JK auza nchi kwa magaidi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK auza nchi kwa magaidi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by akashube, Oct 7, 2010.

 1. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Habari za uhakika tulizozipata masaa machache yaliyopita ni kwamba JK ameingia mkataba na nchi moja kubwa ili shirika la ujasusi la nchi hiyo liweze kumsaidia kupata ushindi kwa wizi bila kuhatarisha amani nchini. Hii ni baada ya balozi wa nchi hiyo kubwa kumpa ripoti ya kijasusi inayoonyesha kuwa bila usaidizi wa nchi hiyo nchi ni lazima itaingia kwenye vita ndani ya Mwezi Novemba.

  Katika ripoti ya shirika hilo la kijasusi imeonyesha kwamba Taasisi ya kijasusi ya Tanzania ama 'idara ya usalama' ukiondoa mkuu wake OR hawana mapenzi kabisa na JK japo kuna wenye mapenzi na CCM. Ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa ndani ya vyombo vya usalama na ulinzi ikiwemo JWTZ wana chuki kubwa na JK na wanamdharau kutokana na namna alivyoendesha nchi kwa miaka 5 iliyopita.

  Ripoti pia inaonyesha kuwa wanamtandao wa 2005 tayari wanaendesha kwa siri kubwa mchakato wa kijasusi utakaomfanya JK apate 'suprise' kwa kujikuta ameshindwa kabisa kiti cha urais japo mikakati yote ya kuchakachua matokeo imeonekana kufanikiwa. Hili ni kundi lililokuwa nyuma ya uanzishwaji wa CCJ kwa usiri na kwa kujificha.

  Ripoti imemtaja EL ambaye majuzi alisifiwa na JK na kutambulishwa kwa wapiga kura huko kaskazini mwa Tanzania kuwa ni mmoja kati ya viongozi wa mkakati huu na ambaye tayari amejiandaa kuhakikisha hata jimboni kwake tu ni yeye peke yake anayepita kwa kushinda kiti cha ubunge lakini JK katu hapiti.

  Yako mambo mengi kwenye ripoti hiyo ambayo yalimfanya JK ashindwe kutoa jibu mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya mwisho ya REDET na mwanamke mmoja BK wa REDET ambapo hii ilikuwa mara ya pili, kwani mara ya kwanza ilionyesha kuwa JK anaongoza kwa asilimia 81.3 na ndipo baada ya kuangalia upepo akawarudishia ili wairekebishe kwani Dk.alionekana kupata asilimia 6.8 tu jambo lililomfanya JK ang'ake 'wewe unataka kuniharibia wewe, ukimpa asilimia sita si itaonekana uongo wa wazi, kabadilisheni haraka'

  Safari hii ilipoletwa alikuwa tayari ameshachanganywa na ripoti ya shirika lile la ujasusi na hivyo baada ya kumgandisha kwa muda mrefu mama huyo ambaye inasemekana ni girlfriend wake wa muda mrefu na ameshaahidiwa ukatibu mkuu wa wizara ya elimu, JK alimwambia tu 'haya kaitoeni' bila kuiangalia kiundani.

  Habari zinasema kuwa nchi hiyo kubwa ina uchu mkubwa wa madini yetu ya Uranium na haiko tayari kuona nchi nyingine yeyote inayakamata. Hivyo tayari wamekwisha sambaza NGO zao sehemu kubwa ya Tanzania wakijifanya kushughulikia HIV, kumbe wanafanya ujasusi kuhusu rasilimali zetu. Hawa ni magaidi ambao hupenda kuita nchi nyingine magaidi huku wakiwaibia rasilimali zao.

  Hivi sasa wameleta na wanaendelea kuleta majasusi wa shirika lao japo wana utaifa wa nchi mbalimbali kama waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi huu ikiwa ni moja kati ya mkakati wa shirika hilo la ujasusi kuhakikisha linatimiza makubaliano ya mkataba, yaani kazi imeanza. Hivyo hata uchaguzi uchakachuliwe mpaka mtoto mchanga mwenyewe aone waziwazi kuwa umechakachuliwa bado waangalizi hao watasema ulikuwa huru na wa haki.

