JK hajui akumbukwe na kitu gani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK hajui akumbukwe na kitu gani

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Oct 30, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]Katika mdahalo wa jana JK aliulizwa swali moja zuri sana: kwamba ktk kipindi chake hiki cha miaka mitano kilichopita, anataka Watanzania wamkumbuke (legacy) kwa kitu gani?[/FONT]

  [FONT=&quot]Muungwana alitulia kama sekunde 40 hivi bila kujibu, maana anajua fika kwamba hana cha kukumbukwa. Kamera ya mtandao mmoja ikafanya ka-uchokozi kidogo, ilielekea kwa Kinana ambaye macho yalikuwa chini. Kimya kilivyokuwa sindano kama ingeanguka sakafuni ingesikika.[/FONT]

  [FONT=&quot]Baadaye akajikakamua (literally, that is) kusema kwamba anataka Watz wamkumbuke kwamba aliwatoa hapa na kuwafikisha hapa – huku akionyesha ishara kwa mikono kuonyesha sehemu moja kwenda nyingine![/FONT]

  [FONT=&quot]Duh! Jamaa hana la kukumbukwa – na anajua hivyo – sijui anataka urais wa nini tena – was matrip ya nje na kula maisha?[/FONT]

  [FONT=&quot]Lakini jibu lake lina tafsiri moja tu – ametutoa kwenye hali nzuri kwenda kwenye hali mbaya. Kutoka kilo ya sukari Sh 500/ kwenda Sh 2,000/-. Kutoka bati sh 5,000/- hadi 16,000/-, kutoka cement 6,000/- hadi sasa 13,000/-, petrol sh 800/- hadi sasa 1,700/-, ulaji wa majani badala ya nyama[/FONT]
  [FONT=&quot]etc etc etc etc etc. [/FONT]

  [FONT=&quot]Kweli muungwana katuhamisha!!!!! [/FONT]
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Lile swali halikuwa rahisi kama wengi mnavyofikiri. Mh. Kikwete ametawala kipindi ambacho kulikuwa na mdororo wa uchumi duniani. Madhara yale ya mdororo wa uchumi kwa kiasi kikubwa yamechangia sana kufuta ndoto yake ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania. Vile vile aliipokea nchi ikiwa katika hali mbaya ya ukame, madhara yake nayo yaligharimu kiasi kikubwa cha pesa ambazo zingeweza kutumika kuboresha maisha ya watanzania. Kama nchi ya Ufaransa inafikia mahali kulazimisha wafanyakazi wake wasistaafu kwa kuwa hawana pesa ya kulipa mafao ya kustaafu jee nchi kama Tanzania ambapo Vita vya Iraq vimepandisha bei ya mafuta zaidi ya mara 10, unadhani ina uwezo wa kustahimili mabadiliko yote hayo bila maisha ya mtanzania kuathirika?
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  Sikufuatilia mdahalo maana nilijua hakuna cha maana zaidi ya usanii.

  Lakini kama kuna kitu anacho Mkwere, basi ni akili ya kuangalizia.

  Hilo swali la legacy nakumbuka aliwahi kuulizwa na mwandishi mmoja wa kimataifa(sikumbuki wa chombo gani cha habari), na alijibu hivyo hivyo kama alivyofanya jana. Kuchelewa kwake kujibu alikuwa anakumbuka(kuangalizia) alichojibu kwa huyo mwandishi wa kimataifa.
   
 4. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Natofautiana na wewe kabisa.Ni swali rahisi sana, nakumbuka na wewe pia jitahidi ukumbe katika moja ya hotuba zake za kampeni akiwa Bukoba alisema."LENGO LANGU NATAKA NIKIONDOKA MADARAKANI WATANZANIA WANIKUMBUKE" Iweje akose jibu wakati tayari alishatamani kukumbukwa.it is ridiculous!!!!!
   
 5. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wewe jamaa ni useful idiot. A useful idiot is an intellectual anaetumiwa na wanasiasa kueleza mafanikio yao kielimu zaidi.
  Sadly JK hajasema hayo. Kasema mengi katelekeza. Yapi? Anajua yeye na Kinana. You just can't accept the fact that your president is failure ambae hajui sababu gani Tz ni maskini. Sijui mjinga hapa ni wewe au blind followers wa JK. Nadhani wote.
   
 6. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Akumbukwe kwa kudondoka dondoka tu inatosha kwa watanzania kumkumbuka
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Tizama hii video ya Youtube, utajua kama Kikwete amepata urais kwa bahati tu.

  Hili swali la legacy ataulizwa mwishoni-mwishoni mwa clip.

  Kwa hiyo swali la jana lilikuwa marudio kwake, lakini bado alikuwa hana jibu zaidi ya kuangalizia:

  http://http://www.youtube.com/watch?v=hCxY2otR6w8
   
 8. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  hahahhhahahahhaaa...!!!
   
 9. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Machinga Complex atakazo zijenga DAR,MWANZA
   
 10. d

  dkn Senior Member

  #10
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wana JF.

  Jana niliandika thread inayohusiana na habari ya Lowassa lakini naona moderator aliipiga chini.

  Kwa mnaokumbuka vizuri, Lowassa alikuwa kiongozi shupavu katika kazi yake ya Uwaziri mkuu na pia alikuwa na mapunguzu lakini siyo limbukeni kama JK anajua anachofanya ni mtu asiyecheka cheka na watendaji wake.

