JK apaa kwenda Paris leo...

JK apaa kwenda Paris leo...

Natamani Mh. Dr. Slaa achukue nchi ili awe rais wa kwanza kutosafiri nje ya nchi, awe rais asiyeomba msaada nje ya nchi, asiyekopa, hakutakuwa na rushwa, mahosipitali yote yatajaa dawa na vifaa, shule zitakuwa na madawati bila kuchangisha wafanyabiashara na wananchi, hakutakuwa na wakwepa kodi, machinga hawatalipa kodi na watafanyia umachinga popote wanapotaka hata kama ni katikati ya barabara na airport, kariakoo igeuke taipei, mfumuko wa bei soko la dunia hautaikumba nchi yetu nzuri, madini tutachimba wenyewe bila kutegemea nchi au makampuni ya kilaghai, vijana tutakua huru kuandamana kufurahia au kulaani jambo bila kuhitaji polisi. Polisi na majeshi yatakuwa katika hali nzuri, mabomuu hayatalipuka hata kwa bahati mbaya/ajali, umeme utawafikia watu wote ndani ya miaka mitano nk.

Hivi kwa akili zako unadhani watu wanalalamika Kikwete kusafiri au wanakerwa na uzururaji wake huko nje?Na kwa busara zako unadhani watu hawataki akatembeze bakuli huko nje au wanapinga uzururaji kwa kisingizio cha kusaka misaada ilhali tuna ministers,na ambassadors wanaolipwa kufanya kazi hiyo?Au unadhani watu wanapinga kuomba misaada pale inapohitajika au wanapinga misaada hiyo kuishia kwenye matumizi ya anasa kuzidi ya hao tunaowaomba misaada,leave alone misaada hiyo kuishia mifukoni mwa mafisadi?

Na kwa akili yako unadhani tunamlaumu JK kwa kila tatizo kwa vile tunamwonea au tunamlaumu kwa vile ufumbuzi wa matatizo huo upo lkn aidha hajui kwanini aliomba kuwa rais au yuko madarakani kwa maslahi ya mafisadi?Kwa akili yako finyu inakuingia akilini kuona wanafunzi shule za msingi wanakaa sakafuni,zahanati hazina dawa,mabomba yamekauka maji,nk lakini mbunge anapewa shs milioni tisini (licha ya marupurupu lukuki aliyonayo)?Na ili akili yako finyu ielewe,ni muhimu uzidishe shs 90,000,000xwabunge 323!

Na kwa akili yako yenye uwezo duni wa kufikiri unadhani watu wanamlaumu jk kuhusu milipuko kwa vile wana chuki nae binafsi au wanamlaumu kwa kushindwa kwake kuwawajibisha waliohusika na milipuko ya kwanza Mbagala na hatimaye wazembe haohao wamepelekea milipuko mingine huko Gongo la Mboto,iliyoua watu wengi zaidi ya ktk tukio la awali?

Ufisadi umezaa tatizo kubwa zaidi ya athari zake kiuchumi.Umezaa tatizo la kisaikolojia.Kwa upande mmoja ni watu waliofikia mahala pa kuamini kuwa manyanyaso na makandamizo ya kifisadi dhidi yao ni destiny yao.Kwa upande mwingine ni reproduction ya wazembe wa kufikiri wanaoishi ktk fantasy land in which nao wanajiona mafisadi (fedha kibao,nyumba ndogo lukuki,gari za thamani,mahekalu ya thamani ya kufa mtu,kuimbwa na akina twanga pepeta na kumwaga noti feki kwa wasanii wanaosifia,kuitwa pedejee,na upuuzi mwingine km huo).Hizi wishful thinking za kifisadi zinamsaidia sana kikwete kupata ana army of silly supporters like wewe.

Get a life,sucker!
 
Akirudi utaambiwa kuwa alikwenda kuhudhuria kikao cha kumuwekea Gaddafi vikwazo....teeh teeeh teeeh.
 
Jamani hata akienda kutibiwa aage? si mnajua anaumwa.
 
Hivi huyu mtu akili zipo ama ameziazima mahala... hivi yote haya hasikii??? Chadema sitisheni maandamano yote mikoani mambo Dar tujichukulie nchi yetu kwa mwendo wa kiulani. Kila mtu achukue chake pam&&**%^#$ Hachoki kutembea alilogwa au ni ulimbukeni.
 
....baada ya kuongea pumba za jana ..tuko hapa airport ..tunaona JK Anaondoka kwenda nje ya nchi ...anaagana na viongozi wote wakuu pale...sijui kwa nini safari hii kimya kimya......

