JK ,EL, kitimutimu?

utu wangu

Member
May 10, 2008
52
3
Wajameni Naomba Data Kwa Mwenye Nazo Hasa Kwa Wenzetu Walio Tz.
Ni Kweli Hawa Maswahiba Wawili (jk,el)hawaivi Tena Chungu Kimoja?habari Tulizozipata Ni Kwamba Muungwana Kachoshwa Na Ubinafsi Wa Huyu Mwenzie Na Ukiukwaji Wa Makubaliano Yao Kabla Ya Kutwaa Madaraka.
Ndo Maana Akamtoa Kafara Kwenye Ishu Ya Richmond Ili Kumzima Spidi Yake.

Je Kuna Ukweli Wowote Au Ni Kiini Macho?mwenye Data Atumwagie Tafadhali.
 

Mutu

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,330
46
liesemamalo lipo...ngoja tusikie wenye data wansemaje .
Ila kulingana na mimi sioni kama EL katolewa kafara na JK kwa maana chombo kilichohusika ni bunge sio serikali.Sasa hapo I don't see the connection.
Isijekuwa ni ni taarifa za kutuosha akili kuwa JK ni antifisadi.
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,925
10,426
Siasa mchezo mchefuu.....jamani lolote linawezekanaa...hata mimi naliona kwa mbali sanaa....lawezekana...jamaa amekuwa mpole sana na hasisikiki tenaa..akifanya mchezo atapoteza ubungee...
 

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,775
2,712
Siasa mchezo mchefuu.....jamani lolote linawezekanaa...hata mimi naliona kwa mbali sanaa....lawezekana...jamaa amekuwa mpole sana na hasisikiki tenaa..akifanya mchezo atapoteza ubungee...

SKILLS4EVER hata mimi ninaiona ule ukaribu uliokuwako kabla umezimika, lakini tusubiri kusije kuwa na mtandao wa chini chini wa kiuhusiano. Kama hili lipo basi ni heri na ushindi kwa wananchi tunaoumia kwa kunyonywa waziwazi na viongozi wetu. Mungu zidi kutupatia nguvu ya kukabiliana na mafisadi hawa.
 

Silas A.K

JF-Expert Member
Apr 23, 2008
807
153
EL na JK kwasasa wanauhusiano wa kinafiki na kama habari za mwanahalisi iliyopita kuhusu kuwepo kwa kambi inayofanya kampeni Tanzania nzima ili wapate nafasi ya kugombea 2010 ni kweli basi hiyo kambi lazima itakuwa inapata ufadhili wa EL na RA. Hakuna ubishi kwamba EL ni billionare kwahiyo kufund shughuli kama hizo akishirikiana na mshirika wake RA siyo suala gumu.Ikitokea EL akitaka kugombea uongozi wa nchi 2010 hata mimi nitaingia katika kampeni ya kummaliza,nipo tayari kuacha shughuli zangu zinazonipatia kipato ili nipite nchi nzima kuwaonyesha watanzania ubaya wa huyu dhalimu. Mungu ibariki Tanzania!
 

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,229
7,890
...ni kweli hilo linasemwa hapa nyumbani...kuwa hawa wajamaa walikuwa wamekubaliana kuachiaana madaraka...na jk aliona spidi ya mwenzake ilikuwa kubwa mnu ndio maana kuna wakati walikuwa wakifukuzana ziara mikoani ..huyu akiweka mguu huyu anatoa...na ndio maana hivi karibuni wakuu wa mikoa .,wilaya ,na wakurugenzi wenye influence ya lowassa wote watamwagwa...maana inasadikiwa walikuwa na ajenda...ya kumpandisha lowassa...jk ataweka timu mpya ...

"kamba hukatikia pembamba...jk aliona njia ya kumtosa kabisa lowassa ili asijeibuka 2010..ni kumkatia...kwenye kosa linaloonekana!
 

Ben Saanane

JF-Expert Member
Jan 18, 2007
14,588
18,023
Safi sana kama utabiri utatimia.

Watanzania Ukombozi uko njiani,hawa jamaa sina huruma nao ila wasitumie raslimali zetu.Kwa kweli sina huruma nao hata kidogo!
 

Jamco_Za

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,330
192
Vita ya kunguru tijara kwa panzi. Waache wacharurane provided tunapata Mafisadi wananchi hatujali ili litakuwa zuri kwa upande wetu kulinganisha na wao maana kila mtu atataka kumchafua mwenzi na kambi yake kwahiyo wataumbuana machafu yao yote.
 

