JK aomba kura, AAHIDI BARABARA YA NJOMBE - MAKETE KUJENGWA KIWANGO CHA LAMI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK aomba kura, AAHIDI BARABARA YA NJOMBE - MAKETE KUJENGWA KIWANGO CHA LAMI

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Boflo, Sep 24, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kikwetechini.jpg
  Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Jakaya Kikwete ,akiwa ameketi chini ardhini kwenye vumbi na nyasi ili kumsikiliza Mama Sara Mageni mkazi wa Wilaya ya Makete, wakati mgombea huyo alipowasili kuhutubia mkutano wa kampeni. Sara alikuwa akitoa shukrani zake kwa Rais
  source: Mwananchi
   
 2. S

  Sylver Senior Member

  #2
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inaitwa gala galauka hiyo !
  watafanya mengi mwaka huu ,ila ndio hivyo karata walizonazo mikononi zote makarasa ,Slaa kashikiria mizingu na madume yote
   
 3. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watafanya wizi wa kura wa hali ya juu ili kuendeleza usanii wao hawana jinsi hata wakijiragaza. Sasa wanapanga mikakati ya wizi mkubwa.
   
 4. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hiyo kampeni ikifika jioni itakuwa ya 'shuka kwa shuka'. Mama Salama amejitakia mwenyewe!
   
 5. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  si kila siku wanatembea kwenye mared carpet hawa.....hapoo imekuwaje tena?
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  hahahah
  nilipoona hii kitu nimecheka sana, anaomba kura kwa nguvu!
   
 7. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mie nadhani ule mzuka wa kudondoka ulikuwa unamuingia akayeyusha kukaa chini. I can see hapo alikuwa anasema "aisee". JK aweza fanya lolote manake usanii anaujua kisawasawa. But haipendizi, it is just too acting, ili watu waseme mtu wa watu? Lol
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Sep 24, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
  Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Jakaya Kikwete ,akiwa ameketi chini ardhini ili kumsikiliza Mama Sara Mageni mkazi wa Wilaya ya Makete, wakati mgombea huyo alipowasili kuhutubia mkutano wa kampeni. Sara alikuwa akitoa shukrani zake kwa Rais Kikwete baada ya kumnunulia Bajaj ili kurahisisha shughuli zake, alipotembelea wilaya hiyo mwaka jana

  Fidelis Butahe, Iringa
  MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete alitumia staili ya aina yake kuomba kura wakati alipolazimika kuketi ardhini ili kumsikiliza mwananchi wakati akiwa kwenye moja ya mikutano ya kampeni za kuomba kura kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31.

  Mbali na tukio hilo, kabla ya kupanda jukwaani mjini Ludewa wilayani Mbalali, Kikwete alikuwa akizungumza na simu na baada ya kumaliza aliwaambia wananchi kuwa alikuwa akizungumza na balozi wa Marekani nchini Tanzania na kwamba balozi huyo amemueleza kuwa Rais Barack Obama ameahidi kuwa serikali yake itaendelea kutoa misaada kwa Tanzania.

  Watu wengi hawakuamini macho yao wakati Kikwete alipoanza kukaa chini kwa ajili ya kumsikiliza mwananchi huyo, Sara Mageni kwenye mkutano wake uliofanyika kwenye Uwanja wa Mabehewa wilayani Makete ambako wakati huu wa majira ya kipupwe vumbi limeshamiri.

  Sara, ambaye ni mlemavu wa miguu, alikuwa akitoa shukrani zake kwa Kikwete ambaye alimnunulia pikipiki ya matairi matatu aina ya Bajaj ili kurahisisha shughuli zake wakati mwenyekiti huyo wa CCM alipotembelea wilaya hiyo mwaka jana.

  Akiwa katika uchangamfu wake wa kawaida na mavazi yake ya CCM, Kikwete aliketi chini kwenye vumbi na nyasi na kumsikiliza Sara na alimuuliza ni hali gani anayokabiliana nayo kwa wakati huo.