Kaenda kumsalimia freemason mwenzie!
 
Hili dude linafaa sana kuwa lihudumu na ndege halina hata moyo wa huruma kwa wanachi wake!!!
 
naona pumba nyingi mno. wakati mwingine naona kupoteza muda kuchangia mada janvini. nakosa serious discussions
 
....baada ya kuongea pumba za jana ..tuko hapa airport ..tunaona JK Anaondoka kwenda nje ya nchi ...anaagana na viongozi wote wakuu pale...sijui kwa nini safari hii kimya kimya......

Nadhani hiyo kwetu watanzania ni additional ya matusi aliyotutukana jana. Maisha magumu-serikali imejizatiti, tatizo la umeme-litaisha hivi karibuni.....na blah bla kibao...Baada ya hapo anapanda zake pipa kuelekea jiji la starehe. Jamaica alikuwa anabembea na kuchezea vigari nadhani Paris atapanda Eiffel Tower kula starehe. Watanzania tutatukanwa hadi lini?
 
mhesh rais wetu, tafadhali tulia nchini uangalie matatizo ya wananchi wako. inakera sana, misafara yako ina misururu ya watu wanaotumbua kodi ya watanzania. kwani miaka kumi ya uwaziri wa mambo ya nje haikutosha? tunashauri u-delegate baadhi ya safari na uache mabalozi wafanye kazi zao na ikiwezekana mwachie waziri wa mambo ya nje afanye kazi hizo.
 
Jakaya Kikwete ameondoka tena nchini jana kuelekea Paris, Ufaransa, kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa kimataifa wa Tansnia ya Uzinduaji (Global Extractive Industries Transparency Initiative -EITI). Katika mkutano huo unaoanza leo, Rais Kikwete anatarajiwa kutoa mada juu ya umuhimu wa shughuli za uziduaji na uwazi katika mapato ya madini. Baada ya kumaliza mkutano huo wa Paris, Ufaransa, Rais Kikwete atasafiri kuelekea Noukchott, Mauritania kwa ajili ya kikao cha marais wa Afrika wanaotafuta suluhisho la tatizo la kisiasa nchini Ivory Coast.


jana kasema yuko busy na kutatua matatizo yetu......labda anaenda nje kupata hewa nzuri iliaweze kutulia vizuri kutatua matatizo yetu
 
Mzee protocal ya rais wa Tanzania anapoenda nje ya nchi ..huwa anasindikizwa na waziri mkuu na makamu...[kama wapo mjini] au na viongozi wa ulinzi na usalama ....ukiona kati ya hao yupo kumuaga basi ujuwe mkuu anaenda nje.....kama anaenda mikoani huwa yeye na walinzi wake tu!!..hope umeelewa mambo yanavyokuwa....

MARA ZOTE akisafiri idara ya mawasiliano IKULU hutoa taarifa ya vyombo vya habari ...kipindi hiki kimya...sijui anaogopa nini?? anafikiri waandamanaji wakijua hayupo wataenda kukalia IKULU?? AU anaogopa wafanyakazi na wanajeshi ambao mishahara inasuasua ..wataziba anga asirudi........mwaka huu kazi ipo.

Hata kama ni kutibiwa idara ya mawasiliano na daktari wake huwajibika kutoa taarifa.....hivi huyu ataweza kukaa nje miezi mitatu kwa matibabu kama mkapa alivyokaa SWITZERLAND na nchi ikawa inaenda?????....mkapa hakuwa na wasiwasi kwa kuwa hazina yake ilikuwa na pesa za kutosha kuendesha nchi hata kwa miezi 10 bila kutetereka.....sasa hivi kila kitu mpaka kungoja kodi ya ikusanywe ...hakuna akiba!!

Idara ya mawasiliano IKULU imetoa taarifa kwa vyombo vya habari

Taarufa Kwa Vyombo Vya Habari - Rais Kikwete Kushiriki Mkutano wa EITI Paris, Ufaransa

Rais Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kutoa mada juu ya umuhimu wa shughuli za uziduaji na uwazi katika mapato ya madini katika mkutano wa Kimataifa wa Tasnia ya Uziduaji, (Global Extractive Industries Transparency Initiative -EITI), ambayo ina malengo ya kuongeza uwazi na uwajibikaji katika mapato yatokanayo na uchimbaji wa madini, mafuta na gesi asilia.

Mkutano huo wa siku mbili unaanza kesho, Jumanne, Machi 2, 2011 jijini Paris, Ufaransa, na Rais Kikwete anaondoka nchini leo asubuhi kwenda kuhudhuria mkutano huo.

