JK aomba walimu toka Jamaica

JK aomba walimu toka Jamaica

Kashishi

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2010
Posts
1,147
Reaction score
641
JK aomba walimu toka Jamaica

Na Mwandishi wetu
Jumatano 29 Mei, 2013

RAIS Jakaya Kikwete ameomba msaada wa walimu wa Hisabati na Sayansi kutoka nchini Jamaica ili kukabiliana na upungufu wa wataalam hao nchini.

Rais Kikwete alitoa ombi hilo juzi kwenye Hotel ya Sheraton mjini Addis Ababa, Ethiopia wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa Jamaica, Mama Portia Simpson Miller.

Ikulu ilisema kuwa Rais Kikwete alikuwa Addis Ababa kuhudhuria sherehe za miaka 50 tokea kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika, Juni 25, 1963 na Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa AU wakati Mama Simpson Miller alipokuwa mmoja wa viongozi mashuhuri wa nchi mbali mbali duniani walioalikwa kuhudhuria sherehe hizo.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyosambazwa jana kwa vyombo vya habari, ilisema kuwa katika mazungumzo ya viongozi hao wawili, Mama Portia Simpson Miller ambaye aliapishwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamaica Januari 5, 2012 baada ya chama chake cha Peoples National Party (PNP) kushinda uchaguzi mkuu nchini humo, alimwuliza Rais Kikwete jinsi gani Jamaica inavyoweza kuisaidia Tanzania.

Kutokana na swali hilo, Rais Kikwete aliomba mambo mawili, mosi kupatiwa walimu wa masomo ya hisabati na sayansi pamoja na kocha wa riadha.
“Mawili makubwa ambayo mnaweza kutusaidia, moja ni walimu wa hisabati na masomo ya sayansi kama mnao wa kutosha na pia kocha wa riadha ili tuweze kufufua upya mchezo huo ambao Tanzania ilikuwa inatamba nao duniani katika miaka ya 1970,” alisema Rais Kikwete.
Kutokana na ombi hilo, mama huyo alimwahidi Rais Kikwete kuwa Jamaica ina uwezo wa kusaidia katika maeneo yote mawili.

“Hili la walimu tutaliangalia mara moja nikirejea nyumbani. Tutasaidia kwa kadri inavyowezekana kwa sababu najua fika juhudi zako kubwa ambazo umekuwa unafanya katika eneo hili la elimu na mafanikio makubwa ya jitihada zako.”

Kutokana na makubaliano hayo, serikali sasa inatarajiwa kupata walimu wa masomo hayo mawili na kocha wa mchezo wa riadhaa. Hata hivyo taarifa hiyo haikutaja idadi ya walimu wa masomo hayo.

Katika matokeo ya kidato cha nne na sita, kumekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaofeli masomo hayo kwa madai kuwa walimu wanaoweza kufundisha masomo hayo ni wachache.
Lakini kibaya zaidi wataalam wa masomo hayo licha ya uchache wao, hawana motisha na ndio sababu yao kutofundisha vizuri na kusababisha matokeo mabaya katika masomo hayo.

Mbali ya makubaliano hayo, nchi hizo mbili zimeahidi kuongeza ushirikiano katika nyanja mbalimbali na kuangalia uwezekano wa Tanzania kufungua aina ya uwakilishi katika Kisiwa hicho cha Caribbean katika miaka miwili ijayo.

Kuhusu kocha wa riadha, Mama Simpson Miller amesema kuwa na hilo halina pingamizi kwa sababu yeye alikuwa Waziri wa Michezo kwa miaka mingi na kuwa kwa sasa Wizara ya Michezo iko kwenye Ofisi yake ya Waziri Mkuu.

“Nilikuwa waziri wa miaka mingi wa michezo katika nchi yangu na kwa sababu ya umuhimu wa michezo, nimeamua kuiweka shughuli ya michezo katika Ofisi yangu ya Waziri Mkuu.”
Jamaica ni moja ya nchi zinazoongoza katika mchezo wa riadha duniani ikiwa imetoa wanariadha wengi mabingwa wa dunia akiwamo bingwa wa sasa wa Olimpiki na dunia katika mbio fupi za mita 100 na 200, Usain Bolt.