  Akiwa wilaya ya Makete, Kikwete amewahakikishia watu wenye ulemavu kuwa mwaka 2010-2015, serikali yake itaendelea kulinda haki za walemavu.

  "Serikali ya CCM inalinda haki za walemavu kutokana na kuridhia haki za kimataifa za walemavu, pia tutajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Njombe-Makete yenye urefu wa kilomita 109," alisema Kikwete.

  Aliongeza kusema: "Kukamilika kwa barabara hii kutasaidia wakulima kusafirisha zao la pareto."

  Kikwete, ambaye anawania kurejea Ikulu kumalizia ngwe ya pili, alisema zao hilo limepata mnunuzi kutoka Marekani hivyo wananchi wa Makete wanatakiwa kutumia fursa hiyo kuimarisha pareto pamoja na kulifufua shamba la Kituro ambalo lilikuwa maarufu kwa ufugaji wa kondoo wa sufi.

  Katika mkutano huo, Kikwete alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Makete, Binilith Mahenge pamoja na wagombea udiwani.

  Akizungumzia ujumbe aliopewa kwenye simu na balozi wa Marekani nchini, Kikwete alisema kuwa amehakikishiwa misaada kuendelea kumiminika Tanzania kutoka taifa hilo kubwa duniani

  "Nilikuwa nazungumza na balozi wa Marekani nchini na amenieleza kuwa rais wa nchi hiyo, Barack Obama akiwa katika mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa alitolea mfano kuwa Tanzania ni nchi inayofuata utawala bora hivyo wataendelea kutusaidia," alisema Kikwete,

  "Maneno haya yanasemwa na Wamarekani sio mimi... watu wanasema tu Marekani, Marekani lakini huo ndio ukweli wenyewe; huo ndio ujumbe niliopata; wameonyesha kutusaidia na watatusaidia,".

  Akiwa Igwachanya, mgombea huyo wa CCM aliahidi kuwa serikali ijayo itaendea kuhamasisha uanzishwaji wa Vyama vya Kuweka na Kukopa (Saccos) ili kuwainua kiuchumi wananchi na kuondokana na umasikini.

  Alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, serikali yake ilihamasisha uanzishwaji wa Saccos hali iliyowawezesha wananchi wengi kupata mikopo na kujiendeleza.

  "Saccos ndio njia zitazowawezesha wananchi wenye kipato cha chini kukopa na kujiendeleza kiuchumi, hivyo tutaenda kuhamamisha uanzishwaji wa Saccos ili wananchi wengi zaidi waweze kujiendeleza," alisema Kikwete.

  "Bila kufanya hivyo, itakuwa vigumu kuwainua wananchi wa chini. Tajiri kama (mwenyekiti wa CCM mkoani Iringa) Deo Sanga akienda benki kukopa Sh400 milioni baada ya saa moja atapatiwa, lakini wewe mwananchi masikini ukitaka hata mkopo wa Sh2,000 itachukua hata miaka 10 na usipate. Hivyo njia ya kuwaokoa ni uanzishwaji wa Saccos," alisema Kikwete.

  Aidha, mgombea huyo wa urais alisema serikali yake ijayo itaanzisha shirika la mazao mchanganyiko, ambalo litawaongezea soko la uhakika wakulima wa mazao mbalimbali.

  "Tulianzisha SGR kwa ajili ya zao la mahindi, lakini sasa tutaanzisha shirika la mazao mchanganyiko ambalo wakulima wa ufuta, maharage, kunde na mengineo wataweza kuuza mazao yao kwa uhakika," alisema Kikwete.