Tanzania iliomba na kupewa uanachama wa muda wa EITI tangu mwaka 2009. Tanzania itaweza kupata uanachama kamili baada ya kuwa imekamilisha na kutimiza vigezo vya kuwa mwanachama kamili na kuweka misingi ya utoaji taarifa hizo muhimu kwa umma juu ya malipo ya kodi kutoka makampuni mbalimbali yaliyopo nchini.

Lengo kuu la kujiunga na EITI ni kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia kwa kutangaza hadharani malipo yanayotokana na rasilimali zake kwa manufaa ya wananchi wake.

Utaratibu huu utaweka uwazi na kuondoa usiri ambao unaweza kuwa mwanya wa kuficha mapato halisi ya makampuni husika.

Baada ya kumaliza mkutano huo wa Paris, Ufaransa, Rais Kikwete atasafiri kwenda moja kwa moja Nouakchott, Mauritania kwa ajili ya kikao cha marais wa Afrika wanaotafuta suluhisho la tatizo la kisiasa katika Ivory Coast.

Katika Mauritania, Rais Kikwete atajiunga na marais wa Mauritania, Afrika Kusini, Burkina Faso, Chad, Nigeria na Equatorial Guinea pamoja na wawakilishi wa Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Balozi Jean Ping na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN).

Katika kikao hicho, viongozi hao watafikia uamuzi wa AU kuhusu mzozo huo na kupendekeza namna gani ya kuutatua mzozo huo uliolipuka kufuatia raundi ya pili ya upigaji kura katika Uchaguzi Mkuu wa Ivory Coast Novemba 28, mwaka jana, 2010.

Matokeo yake, nchi hiyo imegawanyika katika sehemu mbili, moja ikimuunga mkono aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo, Mheshimiwa Alassane Quattara na nyingine ikimuunga mkono Rais aliyekuwa anatetea kiti chake katika uchaguzi huo, Mheshimiwa Laurent Gbagbo.

Kila mmoja kati ya wanasiasa hao amejitangaza kuwa Rais na kila mmoja ameunda na kutangaza Serikali katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Wiki iliyopita, viongozi hao wa Afrika walikutana mjini Nouakchott na baadaye wakaenda Abidjan, Ivory Coast ambako walikutana na viongozi hao wawili nchini humo katika jaribio la kutafuta suluhisho la mzozo huo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM

Ikulu Mawasiliano: Taarufa Kwa Vyombo Vya Habari - Rais Kikwete Kushiriki Mkutano wa EITI Paris, Ufaransa
 
Kikwete to present paper at EITI meeting today

President Jakaya Kikwete is expected to present a paper on the importance of mining and transparency on mineral revenue during a Global Extractive Industries Transparency Initiative (EITI) meeting which takes place in Paris, France from today.

According to a statement from Presidential Information Directorate, the President left the country yesterday and will attend this two days meeting which aims at increasing transparency and encouraging accountability on resources that result from minerals, natural gas and oil mining.

Tanzania applied to be given an EITI membership in 2009 and was given a temporary membership until it meets all membership requirements which include putting down structures that will ease the process of tracking down revenue from mining industries in the country.

The EITI sets a global standard for companies to publish what they pay and for governments to disclose what they receive. Its implementation is likely to lead to more transparency over the revenues generated by the mining sector in Tanzania, where several key aspects of the mining industry have been shrouded in secrecy.

Through EITI the Tanzanian people will be better informed about revenues generated by the mining sector – both where that money comes from and where it is being spent. The revenue should benefit the public.

The statement also indicated that after the Paris meeting, President Kikwete will go straight to Nouakchott, Mauritania to attend a meeting of Presidents from African countries who are seeking for peace deal in Ivory Coast

In Mauritania, President Kikwete will join Presidents from Mauritania, South Africa, Burkina Faso, Chad, Nigeria and Equatorial Guinea. Representatives from the Economic Community of West African States (ECOWAS), Chairman of African Union (AU) Commission, Ambassador Jean Ping and United Nations (UN) representatives will be present.

These leaders are expected to come up with AU resolutions on the crisis and give recommendations on how to resolve the post-elections political crisis in Ivory Coast.

The Ivory Coast's internationally recognized election winner Alassane Ouattara and the incumbent President who refused to step down after losing in the general elections, Laurent Gbagbo, met African leaders last week on a new mission to mediate rival claims for the presidency amid a surge in deadly clashes. Post-electoral violence in that country has claimed at least 300 lives since mid-December, according to the United Nations.

Kikwete to present paper at EITI meeting today - Newhabari
 
Back
Top Bottom