  Lowassa katika kuchagua wakuu wa mikoa, wilaya aliweka watu wake na strategy yake na baadhi ya viongozi wa juu wa CCM ilikuwa ni kumtoa JK baada ya miaka mitano ya kwanza kwani CCM ilikuwa imeshaanza kuyumba mapema na kuwepo na kambi mbalimbali.

  Watu wa karibu na JK wakamtonya kuwa angalia Lowassa mshikaji wako anataka kukufanyizia na hapo ndipo issue ya Richmond ikaanza na ukiangalia kwa undani Lowassa hakuhusika sana katika mambo yaliyokuwa technical bali kutekeleza ya JK nchi ipate umeme, mengineyo kama gharama yalishapitia kwa mkaguzi mkuu wa mahesabu na wengine wengi kabla ya Lowassa..mnaweza kuhoji mbona alikubaliana lakini mwishoni mwa siku ilibidi kuwajibika na hii ilikuwa either yeye akatae kujiuzulu na kujiosha, JK na CCM wakaona wamdanganye kuwa ajiuzulu na immediately watamshafisha na hiki hakikufanyika labda tu spika alijaribu kumsafisha.

  Sasa mkae mkijua CCM imeoza na viongozi na wakongwe, wastaafu kama kina Mkapa wanampiga chenga kwani wanajua kichwani ni SIFURI na habebeki na chama chao kiko kwenye wakati mgumu. Pia Kikwete mwenyewe anajua uozo uliopo na ndiyo maana aliwekwa chini na CC kuwa chama kimekuwa na taswira mbaya sana na itabidi abebe jukumu kwa sasa…Kikwete personally ni mtu mzuri na kama angekuwa anagombea yeye kama yeye basi idadi kubwa ya waTZ ingempa kura, sasa hawezi kusema anawatimua baadhi ya viongozi kwani wao ndiyo wamemweka madarakani…support za kifedha kutoka kwa mafisadi kama Mramba zinaenda kwenye kampeni za CCM.

  Vijana tuchague kiongozi makini kama Dr. Slaa, Prof. Lipumba tunahitaji mabadiliko sasa.
   
 11. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Nchi haina Mustakabali wake unategemea anaweza toa jambo la future.
  Nchi inaendeshwa kihohe hae haina malengo yeye kama yeye hana chakutaka kusema kuwa nataka nchi iwe imefika mahali fulani kwa haili hii eg Kielimu,Kiuchumi,Kimaendeleo, au ??

  Narudi tena kuwa Mkapa alisea ILANI ya CCM aitekelezeki na ndio maana hakuwa na jibu hapo. And this is wat vijana wengi wanaichukia CCM hakuna future strategic plan kabisa.

  IKULU is an Institution ambayo inataka watu makini ambao watamwambia Rais this is what TANZANIA wants matokeo yake wanampotezea kabisa,

  Kwa maaana nyingine usikute Rais yupo hapo ikulu kumbe anafuata matakwa ya Vigogo fulani wako CCM kama wakina kingunge na hatokuwa na watu wa kumkumbuka huyo mzeee ameshindwa kuwakalipia viongozi walio mkuta kuhusu UFISADI which mean nae alikuwa mmoja ya viongozi walikuwa against Mwl. Nyerere.

  [/FONT]
   
 12. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kwa Taaarifa yako EL alikuwa anatupiga filimeeeee hapo nakupa sasa alijifanya anajua utekelezaji huku alikuwa na malengo yake tofauti kabisa na baadhi ya viongozi huko mikoani serikalini walikuwa wanamchukia kwani alitaka kujilinganisha na sokoine kumbe yeye anauma huku anapuliza huku na ndipo RICHMOND ika mwadabisha hakujua hilo lilikuwa laja kwa kutumia kigezo cha PM,

  Kumbukeni alikuwa anawafukuza hovyo watendaji sana huko mikoani na wilayani bila kutupa reasons behind ilivyo mkuta yeye akasema ameonewa sana.

   
 13. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Sasa alisema anataka akumbukwe kwa lipi? Kutawala kipindi cha Vita vya Iraq, ukame na mdororo wa uchumi wa dunia?
   
 14. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mzee kubali au kataa, maisha bora kwa kila mtanzania yameshindikana kutokana na madhara ya vita vya iraq, ukame na mdororo wa uchumi duniani. Tatizo Benki waliwadanganya watanzania kwamba mdororo wa uchumi hauna athari kwa Tanzania. Wanaofanya kazi kwnye NGOs wanafahamu ninachosema, NGOs nyingi pesa walizoahidiwa zimesogezwa mbele kuletwa
   
 15. T

  Taso JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 459
  Trophy Points: 180
  Lilikuwa swali la kijinga.

  Mtu bado hata hajamaliza nusu ya utawala wake anaogombea kuendelea nao unamuuliza unataka kukumbukwa kwa kitu gani, ndio maana alisema anataka awatoe hapa awapeleke hapa. Hapa wapi, akimaliza mtaona!
   
 16. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  :smile-big:
   
 17. s

  shade Senior Member

  #17
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 155
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Jamani kwani hamkuona katika lile daftari lake la majibu? Maana akiulizwa swali hakuwa makini kusikiliza bali alikuwa makini kufungua majibu aloandaliwa. sasa hilo swali la legacy halikuwepo ktk kitabu cha majibu. kwakweli niliwaona kinana na makamba wakitekewa.
  Likini kwakweli mdahalo wa jana ni kama ulikuwa kati ya fideli castro na wabunge wake. maana watu walikuwa wana piga mwkofi hata pasipo stahili.
   
Loading...