hayo hayawezekani.
Makamba alitoa kauli hiyo jana katika kongamano la Femina HIP la vijana walio nje ya shule, lilioandaliwa na Jukwaa la Femina, huku likiwa limebeba mada kuu ya ushiriki wa vijana katika uundwaji wa Katiba mpya na kufanyika katika Ukumbi wa British Council, jijini Dar es Salaam.
Wabunge hao wawili pia walitaka umri wa mtu kuruhusiwa kupiga kura uwe miaka 16 badala ya 18 kama ilivyo sasa.
Akifafanua pendekezo hilo, Makamba alisema Tanzania inapaswa kuiga mfano wa nchi jirani kama Uganda, Burundi na Rwanda ambao tayari wanafuata mfumo huo.
Alisema asilimia kubwa ya wananchi wa taifa hili ni vijana hivyo haoni ni kwa nini hawapewi fursa kugombea nafasi hiyo kwa kisingizio cha umri.
Kuhusu kupiga kura, mbunge huyo alisema anaamini kwamba umri wa miaka 16 alionao kijana wa karne hii ana uwezo wa kuchambua mambo na kumchagua kiongozi anayeona anafaa.
Kwa upande wake Zitto alisema hata yeye anaunga mkono hoja hiyo na kudai kwamba linawezekana kabisa huku akitolea mfano kwamba kipindi cha nyuma wanawake walikuwa hawashiriki katika kupiga kura.
Kama vile haitoshi alisema miaka ya kupiga kura ilikuwa ni kuanzia 21 lakini kadri muda ulivyozidi kwenda na kuonekana kwamba kuna haja ya sheria hiyo kufanyiwa marekebisho, ndipo ikafika miaka 18 hivyo ni wakati sasa muafaka kwa vijana kudai haki hiyo ya kupiga kura wakiwa na miaka 16.
Hata hivyo Zitto aliwataka vijana katika mchakato huu wa Katiba kutokubali mjadala huo utawaliwe na wanasiasa kwa kuwa wengi wanajadili kwa maslahi yao.
Kwa mujibu wa Zitto tayari ameshaona wanasiasa hao wameanza kuutumia mjadala huo kwa manufaa yao huku wakilenga katika kugawana madaraka na kuacha kujadili mambo muhimu kama ajira kwa vijana na namna gani wataweza kulipwa kutokana na kazi wanazozifanya.
Pia mbunge huyo aliwaonya vijana wasije wakafikiri Katiba mpya ndiyo itakuwa suluhu ya matatizo yanayowakabili na badala yake kuwataka wafanye kazi kwa bidii.
“Msidhani kwamba eti Katiba mpya ikiwepo ndipo matatizo ya ajira yatakwisha au uibwaji wa rasilimali za nchi utaisha la hasha kwani matatizo haya yanaweza kuendelea kuwepo; kinachotakiwa ni kuchapa kazi na kujenga hoja pale mambo wanapoyaona yanaenda sivyo,” alisema.
Hata hivyo wabunge hao walipoulizwa swali na mmoja wa washiriki wa kongamano hilo, Humphrey Polepole, kama wangependa kuwa kwenye Bunge Maalum la Katiba, walisema ndiyo kwa madai kwamba wanaamini watakuwa na mchango mkubwa kuwepo kwao katika tume hiyo.
Kwa pamoja wabunge hao walisema kwamba wanataka kuonyesha siasa za tofauti katika kuondoa matatizo ya vijana na wananchi kwa jumla bila kujali vyama wanavyotoka.
Katika kongamano hilo la siku mbili ambapo mgeni rasmi alikuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, linalenga kupata maoni ya vijana wa Tanzania kuhusu Katiba mpya kwani takwimu zinaonyesha kwamba Tanzania ina watu milioni 44 na kati ya hao asilimia 65 ni watu walio chini ya umri wa miaka 25.


Source: Tanzania Daima. 29/Feb/2012



Mimi nionavyo kigezo cha kupata Rais bora ni zaidi ya umri tu,ikiwa ni pamoja na busara na akili iliyotulia.Mh.akitaja umri mzee kwasasa basi, aangalie hata kwa mawaziri,wakuu wa mikoa,wakurugenzi,mabalozi na wateule wengine wa Rais kuwa kwasasa hawana sifa ya kuongoza zama hizi.Huo utakuwa ujumbe uliokuwa umebebwa na hotuba yake.
 
Watu wanaendeshwa kwa hisia na si uhalisia, tufike wakati tuheshimu mawazo ya watu kwani pindi atapotoa mawazo yake si lazima yakubalike na si lazima watu washangae kwani yeye amezungumza kama ni mtanzania mwenye haki ya kuongelea mwenendo wa taifa lake.

pia kusema rais ajaye awe kijana haina maana yeye ajiuzulu wadhifa wake kwani inawezekana kaona matatizo yanayomkuta na uwezo wake dhahifu wa kuweza kukabiliana nayo hivyo anajaribu kuweka mwanga kwa siku za usoni kwani unapojikwaa inama na utoe jiwe mwingine asije jikwaa kwenye jiwe hilo.

Umri wa kupiga kura unaweza kubaki 18 lakini umri wa kugombea urais ushuke mpaka miaka 30. ni mawazo yangu tu naruhusu mgongano wa mawazo
 
Kikwete anafikiri anaweza kuongea lolote bila kuangalia matokeo yake??hajui kwamba yeye ni publick figure??huyu mzee hajitambui kabisa!
 
rais ni taasisi nyeti na muhmu mno wanajf,kwa mawazo yangu tu madogo,suala la umri linamata sana,rais kijana hafai na rais mzee sana naye hafai,hivyo basi atleast kuanzia miaka 50-70 wapewe nafasi,
 
Kikwete hawezi kutuchagulia wananchi Rais ajaye, asitumie udhaifu wake kwamba wazee wote watakuwa na uwezo kama wake.
 
...kama aliyasema yaliyonukuliwa sisi neutrals tunamchukulia JK alikuwa anamaanisha "hatutaki mgombea uraisi mzee ccm 2015".

so, am not bothered at all by JK's comments (if he ever made them that is) because 2015 president is unlikely to come from his ccm.
 
Wazazi huyu Jua anaongea nini kwani hajui maana ya uraisi anagalia navyo watesa watanzania wananchi wamekondeana maana lishe mbovu wazazi idhaa bei ju kilasiku.....watu wanalia maisha magumu yeye anakenua meno.... hawezi kutu chagulia raisi
 
sasa naona january na zitto wamelewa sifa, wanafikiri kila wanachoongea ni sahihi. Swala la umri mkubwa ni muhimu sana katika ngazi kubwa kama ya uraisi wa nchi. tunajua matatizo ya vijana. Na kama wanataka urais si wasubiri. Na JK kama kaongea hivyo naona kachanganyikiwa. Tuache ubaguzi wa wazee na vijana ni kosa kubwa sana. na sio kitu cha kushabikia kwa sisi vijana, tukumbuke Leo kijana kesho utakuwa mzee.
 
Back
Top Bottom