  Source: MWANANCHI.
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Jakaya Kikwete ,akiwa ameketi chini ardhini ili kumsikiliza Mama Sara Mageni mkazi wa Wilaya ya Makete, wakati mgombea huyo alipowasili kuhutubia mkutano wa kampeni. Sara alikuwa akitoa shukrani zake kwa Rais Kikwete baada ya kumnunulia Bajaj ili kurahisisha shughuli zake, alipotembelea wilaya hiyo mwaka jana

  Fidelis Butahe, Iringa
  MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete alitumia staili ya aina yake kuomba kura wakati alipolazimika kuketi ardhini ili kumsikiliza mwananchi wakati akiwa kwenye moja ya mikutano ya kampeni za kuomba kura kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31.

  Mbali na tukio hilo, kabla ya kupanda jukwaani mjini Ludewa wilayani Mbalali, Kikwete alikuwa akizungumza na simu na baada ya kumaliza aliwaambia wananchi kuwa alikuwa akizungumza na balozi wa Marekani nchini Tanzania na kwamba balozi huyo amemueleza kuwa Rais Barack Obama ameahidi kuwa serikali yake itaendelea kutoa misaada kwa Tanzania.

  Watu wengi hawakuamini macho yao wakati Kikwete alipoanza kukaa chini kwa ajili ya kumsikiliza mwananchi huyo, Sara Mageni kwenye mkutano wake uliofanyika kwenye Uwanja wa Mabehewa wilayani Makete ambako wakati huu wa majira ya kipupwe vumbi limeshamiri.

  Sara, ambaye ni mlemavu wa miguu, alikuwa akitoa shukrani zake kwa Kikwete ambaye alimnunulia pikipiki ya matairi matatu aina ya Bajaj ili kurahisisha shughuli zake wakati mwenyekiti huyo wa CCM alipotembelea wilaya hiyo mwaka jana.

  Akiwa katika uchangamfu wake wa kawaida na mavazi yake ya CCM, Kikwete aliketi chini kwenye vumbi na nyasi na kumsikiliza Sara na alimuuliza ni hali gani anayokabiliana nayo kwa wakati huo.

  Akiwa wilaya ya Makete, Kikwete amewahakikishia watu wenye ulemavu kuwa mwaka 2010-2015, serikali yake itaendelea kulinda haki za walemavu.

  "Serikali ya CCM inalinda haki za walemavu kutokana na kuridhia haki za kimataifa za walemavu, pia tutajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Njombe-Makete yenye urefu wa kilomita 109," alisema Kikwete.

  Aliongeza kusema: "Kukamilika kwa barabara hii kutasaidia wakulima kusafirisha zao la pareto."

  Kikwete, ambaye anawania kurejea Ikulu kumalizia ngwe ya pili, alisema zao hilo limepata mnunuzi kutoka Marekani hivyo wananchi wa Makete wanatakiwa kutumia fursa hiyo kuimarisha pareto pamoja na kulifufua shamba la Kituro ambalo lilikuwa maarufu kwa ufugaji wa kondoo wa sufi.

  Katika mkutano huo, Kikwete alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Makete, Binilith Mahenge pamoja na wagombea udiwani.

  Akizungumzia ujumbe aliopewa kwenye simu na balozi wa Marekani nchini, Kikwete alisema kuwa amehakikishiwa misaada kuendelea kumiminika Tanzania kutoka taifa hilo kubwa duniani

  "Nilikuwa nazungumza na balozi wa Marekani nchini na amenieleza kuwa rais wa nchi hiyo, Barack Obama akiwa katika mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa alitolea mfano kuwa Tanzania ni nchi inayofuata utawala bora hivyo wataendelea kutusaidia," alisema Kikwete,

  "Maneno haya yanasemwa na Wamarekani sio mimi... watu wanasema tu Marekani, Marekani lakini huo ndio ukweli wenyewe; huo ndio ujumbe niliopata; wameonyesha kutusaidia na watatusaidia,".

  Akiwa Igwachanya, mgombea huyo wa CCM aliahidi kuwa serikali ijayo itaendea kuhamasisha uanzishwaji wa Vyama vya Kuweka na Kukopa (Saccos) ili kuwainua kiuchumi wananchi na kuondokana na umasikini.

  Alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, serikali yake ilihamasisha uanzishwaji wa Saccos hali iliyowawezesha wananchi wengi kupata mikopo na kujiendeleza.

  "Saccos ndio njia zitazowawezesha wananchi wenye kipato cha chini kukopa na kujiendeleza kiuchumi, hivyo tutaenda kuhamamisha uanzishwaji wa Saccos ili wananchi wengi zaidi waweze kujiendeleza," alisema Kikwete.

  "Bila kufanya hivyo, itakuwa vigumu kuwainua wananchi wa chini. Tajiri kama (mwenyekiti wa CCM mkoani Iringa) Deo Sanga akienda benki kukopa Sh400 milioni baada ya saa moja atapatiwa, lakini wewe mwananchi masikini ukitaka hata mkopo wa Sh2,000 itachukua hata miaka 10 na usipate. Hivyo njia ya kuwaokoa ni uanzishwaji wa Saccos," alisema Kikwete.

  Aidha, mgombea huyo wa urais alisema serikali yake ijayo itaanzisha shirika la mazao mchanganyiko, ambalo litawaongezea soko la uhakika wakulima wa mazao mbalimbali.

  "Tulianzisha SGR kwa ajili ya zao la mahindi, lakini sasa tutaanzisha shirika la mazao mchanganyiko ambalo wakulima wa ufuta, maharage, kunde na mengineo wataweza kuuza mazao yao kwa uhakika," alisema Kikwete.

  Chanzo:JK aomba kura, AAHIDI BARABARA YA NJOMBE - MAKETE KUJENGWA KIWANGO CHA LAMI
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Jamani kuweni AWARE sana na hizi tatics zao.
  Unajua hata shetani hutumia kila aina ya ghiliba ionekane kwamba dhambi unayotarajiwa kufanya ina maslahi mema (KWAKO) lakini mwishowe unakuja kujuta.

  Mbinu hizi za kupiga magoti, kushuka down to earth, bonanza ya kuzuia misafara ni one of the tricks in the stock of the.......

  STUKA.
  ZIKEMEWE na wananchi waelezwe kwamba hiyo ni ghiliba kwani wao ndio watakaopiga magoti na kukaa chini another five years za ukata na majanga
   
 11. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nimeisikia BBC leo asubuhi mama salma sasa ni kitanda kwa kitanda

  Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi alipoulizwa kama ni rushwa hiyo alicheka na kusema utakavyotafsiri wewe
   
 12. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  PJ ....kitanda kwa kitanda ee!

  (mie sijaona vipi inaweza kuwa rushwa japo kuwa kimaadili haipendezi kutamka maneno hayo)
   
 13. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hivi hiyo barabara ndiyo anaiona leo? Miaka yote alikuwa wapi?
   
 14. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  hapo sio kwamba anaonesha unyenyekevu ila ukweli ni kwamba alizidiwa na ule ugonjwa wake akaona apumzike kwa kukaa chini.
   
 15. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  Safari hii utaosha hadi vyombo na kura asipewe
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Sep 24, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Inawezekana!
   
 17. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mimi nashangaa sana mikoa kama Lindi, Mtwara na KUNYUMBA (HOME) Ruvuma tuko nyuma saaaaaaaaaaaana, lkn ndo ngome kubwa ya CCM, sijui tumelogwa agrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr. hiyo barabara ya makete Njombe miaka yote wananchi wanateseka eti leo hii wananchi wanaahidiwa kujengwa, wao wanashangilia wanaona kama wamefanyiwa favour kumbe ni haki yao ya kimsingi tena wamecheleweshewa maendeleo. aaagh wa BONGO tuamke jamani......................
   
 18. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Safi raisi wetu kikwete,mungu akusaidie ukipata urais utimize ahadi zako watendaji wako wasikuangushe kama walivyokuangusha miaka tano unayoimaliza.
   
 19. R

  Rayase Member

  #19
  Sep 24, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Phd utani umezidi
  Nimecheka kwelikweliii
   
 20. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ..........well said
   
Loading...