  Hivi sasa shughuli za saidia JK ashinde zimeanza pole pole kuchukuliwa na shirika hilo kutoka kwa mtandao mpya wa JK unaoongozwa na RK, na shughuli za kampeni zinazoongozwa na AK. 'we are taking over from here gentlemen' wanasema majasusi hao.

  Katika mitambo yetu tumenasa mazungumzo ya ndani ya shirika hilo la ujasusi na inavyoonekana lengo kubwa siyo Uranium peke yake bali ni kufanya undumilakuwili(double crossing) kwa kusaidia JK halafu mlango wa nyuma maadui zake ili kuliingiza taifa hili kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Inasemekana kuwa nchi hiyo imefanya ujasusi wa kutosha wa kiuchumi na kugundua kuwa nchi yao itafaidika sana kama Tanzania ikiwa vitani kuliko hali ikiwa ya amani. Wanahitaji Uranium lakini baadaye wanataka waipate kwa njia za panya, halafu wauze silaha na mengineyo.

  Nchi hii kubwa inaamini kuwa hakuna biashara inayolipa duniani kama vita. Lakini hawakubali asilani vita kwenye ardhi yao.

  Mtaji wao mkubwa kutokana na habari za uhakika kutokwa kwa mmoja wa makatibu wa kwanza wa ubalozi huo ni kwa uchakachuaji wa matokeo.

  WATANZANIA TUAMKE, JWTZ, TISS NA WENGINEO KUMBE SIYO WALINZI KWENYE UCHAGUZI HUU BALI NDIO WATAKAO TUMIWA NA NCHI HII KUBWA KULETA MACHAFUKO NCHINI. HAITAKUWA VITA KATI YA WANANCHI NA WANANCHI, ITAKUWA VITA KATI YA JWTZ A NA JWTZ B LAKINI WATAKAOUMIA NI WANANCHI WA TANZANIA KWA FAIDA YA WAGENI.

  KAMA UNAIPENDA NCHI HII, ZUIA UCHAKACHUAJI WA MATOKEO AMBAO UMESHAANZA KWA MATOKEO YA TAFITI ZA KISHENZI. VINGINEVYO MUDA SI MREFU........ TANZANIA PIA TUTAITWA NCHI YA KIGAIDI, HUKU JAMAA WAKIBEBA URANIUM, TANZANITE, DHAHABU, ALMASI, WANYAMA WETU, HALAFU HAWATOKI NG'O WAKIDAI KULINDA AMANI MPAKA WAMALIZE KABISA KWA FAIDA YA NCHI ZAO.

  JAMANI EBU TUKUBALI MABADILIKO, TUKUBALI SAUTI YA UMMA, VINGINEVYO TUTAJUTA.
   
 2. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Kama wewe umeipata hiyo ripoti basi sio siri tena.
   
 3. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mkuu.. ukiweza kuweka wazi ni nchi gani ni sawa, ila mi naona kama hii habari yahitaji kupata more particulars yaani kama tunazungumzia USA, Mossad, Iranian inteligence services etc. NI vyema ukaiweka wazi ili tuweze kupima unayoyasema. Asante
   
 4. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Jambo la kushtua likishamfikia JK haliwi siri tena. Waulize SS.
   
 5. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hizo data nyeti tunaomba zipelekwe sehemu zinazohusika ili ziwe analyised na kushughulikiwa ipasavyo. Nikisoma kati ya mistari, nimeweza kujua ni nchi gani na ndio maana wanamwaia sifa kem kem utawala huu hata kama kila mtu anaelewa kuna uongozi mbovu. Hata hivyo najua nchi hiyo ikiumbuliwa mapema tutaweza kuepuka na shida hiyo, kwa vile wanapenda kuonekana kuwa ndio mabingwa wa demokrasia. Habari hii inanikumbusha nchi kama Congo na Angola ambazo rasilimali zao, badala ya kuwa neema ziligeuka kuwa laana kwa wananchi. Lakini viongozi wenye uchu wakumbuke yaliyowakuta marehemu Savimbi na Mobutu. Pale nguvu za wananchi zilipowazidi, rafiki yao huyo mkubwa aliwakana na kuwaacha solemba. Savimbi alipigwa risasi vichakani na Mobutu alifia Morocco baada ya nchi nyingi kumzuia asiingie humo. Ole wao!
   
