Sinamatata
Member
- Jan 14, 2011
- 23
- 0
Natamani Mh. Dr. Slaa achukue nchi ili awe rais wa kwanza kutosafiri nje ya nchi, awe rais asiyeomba msaada nje ya nchi, asiyekopa, hakutakuwa na rushwa, mahosipitali yote yatajaa dawa na vifaa, shule zitakuwa na madawati bila kuchangisha wafanyabiashara na wananchi, hakutakuwa na wakwepa kodi, machinga hawatalipa kodi na watafanyia umachinga popote wanapotaka hata kama ni katikati ya barabara na airport, kariakoo igeuke taipei, mfumuko wa bei soko la dunia hautaikumba nchi yetu nzuri, madini tutachimba wenyewe bila kutegemea nchi au makampuni ya kilaghai, vijana tutakua huru kuandamana kufurahia au kulaani jambo bila kuhitaji polisi. Polisi na majeshi yatakuwa katika hali nzuri, mabomuu hayatalipuka hata kwa bahati mbaya/ajali, umeme utawafikia watu wote ndani ya miaka mitano nk.
Ndugu yangu haya ni mawazo ngando!!!!