Gazeti la Tanzania Daima



 
Ni vizuri kama wataweza kumudu mazingira ya kufundishia ya shule zetu za kata

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nitakachosikitika ni pale hao Mwl toka Jamaica atakuwa analipwa mara 4 ya huyu wa Tz ingawa huyu atakuwa nafanya kazi nzuri kuliko huyo mgeni. Yangu macho.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Yes class, iz evibadi ina di clas?
We gwan learn somting nu today!
..................................
...sd#$%fgdg^YTY..
..................................
Whoz gat weed in here, me iz thursty!

:bange::bange::bange::bange::bange::bange::bange::bange:

Jah Bless!

Hahahaha, tunaomba mno, kila kitu tunaombaomba tu
Cha muhimu sasa naona tumwombe Xi Jinping atusaidie kuongoza mwaka mmoja tuone kama tunaweza kupiga hatua!
 
Hii ni aibu isiyostirika wala kumithilika. Miaka 50 plus baada ya kupata uhuru bado unchi kama nchi imeshindwa kuzalisha walimu wa kutosha kwa ajili ya kufundisha kwenye shule zake? Ni Rais huyuhuyu mwaka 2010 alisema kuwa kufikia 2012 uhaba wa walimu nchini utakuwa historia, leo hii ameenda kuomba Jamaica? Tutafikia mahala tutaanza kuomba hata wanaume kuwatimizia wake zetu
 
Tuliyataka wenyewe haya 2010 tusilalamike.... Hakuna jipya hapo... Nchi itazidi kudumaa kuliko miaka ya 1980 ilivyokuwa

asante awamu ya nne.... Jk hoyeeeeeeeeeeeeeee
 
lakini kama ni akili na utashi wako mh. nakusihi kaa chini utafakari upya huenda uliwaza aidha ukiwa umechoka ama ukiwa na mambo mengi kichwani,

ni kwa nini hiyo fedha isireform taasisi ya elimu na kutoa kupaumbele kwa walimu wa hisabati kwa kuwahakikishia maslahi mazuri?

pili serikali itumie hiyo bajet kama ina nia njema iubomoe mfumo wa elimu na kufanya kazi ya ualimu isiwe wito bali iwe kazi kama kazi zingine maana tafsiri ya wito haipo kwani mwalimu anaonekana ni yule mtu aliyefeli masomo na kukosa pakwenda




Jamaica tena? Au ndio after effects za kubembea? Hawa jamaa watatufundisha kula ndumu kwa staili mpya wakija!
 
Hii tabia ya kuomba omba huwa inanikera.
Ni kipi ambacho sisi hatunacho cha kuweza kuyatimiza hayo bila msaada wa jAMAICA?
Vijana wanakaa kambini 2 weeks kabla ya mashindano alafu utegemee kushinda?
Vijana waliopata DIV 4 ndo waalimu wa watoto wetu ilo nalo waitaji msaada wa Jamaica
Mtihani wa hesabu nao uko na multiple choice
Yote yanawezekana bila msaada wa JAMAICA
 
Ameshindwa kuwalipa waalimu wa hapa nchini hao wa kutoka Jamaica watafundisha bure? Tatizo sio kukosa walimu wa kufundisha hayo masomo tatizo ni huyo Kawambwa wake ameshindwa kuongoza wizara na bado anamg'ang'ania aendelee kuwa waziri!!! Kama anampenda sana basi ampe umeneja wa estate yake huko kwao Msoga kuliko kutuharibia nchi.
 
Ni vizuri kama wataweza kumudu mazingira ya kufundishia ya shule zetu za kata

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums


Hata wakipangiwa kufundisha vyuo vyetu vikuu - achilia mbali shule za kata - hawataeleweka vizuri. My English is reasonably very good but the West Indies accent gives me a lot of trouble to understand. Sembuse hawa wanafunzi wetu wa leo? This is becoming beyond a joke now!
 
Tabia ya kuombaomba ni ugonjwa ambao uko ndani ya damu ya mtu. Kuna watu ambao wako tayari kuomba hata maji machafu mradi tu wawe wameomba.
 
somo la reggae music liingizwe kwenye mtaala plz na bado aombe na mateacher toka mexico nasikia ni wazuri sana kwa marijuana
 
Back
Top Bottom