 6. Kionambele

  Kionambele JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa naona Iran utawasingizia ikiwa umesoma vizuri hapo juu. halafu mossad ni waisraeli na hawana uhusiano kabisa na nchi hii. labda marekani. siku hizi redio mbao haziongopi. hata redet ilisemwa humu tangu wiki iliyopita na tumewaona leo.
   
 7. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 670
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  Samahani mkuu hii post yako looks like one of the fabricated stories!!! Nachelea sana kuamini ulichoandika! Ni hisia zangu tu lakini!
   
 8. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mimi hizi taarifa nyeti 'zauhakika' zinazoletwa hapa jamvini kila kukicha nazitilia shaka.
   
 9. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hizi habari za kutisha tisha sasa zimekuwa too much. Watu mmeona JF wanachangamkia sana habari hizi basi kila mtu anaibuka nayo tu. Hebu acheni kututia mchecheto usiokuwa na maana bwana!!
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,899
  Likes Received: 12,035
  Trophy Points: 280
  Tuko pamoja siku hizi watu wanajitungia story na kuzileta JF kupima upepo.
   
 11. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Eti eh? Lkn tusipuuze kama kuna chembe ya ukweli it is interesting. Mi hiyo angle ya REDET ndo nimecheka sana. Kumbe mgombea wao pia anajua uongo ukipitiliza anakuwa kituko? Alichokosea ni kuwa hata hiyo 71% ni kichekesho!
  Alafu mkuu hiyo avatar yako huwa nikiiona natabasamu sana...
   
 12. P

  Percival JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,567
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Mungu ijaalie Tanzania amani, utulivu, haki, maendeleo mazuri, afya njema kwa watu, upendano na heshima kwa sheria. iepushe na majanga na chuki baina ya watu wake. Amin
   
 13. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  hii habari ina walakini, inaonekana mtu katunga tu kupima upepo wetu hapa JF.
   
 14. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  mhhhhhhhhhh
   
 15. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,899
  Likes Received: 12,035
  Trophy Points: 280
  Ingawa nina muda mfupi nimejiunga JF lakini huwa nasoma post nyingi sana kwa siku kiasi mtu akileta post ya jokes, mzaha, ya kweli, ya kupima upepo, ni rahisi kuijua.
  Hii avatar nimeiweka makusudi kunikumbusha kila siku kuwapigia simu jamaa zangu wasisahau siku ya kupiga kura kuwa jamaa ni mahututi.
   
 16. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hii habari imekaa ki-Mtikila lakini inabidi ichakachuliwe kidogo walau ifanane na ukweli.
   
 17. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,009
  Trophy Points: 280
  Kila nikijitahidi kumeza hii report haimezeki, najihisi kama vile nna matatizo.
   
 18. Wun

  Wun JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2010
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 353
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hahaaa kazi kweli kweli JF siku hizi imekuwa kama baraza za kahawa pale kariakoo na magomeni.
   
 19. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #19
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  No comment
   
 20. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,375
  Likes Received: 19,621
  Trophy Points: 280
  JF ni sehemu ambayo hata magazeti yote ya bongo wanakuja kuchukua news hapa. Hii taarifa sipingani nayo hata kidogo kwani mengi ambayo yamesemwa hapa yamekuja kuoneka kuwa ni ya ukweli anzia na redet.Marekani wanajipenda wenyewe tu basi hakuna kitu kingine angalia iraq,kongo,angola. Wamarekani wapo huko hata urusi ana rasilimali nyingi lakini kamwe hataki kusikia kitu USA
   
Loading...