Kipanga

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
676
34
Sio mchanga wa macho jamani kweli??? Unajua waarabu wa pemba wale...Siamini sana kama JK anaweza kumuingiza mkenge EL kiaina kiasi hicho. But as usual time will tell...Let's wait and c'
 

Ben Saanane

JF-Expert Member
Jan 18, 2007
14,588
18,023
Wote hao ni wezi wa raslimali zetu tu,hatuna cha kupoteza wakiparuana wao bila resources zetu
 

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
805
nani anakumbuka urafiki wa thomas sankara na campaore huko bukina faso? ilifika mahali usalama w ataifa wakamwabia sankara kuwa vampaore anataka kukupindua yeye akajibu kuwa akitaka hakuna wa kumzuia kwa kuwa walikuwa marafiki sana,baadaye utabiri ulitimia compaore akampindua sankara tena akamuua. urafiki wa sankara na compaore ulikuwa wa bond hasa hasa tena wa kufa na kuzikana, urafiki wa EL na Jk umeanzia huko udsm na kwenye kinywaji chochote cha wezekana, kwenye siasa hakuna rafiki au adui wa kudumu. kuna tetesi kuwa EL hakushirikishwa hata kwenye mabadiliko ya kwanza kwenye baraza la mawaziri yale yaliyomngoa mshabaha pale energy ministry, kuna mtu wa ukakika anasema uhasama ukuaaanzia hapo, inasemekana EL alikuwamaafia akitanua, si unamjua? mengi yatasikika subirini
 

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
24,107
20,721
Wajameni Naomba Data Kwa Mwenye Nazo Hasa Kwa Wenzetu Walio Tz.
Ni Kweli Hawa Maswahiba Wawili (jk,el)hawaivi Tena Chungu Kimoja?habari Tulizozipata Ni Kwamba Muungwana Kachoshwa Na Ubinafsi Wa Huyu Mwenzie Na Ukiukwaji Wa Makubaliano Yao Kabla Ya Kutwaa Madaraka.
Ndo Maana Akamtoa Kafara Kwenye Ishu Ya Richmond Ili Kumzima Spidi Yake.

Je Kuna Ukweli Wowote Au Ni Kiini Macho?mwenye Data Atumwagie Tafadhali.

Who cares?
Wote ni mafisadi na their days are numbered!
 

Katibu Tarafa

JF-Expert Member
Feb 16, 2007
983
44
hakuna jipya huu ni udaku tu,tena uliokomaa.siku wakiacha kuwalipa richimonduli kidogo tunaweza kuzungumza
 

Ipole

JF-Expert Member
Apr 15, 2008
295
9
Ndugu zangu sio suala la kumtosa hilo ni kosa lake mwenyewemaana hawezi mutu akaachiwa anchota mamilioni eti kwa ajili ya uswahiba hapana EL alikuwa anakwenda mbio sana maana alikuwa anakusanya pesa za maandalizi ya uraisi lakini nawaeleza watanzania wenzangu huyo mutu hafai ana roho mbaya kama mtakumbuka wakati a;lipokuwa anafanya ziara mikoani alikuwa anawdhalilisha sana vingozi mbalimbali mbele ya wananchi akiwata wasimame na wajibu hoja papo kwa papo yeye alipotakiwa ajibu hoja bungeni akasema anajua tatizo ni uwaziri mkuu "mkuki kwa nguruwe"
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Kafara kwa issue Richmond nitakataa kabisa labda kwa jambo jingine.EL atakuwa alimua kufa kiume kumsaidia JK , Richmond ni mali ya JK na RA so EL kafara ipi tena ?Pitia data kuhusu kafara mengine naweza kukubali .
 

siWA baRAFU

Member
Apr 27, 2008
33
0
Ndugu zangu sio suala la kumtosa hilo ni kosa lake mwenyewemaana hawezi mutu akaachiwa anchota mamilioni eti kwa ajili ya uswahiba hapana EL alikuwa anakwenda mbio sana maana alikuwa anakusanya pesa za maandalizi ya uraisi lakini nawaeleza watanzania wenzangu huyo mutu hafai ana roho mbaya kama mtakumbuka wakati a;lipokuwa anafanya ziara mikoani alikuwa anawdhalilisha sana vingozi mbalimbali mbele ya wananchi akiwata wasimame na wajibu hoja papo kwa papo yeye alipotakiwa ajibu hoja bungeni akasema anajua tatizo ni uwaziri mkuu "mkuki kwa nguruwe"

Mie naona suala la kusimamisha watendaji mbele ya wananchi ni suala la kawaida tu katika utendaji..hii ni mojawapo ya technique za uongozi katika ku-promote pre-emptiveness, especially wa watendaji wa mikoa..actually maswali mengi kama hayo mwananchi wa kawaida hutakiwa kuyauliza kupitia SLP..je ni nani anajua kama wananchi hawa hujibiwa maswali na pia hoja zao? Mie kinachoniacha hoi ni huu u-busy wa viongozi wetu, ambao ukienda kwenye office zao ambapo mara nyingi makatibu mukhtasi wao hawakutambui, basi utasubiri mpaka uchanganyikiwe..kwa kweli kwa kufuata utaratibu wa kawaida, siku ambapo unaenda kuwaona hao mabwana basi siku hiyo uwe umeitoa muhanga kwa ajili ya kupoteza muda wa kusubiri..otherwise ukisema mwambie huyo jamaa kwamba ni fulani yupo nnje hapa anakusubiri, basi mara moja utaambiwa pita ndani..ama kama ni tight sana basi utapewa hata kikombe cha chai hapo usubiri.. tukirudi kwa mzee wa richmond..kasi yake ya kujijengea umaarufu ilikuwa kubwa mno..kiasi cha kuelekea kumfunika mshakaji na bosi wake pia..hivyo hiyo imetokea kama oportunity kwa mheshimiwa kuzima kasi na yeye kurudi kewani kwa gia ya kupambana na ufisadi..lakini shughuli za maendeleo ndio ivo...hakuna tena...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom